Kwanini ni mwiko kumnyima mtu chakula?

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
6,441
13,563
Watu wengi wanasikia tu kauli kuwa sio vizuri kumnyima mwenye njaa chakula lakini wengi wao hawana ufahamu hata kidogo kwasababu gani ni mwiko na kosa kumnyima mtu chakula.

Kuna wengine anaweza kuwa na chakula ndani ila akamnyima mtu sababu ya uelewa mdogo wa elimu ya kwann mtu apewe chakula bila maelezo. Anaweza kutompa chakula mtu sababu ya maelekezo ya bajeti, kuogopa kesi zinazohusiana na food poisoning, kutotaka kutegemewa, na kadhalika.

But sababu za watu kupewa chakula kama sehemu ya ibada kwa bahati mbaya hazifunzwi especially kwa kizazi hiki cha sasa na matokeo yake wengi wa vijana na mabinti wa sasa hawafahamu maudhui na mantiki(logic) iliyopo nyuma ya ibada ya kumpatia chakula aliye na njaa.

Zifuatazo ni sababu zinazosababisha kutompa mtu chakula kuwa ni sehemu kubwa ya dhambi ya umauti na pengine chanzo cha mikosi na mabalaa kama sio laana.

1. Njaa huja na maumivu makali sana ya kichwa, mwili, tumbo na kuishiwa nguvu. Hii hali haina tofauti kubwa na mtu aliyemgonjwa wa maradhi makali kama maralia, typhoid, au kipindupindu. Kumnyima chakula mtu mwenye njaa ni sawa na kutaka ateseke na haya maumivu kwa hiyari yako au matakwa yako. Yaani umetaka aumie. Kwa wale ambao wameshawahi kushinda na njaa kwa zaidi ya saa 24 wanaelewa hii hali huwa inakuwaje. Ambao hamjawahi usije ukajaribu.

2. Njaa humpa mtu unyongefu na utulivu wa imani ambapo hii hali humlazimu kuelekeza akili yake kwa MUNGU na kuomba huruma yake japo apate kitu chochote cha kula. Anapokujia mtu mwenye njaa mlangoni pako jua sauti ya MUNGU ipo ndani yake ikikutaka kumpatia chakula. Kumnyima ni kumfanyia kiburi mwenyezi MUNGU na kumwambia hautaki kufanya maagizo yake yoyote yale.

3. Njaa huzaa maumivu ya hisia na mwili, maumivu haya hupelekea mtu kuingiwa na hali ya unyama na kuwa tayari kufanya lolote ili aweze kutibu njaa yake. Kumbuka mtu mwenye njaa anaweza kula hata mzoga, chakula kilichooza, na hata kumla mwanadamu mwenzake. Kama unabisha hili nenda kasome historia ya urusi miaka ya vita vya dunia nini kilitokea pande zile utasoma testimonies za watu kuviziana na kuuana ili kupata nyama ya kula.

4. Ubinafsi ni zao la njaa. Mtu ambaye aligonga milango kuomba msaada na hakupewa msaada akaachwa na njaa yake imuue akienda zake akala hata chakula kichafu au akaiba, huwa anageuka kuwa mtu katili asiye na utu na kuwa mbinafsi asiyehurumia wengine. Zao la hii hali ni uchoyo wa chakula wakati wa njaa kali aliyokuwa nayo.

5. Njaa huchangia ulafi na kuvimbiwa. Ulafi ni mojawapo ya dhambi ya umauti na yafaa kukemewa kwa kauli na vitendo. Mtu mlafi huwa ni matokeo ya kutokuwa na uhakika wa kupata chakula siku inayofuata huwa anakula ili njaa isimpate tena. Ndani ya akili ya mtu mlafi ni hofu ya kuumizwa na njaa siku inayofuata so huwa anakula kwa bidii ili kesho asiteseke tena. Unapomuona mtu mlafi usimchukie, muonee huruma na tafuta namna ya kumsaidia kula yake isiwe ya mashaka.

6. Watu wanaotokea mazingira au familia zenye njaa kisha wakafanikiwa mara nyingi huonekana ni watu wenye roho mbaya sababu ya tabia zao za kuwa na tabia za ubinafsi, uchoyo na kunanga watu eneo la chakula. Huwa wanakuwa na tabia za ajabu eneo la chakula kama matokeo ya wasi wasi wa kupoteza chakula au kumaliziwa au chakula. Hii inatokana na history ya kutosaidiwa wakati wa njaa.

7. Njaa inaweza kusababisha vita kama ikikaa muda mrefu na kuwa sugu. Inaweza haribu mahusiano mazuri kuwa mabaya, hupelekea chuki baina ya ndugu au majirani.

Hizi ni sababu chache sana nimeweza kukupatia ujue ni kwasababu gani tunafunzwa kuwa ni mwiko kumnyima mtu chakula au kutengeneza mazingira mtu akose chakula.

Je, una wajibu gani kama mwanajamii katika kusaidia mwingine asipatwe na njaa?

Njaa ni kitu kibaya sana. Hata taifa letu kupitia baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikemea sana uzembe wa kutokuwa na chakula na kuwasihi wanainchi kuanzia ngazi ya kata kuwa na akiba ya chakula na kuwa na jitihada za makusudi kupitia ujamaa kutokomeza njaa kwa bidii zote. Ghala ziwe na chakula cha kulisha watu kwa zaidi ya muda wa makadirio. Uhakika wa chakula uwe mkubwa sana.

