Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,820
4,573
Mwandishi wa Habari, ERICK KABENDERA ameitaka Kampuni ya Simu ya VODACOM TANZANIA kumlipa USD 1,000,000 MILIONI ndani ya SIKU 14 kwa Kufanikisha kutekwa kwake mwaka 2019.

Amefanya hivyo kupitia kwa WAKILI wake Peter Madeleka.

IMG_20240426_103704_284.jpg


PIA, SOMA:
-
Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano
 
Ni jambo jema kuwajibisha makampuni yanayosababisha kadhi kwa raia kukumbushwa wajibu wao kwa raia kwa mujibu wa sheria na kukataa kupindisha jambo lolote kisa kampuni ilitishiwa au inataka kuwafurahisha wanasiasa.

Akifanikiwa huyu raia mwenzetu basi makampuni yatakuwa yanawaheshimu raia ambao ni wateja wao kwa kuzingatia sheria masharti na vigezo kama kila siku wanavyosisitiza wakiingia mkataba wa kutoa huduma au kuuza bidhaa yao maneno sheria, masharti na kanuni ktk maandishi madogo husisitizwa sana ndani ya matangazo.

Sheria ni msumeno wanasema katika semi za wahenga, tusubiri mahakama itatafsiri nini kuhusu maneno hayo makampuni husisitiza katika mikataba yao na customers (wateja/ walaji)
 
Back
Top Bottom