Elimu yetu, vijana wetu, umasikini wetu

Lucidator

New Member
Jul 2, 2020
2
2
Nimepata nafasi ya kukutana na Watu Wengi ikiwemo wabunge na madiwani na Kati ya mada Nilizoongea nao Ni Kuhusu Elimu yetu na Vijana wa kitanzania.

Natamani kusema mfumo wa elimu Ni mbovu na hauandai akili ya kijana kuyakabili Maisha yaliyo mbele yake mitaani, lakini najua Fika Kila mtu analifahamu hilo. Leo nitaongelea zaidi Maisha Baada Ya elimu na mchango wa Elimu yetu kwenye Maisha ya Vijana Wenyewe.

Wakati Nahitimu darasa La Saba tulikuwa wanafunzi Zaidi ya 800,000 kwa Tanzania Nzima, Tulioenda Sekondari tulikuwa Chini Ya 500,000 kwa mwaka ule peke yake. Hii inaonesha wanafunzi laki 4 (400,000) walibaki mitaani.

Tulipohitimu kidato Cha Nne, Kuna Waliofeli, walioendelea kidato Cha 5, na Vyuo, Na walioshindwa kuendelea na Masomo kwa sababu MbaliMbali za Maisha.

Kwenye kata Yetu kulikuwa na Shule za Sekondari zaidi ya 5, na Kwa wastani kila shule angalau wanafunzi 60 pekee ndo wanaoendelea na Masomo wengine waliobaki wanaishia kurudi mtaani. Hivyo, kwa wastani, kata yangu peke yake inazalisha Vijana 500 kila mwaka waliohitimu kidato Cha Nne Ila hawakuendelea na Masomo yao, na Kuanza kujishughulisha na Shughuli ndogo ndogo za kujiingizia Kipato Mtaani.

Vijana Hawa Hawaonekani kwa sababu kila mmoja anafata njia yake, kuanzia kuhama mikoa, mitaa, au kubaki majumbani.

Kwa Tanzania Nzima, mpaka kufikia mwaka Huu 2023, Takwimu zinaonesha kutakua na Angalau wanafunzi Milioni Tatu (3,000,000) tukizingatia juhudi za Mh.Rais Samia Suluhu za hivi karibuni kwenye sekta ya Elimu. (Kwa data kamili ya mwenendo wa shule, walimu na Wanafunzi Soma linki niliyoambatanisha mwisho wa andiko hili)

Hawa Wengi wao Wataishia Tena Kurudi Mitaani, Na Kuchangia Umasikini kwa njia Nyingi Mbali Mbali ikiwemo kuongeza Wimbi la Watu tegemezi. Pia kwa sababu Ni Vijana Maisha yakiwa Magumu watapita Zile njia tunazozijua wote ikiwemo Wizi, Ujambazi, Kuuza Miili Yao, Matumizi ya Madawa ya Kulevya, Biashara Haramu N.k

Wengine wamefikia mahali wanasema Vijana hawataki kazi wao wanataka Hela tu au sekta za michongo wapige mawe kirahisi, na Mimi leo nawajibu kwa kusema hao Vijana wao ndo hawataki kazi, Moshi kila mtu anapambana na Mitaji ya kufikia Zile ndoto zetu ndo imekua changamoto Kubwa kwetu. NANI ATUWEZESHE?! tunaweweseka kwa mawazo usiku tukifikiria jukumu lililopo mbele yetu na Namna ya kulikabili tunapambana peke yetu na misongo ya mawazo Namna gani tutazikomboa familia zetu na Jamii zetu na Vijana wenzetu kwenye huu umasikini uliokithiri. Huzuni iliyopo kwenye mioyo yetu kwa Mara Zote tulizoshindwa kuwa wa msaada pale tunapohitajika Kama Vijana Wa Jamii zetu. Tuna wasiwasi huenda tumesahaulika.

Wachache waliobaki wanafanya Biashara Halali Ila Za kipato Cha Chini Kama bodaboda, Ufundi, BaaMedi, Ulinzi shirikishi N.k. Kwa Bahati mbaya Hawa Nao wana watu wanaotegemea hicho kidogo wanachopata, na hata Kama Hakuna Basi hawafiki mahali na Kuishia Kuwa Masikini wanaomudu Maisha Ya Kula Na Kulala Wasiweze Mengine.

Kufikia Hapa Nataka Nikuulize Msomaji, NANI ALAUMIWE? Ni Elimu, au Mfumo wake? Ni Serikali? Au Ni Hawa Hawa Vijana Kwa kushindwa Kujinasua Kwenye huu mtego waliosukiwa wakiwa angali wachanga?

NB: ubovu wa Elimu unasukwa pale shule ya msingi kwa kisingizio Cha kutetea Lugha Ya kiswahili, alafu msumari wa Mwisho Ni pale Lugha ya kiingereza inapowasili Sekondari.

Kama Taifa La Kesho, Kama Vijana, Tunatekeleza Haki Yetu Kikatiba Kwa Kuuliza: SERIKALI INA MPANGO GANI NA MAISHA YA VIJANA HAWA WENGI WANAOTENGENEZWA MASHULENI?

Serikali Ina mipango Kama Mikopo ya Halmashauri kwa Vijana, BUILDING BETTER TOMMOROW ya dodoma, na Kuongeza Elimu bure mpaka A-level. Tunashukuru jitihada hizi za Serikali yetu, Ila swali Ni Je? Zinatosha?.

Jambo hili linavyozidi kuleta na kusababisha wasiwasi kwetu Vijana tunapojiuliza kesho yetu na Upi mpango wa serikali kwetu Kama ilivyo haki yetu kikatiba.., wachache tunaofahamu tunajitahidi tupite njia hizi ili kujikwamua..

Mikopo Ya Taasisi.
- Mabenki Kama Kcbl, Saccoss, na vikundi..(tumepambana kote Ila mwisho wa siku benki Kama Kcbl walitutuma hati ya nyumba au shamba tutatoa Wapi Sasa?! kwa madai hawana mikopo ya kilimo. Ila walishachukua kwetu zaidi ya laki moja ili tu kukamilisha hizi taratibu zao na vigezo Kama kuwa na account za Kikundi na za kila mwanakikundi.. EMBU TAFAKARI.)

-Halmashauri ya Manispaa.. (Hapa tuliwekeza Muda tangu 2022 na pesa kufungua Account ya benki, kulipa stationary hizi taratibu, kuandaa na kuchapisha katiba nyingi Sana pamoja na za benki, kujisajili Manispaa, nk. lakini Hadi Leo hii hatujafanikiwa kwa lolote Tena tumejizidishia umasikini)

-Watu Binafsi (Hii najua unafahamu ilivyo)

-BBTommorow haijatufikia mashamba ya pamoja.

Asante.

Andiko hili Ni kwa ajili ya STORIES OF CHANGE 2023 Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeshindwa kuliweka katika Jukwaa Husika!

RONALDO FOCUS, KIJANA MTANZANIA.

Screenshot_20230801-115301_1.jpg
SAMIAI.jpg
jummah.jpg
 
Muda mwingi unatumika kumfundisha mwanafunzi ambaye anashindwa kujiajiri baada ya hapo it's a shame siyo kwa vijana bali kwa Taifa kutokana na kushindwa kuwanyanyua hao vijana kwa namna nyingine na kubaki na porojo tu za ruzuku hewa kwa vijana.
 
Back
Top Bottom