Mada: Fahamu mambo mbalimbali kuhusu gari aina ya Subaru Forester

Subaru forester za SH 5 ziko aina 4 zenye engine ya 2000cc na 2500cc
1. Forester x hii haina fog lights, mziki ni wa kawaida, dash board ni full plastics na haina rear spoiler, haina alloy wheels

2. Forester Xs hii ina fog lights, rear spoiler, mziki umeboreshwa hasa speakers, na kwenye redio pale pamerembwa na bodi ya mbao, ina cruise control, alloy wheels

3. Forester Xs premium hii ina sifa zote za Xs hapo juu na kuongezeka kwa sunroof, leather seat, taa kali na interior imeboreshwa

4. Forester Xt hii ina sifa zote za Xs ila imeongezewa turbo
asante mangi
 
Wakuu msaada hapo,interms of fuel consumption, spear na kuhimili mikiki ya barabara mbovu!
Forester ni gari nzuri sana kuhimili
Wakuu msaada hapo,interms of fuel consumption, spear na kuhimili mikiki ya barabara mbovu!
Forester ni gari nzuri na imara ..kwenye offroad pia ipo vzuri
shida ni running cost yake ipo juu interms of fuel na spare parts pia
 
Kweli tunatofautiana, hii chuma siielewi kabisa.

Ulishawahi kuwa nayo au unahisi kwa kuiona tuu? Kuna kitu unasahau , ni gari ya bei rahisi yenye nguvu, speed na imara.. naona unafananisha sijui na v8 hayo ni matambo tuu ya sisi vijana ila usisahau hii mada ni ya Subaru’s..japo usisahau ukiweza manage kuitunza subaru ni rahisi sana ku manage v8
 
Ulishawahi kuwa nayo au unahisi kwa kuiona tuu? Kuna kitu unasahau , ni gari ya bei rahisi yenye nguvu, speed na imara.. naona unafananisha sijui na v8 hayo ni matambo tuu ya sisi vijana ila usisahau hii mada ni ya Subaru’s..japo usisahau ukiweza manage kuitunza subaru ni rahisi sana ku manage v8
Siipendi niwe nayo vipi tena..
 
Kwa niaba ya watu wengine.. kubali kusikiliza ya wanaokwambia subaru nimekaa nayo miaka bila kwenda garage au sikiliza uhalisia.
Gari zote ni nzuri lakini kuna competitive advantage ya nyingine. Mtu anakwambia nafunga oil filter ya subaru 35,000 nasahau nani kakwambia wamili wa toyota wanafunga oil filter kila siku? Oil filter 10k na unaenda nayo service to service.

Ni kweli subaru tena upate yenye ej20 au ej25 zina performance nzuri lakini achana na maneno ya V8 ilisoma namba performance haipimwi na mtu ambae hajui mnashindana. Kufanya service ya subaru inahitaji mtu mwenye kipato cha kuifanya gari yake iishi vizuri Subaru sio gari imara ndo maana haiwezi handle service za mtaani kama toyota na naona watu wanazidi comment ati subaru ni reliable kuliko rav4 nendeni mtaani mkaone hizo fozzy zilifokufa engine na rav4 zinavodumu misukosuko.

Kingine ni sawa zipo rav4 full time 4wd lakin AWD ya forester ni bora sana na inaweza kukuhakikishia kutatua changamoto nyingi kwenye barabara kuliko rav4. Twende kwenye performance toyota wana engine ngumu na imara za kumudu stress kama hitting redline na kuna emgine zilisukwa zinakubali na kuhandle stress za nguvu kubwa unlike subaru chezea redline ununue engine mpya, mod gari yako uihesabie siku za kuendesha. Maamuzi ni yako.
Umekata hamu yote ya Subaru hapa
 
Mkuu bado huna vitu huvielewi.

Turbo inapunguzaje ulaji wa mafuta kwenye gari?

Audi A4 1.8L ina turbo ila ina the same fuel consumption na Audi A4 2.0L. Hapo turbo imesaidiaje?

1HZ ni pure mechanical wakati 1HDT ina mifumo mingi ya umeme na electronic.

Mfano wa Mwisho 1az-fse na 1az-fe ni engine ambazo zina displacement sawa ila zina fuel consuption tofauti hata kama zimefungwa kwenye gari moja.

1az-fse ni D4 hivyo mafuta yanaingia direct kwenye engine. Engine inarun leaner na inatumia mafuta kidogo.

Utofauti wa technology moja ya direct injection umefanya 1az-fse kuwa na matumizi mazuri ya mafuta kuliko 1az-fe.
Mmmh!tukukubalie wewe tuachane na wataalamu?mkuu usilazimishe hoja yako iwe ya nguvu.
 
Gharama ya Subaru Forester XS na XT kwa sasa ni kiasi hadi mkononi .
Naona kupata ufafanuzi wa namna ya kujua gharama.

Second generation.
 

Attachments

  • Screenshot_20230624-183627~2.png
    Screenshot_20230624-183627~2.png
    197.7 KB · Views: 62
  • Screenshot_20230624-183533~2.png
    Screenshot_20230624-183533~2.png
    226.6 KB · Views: 63
Back
Top Bottom