Mimi kwa uzoefu wangu wa kesi za jinai na madai, naona kuna vitu vya kisheria vitajitokeza au kuibuliwa kabla ya kesi ya msingi maana hatujui Kabendera atafungua Shauri la kudai fidia la aina gani. Je, ni la madhara ya kimadai? (Tortious Liability), je ni madhara ya kijinai? (Criminal Liability and Tresspass to person).
Mdai atakuwa na ushahidi gani iwapo Vodacom wanao utetezi wa kutakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi au Takukuru au TISS kumtia nguvuni mtuhumiwa wa uhalifu. Ndiyo awali niliona umuhimu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kuunganishwa. Hata hivyo linaweza kuzuka swali mahakamani namna AG au Serikali itakavyounganishwa. Mdai akiomba kurekebisha hati ya mashitaka kumuingiza AG, ataambiwa kuishitaki Serikali lazima kuanza na notisi ya siku 90 hivyo mashitaka yaondolewe yote akaanze upya. Atakapoanza na hiyo notisi, atapigwa PO (Preliminary Objection on Point of Law) kwamba kesi za madhara (law of tort) hufunguliwa Mahakama Kuu ndani ya miaka mitatu tangu madhara yapotokea.
Kwa Wakili wa Serikali na Wakili wa Vodacom ataomba mahakama iondoe àu kufuta hiyo kesi kwani ni imepitwa na muda (the suit is time barred). Maana ktk hali halisi tangu 2019 to 2024 ni zaidi ya miaka mitatu. Mdai na wakili wake wanaweza kuomba kuongezewa muda na kuzingatia muda uliopotea wakati akiwa mahabusu gerezani. Kwa hiyo, Wakili Madeleka na Mteja wake Kabendera, watakutana vikwazo vingi vya kiufundi (legal technicalities) vya namna hiyo. Kuna kuchoshana kwa mapingamizi mengi ya kisheria wakati shauri la msingi linasumama kuanza.
Halafu kwa kumbukumbu zangu Vodacom haijawahi kushindwa kesi za namna hii kwani ina misuli ya kifedha na wanahisa wazito wafanyabiashara wakubwa na viongozi wastaafu wazito wenye ushawishi mkubwa!!!
AAK Jnr, SC, Esq.
27th April 2024
19:42 Hrs EAT
Pia soma: Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019