Kwanini hapa Tanzania kama haujui kiingereza watu wanasema haujasoma hata kama umesoma?

Wacheni uongo na Ugaidi wa mtandaoni.

Kuongea lugha ya Kiingereza sio kipimo cha akili.

Kasema nani hayo?

Haifikirishi, wewe ndie unaetaka kulazimisha mtu afikiririe kwamba hilo nalo ni lakufikiria.

Ni nani au wapi hapa Tanzania huwa wanapima uwezo wa akili?":rolleyes:
Isitoshe, unaposema "Tunapima" una maana ya wewe na nani?

Wacha kutukana vijana. Na kupotosha umma.

Maarifa hayatokani kwa kujifunza lugha ya Kiingereza na vilevile sio kweli kwamba maarifa mengi yapo katika lugha ya Kiingereza. Huo ni upotoshaji
Mkuu ni kweli maarifa mengi yapo kwenye Lugha ya kingereza kutokana na ushawishi wake kiteknolojia , sayansi na biashara.
 
Mbona hata ma lecturers vyuoni nawenyewe hajui kiingereza wanaongea kiswahili 70% kwa 30 wakiwa wanafundisha, huo niugonjwa mkubwa wakutojua kiingereza, na tunaanza kutetea ujinga kwa kujilinganisha na nchi kama japan, China na Russia, kwa kusahau kwamba sisi kiingereza tunaanza kufundisha darasa la kwanza.

Nilishangaa sana kwa kweli kuona Dr anamuelezea mwanafunzi kwa kiswahili...
 
kibongo bongo, kama unajua kingereza, wewe ni Dr....ukionekana unaongea na mzungu na mukaelewana vizuri basi wewe ni professor....na cv yako ya vijiweni itaeleza kuwa uliishi ughaibuini ukisomea masomo mtambuka..😆😅😂🙄❗
 
Mbona hata ma lecturers vyuoni nawenyewe hajui kiingereza wanaongea kiswahili 70% kwa 30 wakiwa wanafundisha, huo niugonjwa mkubwa wakutojua kiingereza, na tunaanza kutetea ujinga kwa kujilinganisha na nchi kama japan, China na Russia, kwa kusahau kwamba sisi kiingereza tunaanza kufundisha darasa la kwanza.
Lecturer akifundisha ung'eng'e mwanzo mwisho hakika mtasapu sana
 
Shida inakuja, umesomaje wakati kugha ya kufundishia elimu ya juu ni kiingereza, na wewe hujui kiingereza?
 
Yaani hii nchi MTU anayejua kiingereza ndo MTU anayekubalika Kama Naomi.

Inafikirisha Sana hili jambo.

Tunapima level ya intelligent kwa kuangalia lugha.

NB : vijana jifunzeni kiingereza ili msipitwe na maarifa maana maarifa mengi yapo katika lugha ya kiingereza.
Ni kweli kwamba kujua Kiingereza si usomi.

Lakini pia, hata wewe mwenyewe umekubali kwenye NB kuwa kujua Kiingerwza ni muhinu katika kujua maarifa mengi ya dunia ambayo yapo katika Kiingereza.

Mtu ambaye anajua Kiswahili tu ni vigumu sana kuanza kujadikiana naye habari za faksafa za Bertrand Russell au String Theory.

Mambo hayo hayajaandikwa wala kutafsiriwa kwenye Kiswahili.

Mara kadhaa ninekuwa nikifanya majibizano na watu hata hapa JF. Unabishana na mtu, unamletea link ya kuonesha source au kuongeza mazungumzo yaende kisoni zaidi, halafu kumbe kwa sababu link ya Kiingereza na mwenzako hajui Kiingereza, hiyo kazi inakuwa bure tu.

Unapata kazi nyingine ya kutafsiri link.
 
Sasa mkuu utafaulu hata form four tu kama hujui English? Kama kweli wew ni intelligent means utafaulu hata form four tu, sasa kama hujui English utafaulu vipi ? Hio ni basic examination kabla hatujapima mambo yako mengine
Basic examination = preliminary examination.
 
Naandika na kuwasilisha Bila ya mpangilio maalum.

