Kweli nimeamini elimu tuliorithi kutoka kwa wakoloni ni chanzo cha umasikini mkubwa sana Tanzania na Afrika kwa ujumla wake

Mzee wa old school

JF-Expert Member
May 16, 2021
578
919
Jana jioni kabla ya usingizi nilikuwa natafari kwa kujilaumu na kulalama... Nakuona kuwa maisha ni magumu sana, niliumia zaidi kuona watoto na mke wananitegemea, wazazi pia tena zaidi wanaamini kijana wetu msomi... Daaaah!

Nikapiga hesabu muda niliotumia shule... Miaka 7 msingi + miaka 4 sekondari + jumlisha miaka 3 diploma au 2 kwa kidato cha sita + 3, 4 au 5 degree kutegemea na course uliyo soma.

Sasa hapa tufanye mtu kapita form six 2 miaka na chuo miaka 3
7+4+2+3= 16
Tufanye umeanza shule na miaka 7.. sasa hiyo 7+16 = 23.

Hebu fikiria hadi unamaliza shule una miaka 23... Hujaanza maisha zaidi ya kujitia msomi, huna maarifa ya kazi za mikono kwa madai ya kwamba hizo kazi za wasio soma.... Sasa sisi TULIO soma tunajua nini? Tunajua newton law? Archimedes principle? Historia ya wazungi kuja kututawala?

Turejee kwenye mada... Sasa umri huo wa miaka 23 kijana deni board ya MKOPO limefika mil 25, Hana kazi, Hana mbele wa nyuma... Kapambana hapa na pale anakuja kupata kazi ana miaka 30 hadi 35..... Ndo anaanza life... Ile mshahara unsingia tu... Panga linapita shwaaa! Bodi ya MKOPO..... Mshahara anaanza kupokea nusu.. mara huku pay as you earn, mara chama cha wafanya kazi n.k,, kuja kushtuka umri umeenda kabakiza miezi 2 astahafu...

PENDEKEZO/TUJIULIZE
1.Kwanini serikali isupunguze muda wa wanafunzi kukaa mashuleni?

2. Kwanini wizara husika isibadili mtaala wa elimu?

Vyote viwili ni muhimu.
Tuanze na 1. Muda wa miaka kwa wanafunzi upungue kukaa mashuleni.. badala ya miaka 16 walau basi miaka 10.

Badala mtoto aanze shule ya msingi miaka 7 basi aanze na miaka 4, yaani miaka 4 chekechea akiwa na 5 anaanza shule ya msingi. Hadi miaka 8 kamaliza shule ya msingi, miaka 11 kamaliza sekondari baada ya hapo college ama chuo cha kati kusoma ujuzi miaka 2 na akitaka degree sasa hapo ndo yeye miaka 3 na kuendelea... Akimaliza college ana miaka 13 walau ana muda wa kujitafuta na kama akiendelea degree atamaliza na miaka ,16 walau bado tena ana muda.. na zile kozi za miaka kama udaktari atamaliza akiwa na miaka 18 bado muda anao....

Kwa minajiri hiyo basi, miaka ya madarasa iwe hivi.
*Chekechea mwaka 1
*Msingi miaka 4
*Sekondari 3
*Chuo cha kati yaani college miaka 2
* Chuo kikuu miaka 3 hadi 5

Jambo la 2. Kwa nini wizara husika isibadili mtaala wa elimu? Badala watu kusoma nadharia wasomee wakiwa karakana, mahospitali, mahakamani, viwandani, masomoni n.k? Kama ni historia basi tusome historia yetu ya kweli.... Yenye asili yetu! Badala ya kusoma dawa za wazungu... Kwa nini tusitumie miti Mungu alotupatia tuongeze elimu ya madawa na matibabu ya kikwetu? Kwanini China Russia waliweka utaratibu wao na waliweza?

Hebu viongozi fikirieni nje ya box....

Mfano wa kweli: siku moja shileni kwetu wazungu kutoka nchi Fulani walitutembelea(maana ile ilikuwa shule ya diocese Fulani) katika kujitambulisha kuna mmoja alisema wasifu wake kwamba anasoma masters ya chemistry halafu alikuwa na miaka 18... Wakati shileni kuna mijamaa ipo form ina miaka 18 na mengine form 6 ina miaka 19 hadi 20....

Ni hayo tu.... Moderator wakati mwingine huwa anaficha post zangu watu hawaoni... Basi naomba huu muuruhusu
 
Elimu ya Tz inamfanya kijana achelewr sana kujitambua na kujua nini anataka maishani.

Wazazi hawawaandai watoto bali nao hutegea shule pekee ndio ziwaandalie watoto kua vile wazazi wanategemea watoto wawe.

Mzazi anatamani mwanae awe daktari/engineer nje ya kumpeleka shule hamna kitu mzazi anafanya kutimiza hizo ndoto zake/za mwanae.

Mbaya zaidi ni kua baadhi ya wazazi hawajui hata wafanye nini!!

Matokeo yake, ikitokea bahati mbaya mtoto kashindwa kwenda form 5 kwasababu ya matokeo yake, mzazi atakomalia huyu dogo arudie mtihani tena na tena mpaka aende form 5, wakati options nyingine zipo!!

Dogo atarudia sana mitihani, mpaka afike chuo tayar ashakua jitu zima +25yrs, hapo anakua anaangilia tu course itakayofanya apate ajira na sio tena zile ndoto zake.
 
Jana jioni kabla ya usingizi nilikuwa natafari kwa kujilaumu na kulalama... Nakuona kuwa maisha ni magumu sana, niliumia zaidi kuona watoto na mke wananitegemea, wazazi pia tena zaidi wanaamini kijana wetu msomi... Daaaah!

Nikapiga hesabu muda niliotumia shule... Miaka 7 msingi + miaka 4 sekondari + jumlisha miaka 3 diploma au 2 kwa kidato cha sita + 3, 4 au 5 degree kutegemea na course uliyo soma.

Sasa hapa tufanye mtu kapita form six 2 miaka na chuo miaka 3
7+4+2+3= 16
Tufanye umeanza shule na miaka 7.. sasa hiyo 7+16 = 23.

Hebu fikiria hadi unamaliza shule una miaka 23... Hujaanza maisha zaidi ya kujitia msomi, huna maarifa ya kazi za mikono kwa madai ya kwamba hizo kazi za wasio soma.... Sasa sisi TULIO soma tunajua nini? Tunajua newton law? Archimedes principle? Historia ya wazungi kuja kututawala?

Turejee kwenye mada... Sasa umri huo wa miaka 23 kijana deni board ya MKOPO limefika mil 25, Hana kazi, Hana mbele wa nyuma... Kapambana hapa na pale anakuja kupata kazi ana miaka 30 hadi 35..... Ndo anaanza life... Ile mshahara unsingia tu... Panga linapita shwaaa! Bodi ya MKOPO..... Mshahara anaanza kupokea nusu.. mara huku pay as you earn, mara chama cha wafanya kazi n.k,, kuja kushtuka umri umeenda kabakiza miezi 2 astahafu...

PENDEKEZO/TUJIULIZE
1.Kwanini serikali isupunguze muda wa wanafunzi kukaa mashuleni?

2. Kwanini wizara husika isibadili mtaala wa elimu?

Vyote viwili ni muhimu.
Tuanze na 1. Muda wa miaka kwa wanafunzi upungue kukaa mashuleni.. badala ya miaka 16 walau basi miaka 10.

Badala mtoto aanze shule ya msingi miaka 7 basi aanze na miaka 4, yaani miaka 4 chekechea akiwa na 5 anaanza shule ya msingi. Hadi miaka 8 kamaliza shule ya msingi, miaka 11 kamaliza sekondari baada ya hapo college ama chuo cha kati kusoma ujuzi miaka 2 na akitaka degree sasa hapo ndo yeye miaka 3 na kuendelea... Akimaliza college ana miaka 13 walau ana muda wa kujitafuta na kama akiendelea degree atamaliza na miaka ,16 walau bado tena ana muda.. na zile kozi za miaka kama udaktari atamaliza akiwa na miaka 18 bado muda anao....