Kama mwanajamii wa kawaida unaweza kufanya haya kuondoa roho mbaya wa njaa nyumbani kwako na pia uweze kufanya ibada ya kutoa chakula kwa watu sahihi na kupata baraka kumshinda hata anayekwenda kutoa milioni kwa mwamposa.

1. Hakikisha nyumbani kwako kuna kiasi cha kutosha cha chakula kutosheleza familia yako kuanzia mwezi mzima kuendelea.

2. Hakikisha ratiba ya chakula inakaa sawa nyumbani chakula kiwe tayari njaa ikute chakula sio njaa iwe matumboni mwa watu wewe ndio unajadili kama kipikwe nini. Ratiba ya chakula inajulikana kuwa ni kuanzia asubuhi kunapikwa nini, mchana nini, jioni nini.

3. Tambua mgeni anapokuja kwako usimkadirie kwa macho ndipo ujue anatakiwa kula ama vipi. Mgeni huwa haulizwi utakula ama laa. Andaa chakula kizuri kudiri ya uwezo wako na umpatie mgeni chakula kulingana na wakati gani huo wa chakula. Kama ni asubuhi basi muandalie chai, kama mchana basi lunch kama jioni basi dinner.

4. Jenga tabia ya kuwafungia chakula wageni especially hawa mabachelor ambao hawajaoa,au hata mtu ambaye ameoa ila unamuona tu kuwa hali yake si nzuri. Muwekee chakula cha kuondoka nacho kama ameshindwa kula pale nyumbani tena kwa usiri na faragha kubwa sana.

5. Anapokugongea hodi mtu mwenye njaa bila kujali unadhifu wake sababu wapo watu wanavaa nadhifu ila mfukoni hana hata buku ya chakula, msaidie aweze kupata chakula inaweza kuwa ni cha kupika au basi mpeleke pale kwa mama ntilie akale mlipie na umuache anakula mpatie hata ya chai ya kuanzia kesho.

Pia wapo wale watu ambao unaona kabisa huyu ana ulaji wa mashaka nenda kamlipie bili kwa mama ntilie awe anakula kila siku wewe muwekee hata ya mwezi kama una mudu. Chai 2000,mchana 2000 na jioni 2000 kama MUNGU amekuwezesha kufanya hivyo. Kama ni gharama kwako basi unaweza muwekea hata portion ya chakula kila jioni nyumbani kwako akaipitia aende kula kwake asilale na njaa. Usisahau maji ya kunywa. MUNGU atakubariki sana. Fanya iwe siri.

6. Unapoona familia inakula kwa shida sana. Usishindwe kuwasaidia kupata chakula especially kipindi cha sikukuu japo waweze kupata furaha ya chakula siku ya sikukuu. Unaweza kutunza hii pesa ya sadaka yako mwaka mzima ukasubiria sikukuu kama Eid, pasaka, Christmas, au mwaka mpya na ukawasuprise hiyo familia na kilo tano za mchele, mkungu wa ndizi, nyama kilo tano , viazi, mafuta ya kupikia, vitunguu, na vikolokolo vyote vya kupata msosi mzuri na wamaana, kisha ukawachapa na kreti moja au mbili za soda au kama ni bei basi hata katoni mbili za Azam cola na mochungwa haitakuwa mbaya.

Nachotaka kusema ni kuwa pepo wa njaa ni mbaya sana. Unapomuona sehemu mchukie na umfukuze asiwepo mazingira unayokuwapo.

Ukiwa na mwanamke ambaye muda wa chakula yeye anajizungusha zungusha haeleweki huyo ni wakala wa pepo la njaa analivuta, mkemee na kuwa mkali kama Simba usicheke nae. Chakula kiwepo mezani njaa ikikute.

Sio unakuja na wageni muda wa lunch au muda wa chakula cha jioni mwanamke anazunguka zunguka jikoni hadi wageni wanaaga maana masaa yamekwenda hiyo ni aibu mkemee na umseme kwa muda usiopungua masaa mawili bila kukujibu wala kujitetea kwa lolote.

Na ukiona hajirekebishi tafuta house girl mpatie ratiba ya chakula na maelekezo yako muhimu asimamie na huyo mkeo asilete neno lolote hapo amuache dada afanye majukumu yake kwa mujibu wa maelekezo yako. Ilitokea mkeo akaleta interference yoyote itayomfanya dada kushindwa kuandaa chakula kwa wakati hakikisha unachimba biti kali ajue upo serious.

Kama mkeo ana tabia za kunyima watu chakula peleka kwao akajifunze na kujutia tabia yake mbovu. Kama mkeo anagawa chakula hovyo hadi ndani kwako kinaisha muelekeze atambue kuwa hapo ndani kuna wageni wanaweza kuja hivyo hawe na utaratibu, kama kuna mtu ana haja huko nje akuletee hizo shida wewe ili utoe suluhu ya kudumu na kumpatia chakula mhitaji badala ya kuharibu ratiba ya kaya yako unayoilinda.

Njaa sio kitu kizuri, pambana na mazingira inapotokea, usiiruhusu iwepo mazingira yako, mtetee mtu anayepambana nayo, na hakikisha unasaidia wenye njaa.
 
wahehe wana msemo wao wanakwambia yeeee beeee ugali sio chakula cha kumnyima mtu beee muyawe wahehe ni moja kati ya makabila ya watu ambao ni Ngumu sana kumyima mtu chakula kwa hili nawapongeza sana hii nime experince wakati naishi Iringa
 
Back
Top Bottom