=========
Ingawa kiingereza ni lugha inayozungumzwa na watu wengi na hutumika katika mawasiliano na baadhi ya wasomi wa kimataifa, kudai kuwa na ustadi wa lugha ya kiingereza ndii kunaonyesha kuwa na akili, ni kupuuzia utamaduni na utajiri wa lugha mama za mataifa mengine.

Kwa kiinegereza, 'equating intelligence with english proficiency alone overlooks the cognitive and cultural richness of multilingualism'

Itoshe, Elimu wala maarifa haukomi kwa lugha ambayo inapokelewa bali inajumuisha wigo mpana wa maarifa na ujuzi wa kufikiri kwa kina unaovuka mipaka ya lugha.

Maarifa yapo katika aina na lugha nyingi.

Mfano mdogo tu hapa, miaka ya nyuma tukiwa tunabadilishana mawazo, mnaigeria mmoja alinisii nitafute kitabu kinachoitwa 'Ezumezu' kilichoandikwa na Mnaigeria mwenzake , kitabu hicho anadai 'kinafundisha mifumo na misingi ya falsafa ya Mwafrika'.

...kitu ambacho kwa utafsiri wa haraka, kuwa Waafrika waliweza kupata na kutumia maarifa kwa Lugha zao.

Itoshe pia kusema, mleta mada amewasilisha hoja yake kwa njia ya ushawishi ya "Logos" ambayo iliasisiwa na kuandikwa kwa lugha ya kigiriki.

Mtakumbuka, Aristoto"Aristotle" na wenzake ndio walikuwa ni wabobezi wa mabishano na kushawishi hadhira-walikuwa hawajui kiingereza, lakini bado wanatambulika kuwa walikuwa na Akili na Maarifa makubwa Duniani.

Walitumia lugha ya kwao ambayo baadae ndio ilitafsiriwa kutoka lugha ya kilatini na baadae lugha zingine za watu wa Ulaya na baadae tena na wazungu wa Ulaya-kwa kiingereza. ~Brittanica dot com

Itoshe hata hao kina Aristotle walisoma Afrika. Ikiwa in maana haya maarifa ambayo wazungu wanadai wanayo, wametoa Afrika.

Anachokifanya huyu haya land ni kufunika historia ndefu na utajiri wa maarifa ya Mwafrika kwa kupotosha. Sidhani kama kuna lugha nyingine laini zaidi ya hiyo-kwamba ni mpotoshaji na ni mzushi.

Hatahivyo-nonetheless:rolleyes:🧐

Kama anavyosema mbatizaji. Lala unono Ukijua kwamba maarifa mengi yametoka Afrika.
 
Mkuu ni kweli maarifa mengi yapo kwenye Lugha ya kingereza kutokana na ushawishi wake kiteknolojia , sayansi na biashara.
Sio kweli hata kidogo...

Kwa maana kwamba hata mifumo ya kiserekali waliyoikuta kwetu Afrika au kwingine; wakoloni walienda na kutafsiri kwa lugha ya kiingereza. Lakini maarifa yalikuwa ni ya wenyeji walikoikuta.

Hiyo haina maana maarifa kama hayo ya kiserekali ni ya kutoka kwa 'Wazungu' kama mnavyotaka kuaminisha watu hapa.

Inatuambia, wametumia maarifa ambayo wameyatafsiri kwa lugha ya kiingereza na kuwasilisha tena kama maarifa yao.

Nakataa katu katu maarifa 'mengi'yapo kwenye lugha ya Kiingereza.

Unaijua misamiati ya kiswahili? Unafikiri maarifa na lugha zile zimetoka Ulaya? Hapana.
 
Kwasababu tunasomea KINGREZA tangu 4m1 mpaka Chuo, Inawezekana vipi uitumie lugha kwa miaka karbu 10 na usiijue? Hiyo Elimu unakua umeipatapataje?
 
Sasa ukae darasani miaka 17 bado usijue kingereza wewe sinutakua mpumbavu wa kiwangoncha Lami.

