Matembezi ya kuwatembelea vijana/wananchi wenzangu wa wilaya ya Ilala

Apr 11, 2024
19
52
Nilifanikiwa Kutembelea Baadhi Ya Wananchi Wa Wilaya Ya Ilala, Kutoka Kata Ya Kivule, Ili Kujua Maendeleo Ya Wananchi wa Wilaya Yetu Ya Ilala.

Katika Matembezi Haya, Nilifanikiwa Kujua Mafanikio Yaliyofikiwa Na Serikali Ya Chama Cha Mapinduzi Kwa Wananchi Wake, Changamoto, Pamoja Na Mapendekezo Ya Wananchi Kwa Serikali Yao.

Mpaka Sasa, Wananchi Wananufaika Na Mazingira Ya Fursa Mbalimbali Za Kiuchumi, Ikiwemo, Uwezeshwaji wa Vijana Wengi Kuingia Kwenye Biashara Ya Bodaboda Na Bajaji. Uwepo wa Usalama Kwenye Maeneo Yao. Pamoja Na, Upatikanaji wa Huduma Za Kijamii, Kama; Maji, Elimu, Na Huduma Za Afya.

Lakini Pia Nilipata Nafasi Ya Kujua Changamoto Wanazokabiliana Nazo, Ikiwa Ni Pamoja Na;
  • Ukosefu wa BARABARA, Inayowaingiza Kwenye Gharama Kubwa Ya Maisha, Ugumu Katika Kuendesha Shughuli Zao Za Kila Siku, Pamoja Na Kuchochea Uvunjifu wa Ndoa Zao.
  • Mgawanyo wa Leseni Katika Biashara Ya Aina Moja.
  • Ukubwa wa Gharama za Leseni na Ulipaji wa Kodi; Hususani Kwa Wafanyabiashara Wanaoanza Biashara, Lakini Pia, Uwepo wa Kodi Kubwa Tofauti, na Hadhi Ya Biashara/Mapato, Ya Muuzaji/Mfanyabiashara.
  • Maboresho Ya Soko La Biashara, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuboresha Mazingira Ya Soko.
  • Uwepo wa Gharama Kubwa Za Kuunganisha Umeme, Zinazokwamisha Baadhi Ya Watu Kushindwa Kuunganisha Umeme, Mf; Nyumba za Chumba Na Sebule.

Lakini Pia, Walishauri Mapendekezo Yao Kwa Serikali, Ikiwa Ni Pamoja Na;
  • Uwepo wa Barabara Ya Kiwango cha Lami, Ambayo Itasaidia Kuchochea Ukuaji wa Uchumi, Ikiwa Ni Pamoja Na Kurahisisha Kuendesha Shughuli za Kiuchumi.
  • Gharama za Ulipaji wa Kodi na Leseni, Uendane na Hadhi Ya Biashara Husika, Na Wafanyabiashara Wadogo, Kupewa Muda Kidogo wa Kujiimarisha Kibiashara.
  • Kuwepo Na Leseni Moja Kwa Aina Moja Ya Biashara
  • Kupatiwa Mashine za Risiti Kwa Gharama Nafuu, Ili Kuchochea Matumizi Ya Mashine Ya Risiti Kwa Ukubwa, Na Kuchangia Mapato Kwa Serikali.
  • Uwepo wa Unafuu wa Uunganishwaji wa Umeme, Kwa Kuzingatia Ulipaji wa Kodi Ya Pango Hulipwa Moja Kwa Moja Kutoka Kwenye Bili Ya Umeme, Hivyo Punguzo La Uunganishaji, Utachochea Ongezeko La Walipa Kodi Ya Pango, Kutokana na Upatikanaji wa Umeme Kwa Gharama Nafuu.

Ni Matumaini Yangu, Serikali Yetu Sikivu Ya Chama Cha Mapinduzi, Itaenda Kutatua Changamoto Hizo, Ikiwemo Changamoto Ya Barabara, Ambayo Tayari Ipo Kwenye Ilani, Ikisubiri Kutengwa Kwa Bajeti Ya Ukamilisho Wake.

Ulikuwa Wakati wa Kujenga.

#KaziInaendelea 🇹🇿
 

Attachments

  • 11EA5C64-8C24-47F1-9665-FAECBDF06018.jpeg
    11EA5C64-8C24-47F1-9665-FAECBDF06018.jpeg
    6.3 MB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom