Marekani yapiga marufuku bidhaa za nguo za viwanda 26 vya China.

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
13,128
15,599
Marekani ilisema Alhamisi inazuia uagizaji kutoka kwa kampuni kadha za nguo za China, ikitaja wasiwasi wa China kutumia nguvu kazi ya kulazimishwa katika utengenezaji bidhaa.

Kati ya nyongeza 26 mpya kwenye orodha ya taasisi ya Sheria ya Kuzuia Kazi ya Kulazimishwa ya Uyghur, 21 zilichukuliwa kuwa chanzo na kuuza pamba kutoka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Xinjiang wa China kwenye soko la jumla.

Wengine watano pia walipatikana kununua pamba kutoka mkoa huo.

US bars imports from 26 Chinese textile firms over forced labor.

US bars imports from 26 Chinese textile firms over forced labor
 
China wameshatoboa kimaisha marekani anajichosha tu
Watauza wapi nguo hizo? una kupoteza ajira hapo, si rahisi unavyofikiria.......Kuna kiwanda cha nguo cha mabibo kilikuwa cha serikali, soko la products za kiwanda hicho lilikuwa jeshi la marekani.

Sikumbuki kilitokea nini, USA ikasimamisha ununusi wa nguo hizo na kiwanda kikafa mpaka leo. Nilikuwa na dada yangu tumbo moja anafanya kazi pale.....hivyo hii ni story ya kweli...alipoteza ajira na wengine wengi mpaka leo kikafa kabisa.
 
Sio sitoboi tu, nani anataka kuvaa manguo ya dukani yamefanana kila kona?

Pili Mitumba ni Affordable kwa watanganyika wengi
Kariakoo mbona nguo zipo bei rahisi tu! Kuna mkenge nilitaka kuuva wa kuuziwa mashati bei ya kuruka, kwenda Kariakoo nikakuta hayo hayo niliyoambiwa 22k yanauzwa 12k kama ukichukua kuanzia matatu!😁😁
 
Watauza wapi nguo hizo? una kupoteza ajira hapo, si rahisi unavyofikiria.......Kuna kiwanda cha nguo cha mabibo kilikuwa cha serikali, soko la products za kiwanda hicho lilikuwa jeshi la marekani.

Sikumbuki kilitokea nini, USA ikasimamisha ununusi wa nguo hizo na kiwanda kikafa mpaka leo. Nilikuwa na dada yangu tumbo moja anafanya kazi pale.....hivyo hii ni story ya kweli...alipoteza ajira na wengine wengi mpaka leo kikafa kabisa.
Cha pale epz?..nilisikia kinauza nguo ulaya,ikiwemo jerseys kwa timu mbalimbali
 
Marekani ilisema Alhamisi inazuia uagizaji kutoka kwa kampuni kadha za nguo za China, ikitaja wasiwasi wa China kutumia nguvu kazi ya kulazimishwa katika utengenezaji bidhaa.

Kati ya nyongeza 26 mpya kwenye orodha ya taasisi ya Sheria ya Kuzuia Kazi ya Kulazimishwa ya Uyghur, 21 zilichukuliwa kuwa chanzo na kuuza pamba kutoka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Xinjiang wa China kwenye soko la jumla.

Wengine watano pia walipatikana kununua pamba kutoka mkoa huo.

US bars imports from 26 Chinese textile firms over forced labor.

US bars imports from 26 Chinese textile firms over forced labor
Haina shida US wasiponunua wapalestina, wairan, wayemen, walebanon, wapo watanunua
 
Mchina alipofikia naona ana lift juu middle finger kwa EU,Japan na US.
Kuna hizi gari zao zinaitwa Nio za umeme, kuna model moja inaitwa ET9, ile gari jamaa walipanga glass nyingi juu ya bonet kwa kuzibebanisha, halafu zile glass zikawekewa mvinyo, chuma ikawashwa ikawa inapita kwenye bumps, hakuna hata glass moja imemwaga mvinyo ukiachilia kuangusha glass.

Ikachukuliwa benz s class inayosifika kwa comfo ikawekewa glass vile vile ikaanza kupita juu ya bumps, zile glass zote zimevunjika.

Nakumbuka hili jaribio walifanya Lexus lakinj gari iliwekwa kwenye dyno haikuwa inatembea.

Hio Nio ET9 comfortability yake ni next level mzee, ni noma na nusu mi mwenyewe nilisema kwa hizi level mchina amefikia amezidi kiburi na dharau sasa ni bora EU na US wamvamie na kumtandika tu kwa maana hamna namna, vijamaa vimekuwa too much na tishio.

View: https://youtu.be/WEr_sNp7XLM?si=2M7C0-0xXr3DhoG5
vehicle-platform-hero-desktop.jpg
 
Marekani aliwashinikaza VW kuwa viwanda vya joint ventures kati ya Mchina na Ujerumani vya FAW-VW na JAC-VW vilivyopo Xinjiang pia vifungwe kwa sababu ya utumikishwaji na ukiukwaji wa haki za binadamu

VW wakaenda hadi Xinjiang hawakukuta madai ya Marekani kuwa ni ya kweli

Marekani akazuia magari yaliyotengenezwa kati ya joint venture ya FAW-VW kutoka Xinjiang China.
 
Back
Top Bottom