Kwa minajiri hiyo basi, miaka ya madarasa iwe hivi.
*Chekechea mwaka 1
*Msingi miaka 4
*Sekondari 3
*Chuo cha kati yaani college miaka 2
* Chuo kikuu miaka 3 hadi 5

Jambo la 2. Kwa nini wizara husika isibadili mtaala wa elimu? Badala watu kusoma nadharia wasomee wakiwa karakana, mahospitali, mahakamani, viwandani, masomoni n.k? Kama ni historia basi tusome historia yetu ya kweli.... Yenye asili yetu! Badala ya kusoma dawa za wazungu... Kwa nini tusitumie miti Mungu alotupatia tuongeze elimu ya madawa na matibabu ya kikwetu? Kwanini China Russia waliweka utaratibu wao na waliweza?

Hebu viongozi fikirieni nje ya box....

Mfano wa kweli: siku moja shileni kwetu wazungu kutoka nchi Fulani walitutembelea(maana ile ilikuwa shule ya diocese Fulani) katika kujitambulisha kuna mmoja alisema wasifu wake kwamba anasoma masters ya chemistry halafu alikuwa na miaka 18... Wakati shileni kuna mijamaa ipo form ina miaka 18 na mengine form 6 ina miaka 19 hadi 20....

Ni hayo tu.... Moderator wakati mwingine huwa anaficha post zangu watu hawaoni... Basi naomba huu muuruhusu
Tatizo sio miaka mingi ya kusoma ni vitu tunavyosoma. Vingi havina msaada wowote katika maisha yetu. Baada ya kujua kusoma na kuandika na kujua lugha vizuri ilitakiwa watoto waanze kutambulishwa moja kwa moja kwenye fani mbalimbali

Yaani kuanzia darasa la tatu, mwenye uelekeo wa kuwa enginia aanze, daktrai, sheria nk. Chuoni ingebaki kwenda kupata umahiri tu tofauti na ilivyo sasa

Mimi siku moja lilipita wazo kama hilo la kuwa Elimu ndio chanzo cha umasikini. Tafakari yangu ilipishana kidogo na hii. Mimi nilijisemea hivi:

Kusingekuwa na Elimu kila mmoja angekuwa kwenye eneo lake la asili alilozaliwa. Huko kuna shughuli lukuki zinaendelea. Kama ni wakulima ungekuwa mkulima, wengine wavuvi, wasusi, wafugaji nk.

Kila mmoja lazima angekuwa na shughuli ya kufanya tofauti na hivi sasa ambapo elimu inawatoa watu kwenye maeneo yao ya asili na kuwaleta kuwarundika eneo moja la mjini halafu baada ya kumaliza elimu wachache sana wanarudi kwao, wachache wengine wanapata ajira na kundi kubwa linabaki bila ajira au shughuli ya kufanya.

Hili kundi lisilo na ajira haliwezi kurudi tena kwenye maeneo yao ya asili kwasababu tayari elimu imeshawaaminisha kule walikotoka hakuna maendeleo, kuna maisha duni, hakuna shughuli zao kwa elimu imeshawafuta asili yao na kuwatambulisha kwenye shughuli mpya ambazo wanapoteza muda mwingi wakizitafuta

Kwani bila elimu hii ya wazungu tungekosa nini?
 
Upo sahihi pia, ila kwa mtazamo wangu... Muda unaathali katika kila jambo analofanya mwanadamu..... Mi niona si sawa mtu muafrika ana umri wa miaka 25 au 26 eti bado mwanafunzi....
 
Umeongea vyema sana mkuu, hii elimu yetu ya Tanzania inachangia sana umaskini na kupoteza muda, kijana anamaliza chuo amesomea business, lakini ukimwambia atengeneze business plan hawezi.

Angalia hizi shule za cambridge na IB curicculum, mtoto anaanza primary akiwa na miaka 5-11 years kamaliza primary, secondary ni 2 years, hapo ameiva balaa kwa nadharia na vitendo
 
Back
Top Bottom