Kwenye Vyakula na Mapishi bora 50, Tanzania hatumo

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Kwangu mambo yote ni shega tu!

Nimeshangaa eti Tanzania hatumo kwenye haka ka listi ka misosi yenye unyama mwingi duniani!.

Yawezekana tumefanyiwa tu fitina.

Ina maana hawa waliotoa haka ka listi walijui Zege? (CHIPS MAYAI) au (WALI MAHARAGE)?

20240310_224808.jpg
 
Kama nchi haifahamiki na mambo yake hayafamiki. Watu hawajui kabisa kama TZ ina exist let alone mapishi yake.
Mapishi yetu ni Yapi? Sisi wenyewe hatuyapendi, Chipsi, Wali, biriani, Maharage, mchuzi wa nyama etc vyakula ambavyo ni common asili yake sio Tanzania.

Vyakula vya asili kama kisusio, muhogo wa Nazi, Ugali sijui wa mtama na vinginevyo hapa Tanzania kwenyewe sio maarufu.
 
Naweza kukubaliana nao, ila sio Tz tu ngozi nyeusi kwa kifupi swala la msosi wenye ladha nzuri bado sana ukilinganisha na race zingine.
Hio list inahusu Africa tu, Ethiopia hapo ana mapishi kama 6, South kama 10, kuna Nigeria etc.
 
Hio list inahusu Africa tu, Ethiopia hapo ana mapishi kama 6, South kama 10, kuna Nigeria etc.
Hiyo namba bado ni ndogo sana mkuu, pia haiwezi kuondoa ukweli.
Sisi tunajivunia chakula chenye virutubisho vingi ila kwenye suala la ladha nzuri kuna mengi ya kujifunza.
 
Hiyo namba bado ni ndogo sana mkuu, pia haiwezi kuondoa ukweli.
Sisi tunajivunia chakula chenye virutubisho vingi ila kwenye suala la ladha nzuri kuna mengi ya kujifunza.
Haya machips kuku tu nayo kula utahesabu nayo kama vyakula vya virutubisho?

Ukumbuke mtalii akija nchi hii akitaka hotel ya kula ugali wa mtama ama wa muhogo hapati, atapata tu vyakula ambavyo asili yake sio Tanzania, Chapati, fried rice na Wali wa aina zingine, sisi wenyewe hatuthamini vyakula vyetu hivyo vimekua ni nadra kuipata na kukosa exposure.
 
Ni kwasababu wenyeji pia wanapenda vyakula vyenye ladha nzuri bila kuzingatia ubora wa hicho chakula kwenye mwili.

Mi nafikiri kuna namna inahitajika kuongeza ubunifu kwenye hivi vyakula asili ili vijitangaze vyenyewe maana ladha nzuri na ubora ni vitu vinavyopaswa kuendana kwenye chakula.
 
Back
Top Bottom