KERO Malori yanaegeshwa karibu na makazi ya watu Tabata, yanaharibu barabara na kuvamia maeneo ya wazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Insidious

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
610
837
Kumekuwa na ongezeko ya idadi kubwa ya malori yanayopaki ama kuegeshwa katika mitaa ya tabata mfano; mtaa wa shule ya st.mary’s na NSSF huku malori hayo ikileta maafa yafuatayo;

1. Kuharibu barabara

2. Kuziba njia kwa kupaki vibaya au kuharibika pamoja na kuziba njia zilizokuwepo hapo awali

3. Uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele na uchafu (oil)

4. Kuvamia maeneo yaliyotengwa kama maeneo ya wazi

Hivyo; tunaomba mamlaka husika iweze kushughulikia jambo hili.
 
Kwa kweli ni kero kubwa Sana karibia barabara Zote iwe Nelson Mandela , Bagamoyo Rd, Shekilango, Morogoro Rd
 
Nchi haina sheria wala taratibu hii. Inajiendesha yenyewe yaani iko ktk autopilot
 
Back
Top Bottom