Rasi simba anafundisha kwa miez mi 3 mtu anaongea ngeli freshbhalaf we uakapoteza 17yrs kwenye madawati bado uje utuongelee No. Yes..You know za kuunga unga.lazima tukushangae tu
 
Shida inakuja, umesomaje wakati kugha ya kufundishia elimu ya juu ni kiingereza, na wewe hujui kiingereza?
Mkuu pamoja na kwqmba haya ni ya mjadala tofauti, hiyo ni shida ya kujitakia.

Elimu ya juu siyo lazima ifundishwe kwa lugha ya kiingereza.

Labda unasema kwamba Vitabu vingi vya elimu ya juu vimeandikwa kwa lugha ya kiingereza, na haina maana maarifa yapo kwa Kiingereza peke yake.

Itoshe, kuondokana na kadhia hii, hivi vitabu vinaweza kutafsiriwa kuenda kwenye lugha ya kiswahili.

Wachina Je? wamepataje elimu na maarifa yao? This is rhetoric. Ni balaga tu.

Shida ipo kwenye vita hizi za kisaikilojia. Ahida ipo kwenye kwenda kutafsri hivyo vitabu kwenda kwenye lugha ya kiswahili Sasa labda pia useme Baraza la Kiswahili limekosa vipaumbele. hapo sawa.

Ila maarifa hayatokani, akili haitokani na kujua kiingereza.

Huyu mchwara nimpotoshaji tu. Ni mbaguzi anaytaka tuamini kuwa lugha ya kiingereza ndio lugha kuu. Na kwa tafsiri nyingine, ni kwamba wazungu wako juu. Huo sio ukweli na hakuna tafiti yeyote ile ya kisayansi inayotamka hivyo.
 
Wacheni uongo na Ugaidi wa mtandaoni.

Kuongea lugha ya Kiingereza sio kipimo cha akili.

Kasema nani hayo?

Haifikirishi, wewe ndie unaetaka kulazimisha mtu afikiririe kwamba hilo nalo ni lakufikiria.

Ni nani au wapi hapa Tanzania huwa wanapima uwezo wa akili?"🤓:rolleyes:
Isitoshe, unaposema "Tunapima" una maana ya wewe na nani?

Wacha kutukana vijana. Na kupotosha umma.

Maarifa hayatokani kwa kujifunza lugha ya Kiingereza na vilevile sio kweli kwamba maarifa mengi yapo katika lugha ya Kiingereza. Huo ni upotoshaji
60% za content zilizopo kwenye internet zipo in English,

So waweza jua maarifa mengi yapo kwa lugha gani
 
Mkuu pamoja na kwqmba haya ni ya mjadala tofauti, hiyo ni shida ya kujitakia.

Elimu ya juu siyo lazima ifundishwe kwa lugha ya kiingereza.

Labda unasema kwamba Vitabu vingi vya elimu ya juu vimeandikwa kwa lugha ya kiingereza, na haina maana maarifa yapo kwa Kiingereza peke yake.

Itoshe, kuondokana na kadhia hii, hivi vitabu vinaweza kutafsiriwa kuenda kwenye lugha ya kiswahili.

Wachina Je? wamepataje elimu na maarifa yao? This is rhetoric. Ni balaga tu.

Shida ipo kwenye vita hizi za kisaikilojia. Ahida ipo kwenye kwenda kutafsri hivyo vitabu kwenda kwenye lugha ya kiswahili Sasa labda pia useme Baraza la Kiswahili limekosa vipaumbele. hapo sawa.

Ila maarifa hayatokani, akili haitokani na kujua kiingereza.

Huyu mchwara nimpotoshaji tu. Ni mbaguzi anaytaka tuamini kuwa lugha ya kiingereza ndio lugha kuu. Na kwa tafsiri nyingine, ni kwamba wazungu wako juu. Huo sio ukweli na hakuna tafiti yeyote ile ya kisayansi inayotamka hivyo.
Hakuna aliyebisha, mimi naongelea katika mazingira ambayo elimu ya juu inatolewa kwa kiingereza, utasemaje umesoma na huijui lugha inayotumika kufikisha elimu husika kwa wanafunzi?
 
Back
Top Bottom