Kwa wajuzi wa Tractor za Massey 290 au 385 ipo bora kwa kulimia

Shamba lipo mkoa gani
Ruvuma Songea

JPEG_20200618_175350_-1252901083.jpg
 
Je, muda wa ukame udongo wa huko ukoje? Jembe la mkono ukipiga linadunda?

Je, kuna milima huko?

Je, shamba lako linalinganaje?

Muda wa mvua je shamba lako linakuwa na tope?

Mtazamo wangu binafsi kwa nilichoona. (Sio kitaalam) Kama shamba lina udongo mlaini wa kichanga na shamba halina visiki na mizizi shambani basi trekta la 2wd na nguvu (50hp-70hp) inatosha.

Kama ni eneo lenye ardhi ngumu unaweza chukua la nguvu (70hp-90hp). Kama ni eneo ambalo mvua ikipiga ni utelezi na tope inabidi upate 4wd na nguvu ya (70hp- 90hp). Pia hizi za 4wd zinatumika kwenye mpunga pia.
 
Je muda wa ukame udongo wa huko ukoje? Jembe la mkono ukipiga linadunda?
Je kuna milima huko?
Je shamba lako linalinganaje?
Muda wa mvua je shamba lako linakuwa na tope
Kuna maeneo yana tope mengine hayana lakini pia matarajio kulima mpunga na mahindi ,nadhani hii option ya mwisho ni nzuri zaidi 4wd/70-90
 
Okay, hapo option ni 4wd horse power si chini ya 70 na kuendelea. Ila pia horse power zinavyozidi kuongezeka na bei ya trekta inaongezeka na kwakua umechagua massey ferguson basi hiyo hiyo itakufaa maana ni trekta ya muda mrefu kwa Tz na spare zake zinapatikana kama za toyota tu
 
Kikubwa service kwa wakati(usichelewe hata siku moja), usimamizi uwe mzuri sana, kabla hujalima shamba la mtu shuka ukague shamba ukiwa pamoja na mwenye shamba (ukaguzi ufanye wewe mwenyewe kwa umakini) ili sehemu zenye visiki na mawe makubwa uweke alama. Kwa mashamba yetu bongo, ni visiki na mawe ndo vinachangia kwa kiasi kikubwa sana kuua matrekta zingatia sana hilo.

Liheshimu trekta hilo sana sio kwasababu linafanya kazi ngumu ndo ulitumie kwa namna ambayo haitakiwi, utajuta. Ukilitunza na lenyewe litakutunza. Nunua trekta, jembe la disk 3 na trailer.

Msimu wa kulima ni mfupi sana kuliko msimu wa kusomba bidhaa. Ukiwa na trailer lako utafaidi sana mashambani na hata mjini kwako(speaking with experience). USIMAMIZI ZINGATIA.
 
Kuna maeneo yana tope mengine hayana lakini pia matarajio kulima mpunga na mahindi ,nadhani hii option ya mwisho ni nzuri zaidi 4wd/70-90
Sawa, hio ndio inatosha.
Kama pesa unayo Inabidi uwe na jembe (disk), trailer la kubeba mizigo, jembe la kuvuruga kwa ajili ya mpunga, mashine ya kupukuchua mahindi inayoendeshwa na engine ya tractor, mashine ya kupiga mpunga inayoendeshwa na engine ya trekta.

Pia ongeza shamba lako binafsi angalau liwe eka 200 mpaka 500. Ili ukikosa wateja bado utakuwa na backup.

NB: kuwa makini sana visiki na mawe. Service pia ni muhimu.
 
Kikubwa service kwa wakati(usichelewe hata siku moja), usimamizi uwe mzuri sana, kabla hujalima shamba la mtu shuka ukague shamba ukiwa pamoja na mwenye shamba(ukaguzi ufanye wewe mwenyewe kwa umakini) ili sehemu zenye visiki na mawe makubwa uweke alama. Kwa mashamba yetu bongo, ni visiki na mawe ndo vinachangia kwa kiasi kikubwa sana kuua matrekta zingatia sana hilo...
Nashukuru sana mkuu kwa moyo wako wa ukarimu
 
Ushauri wenu ( Wewe na Akilindogosana ) upo vizuri sana hasa kuhusu service na kwamba kama anaweza anunue na trailer
Ni kweli, mimi ndo shughuli ninazofanya hizo nafahamu kwa kiasi chake kuhusu haya mambo. Yani hapa anunue trekta, jembe la disk 3(standard) na trailer ni muhimu sana. Kule kwa Songea atapata used mazuri tu na kama mfuko wake unaruhusu anunue na mashine ya kupukucha mahindi maana Songea mahindi huwa ni mengi sana(akipata ile kubwa ambayo inatumia pto shaft ya trekta atapiga kazi kwa amani)
 
Nakupa siri ya Massey ambayo wengi hawaijui. Yaliyosemwa hapo juu yote ni sahihi kuhusu MF. Ugonjwa mkubwa wa MF ni Hydraulic system yake (mikono ya kuinua jembe) inachoka mapema na ikichoka haina dawa.

Mimi nina MF,New Holland na John Deer na zote nilimenya mpya. Huo ndio ugonjwa wa Massey ambao kila mtu alie na Massey analia bila kujali ni U.K au Agroasia. Chukua New Holland (NH) TT75 DV series injini ya Iveco hutajuta. Au kama mfuko hauruhusu chukua Shangai New Holland CNH yenye injini model ya Boomer,Case DX series. Utaipata kwa bei chee kutoka China ikiwa mpya.

Mimi nipo Kalambo ranch ni mkulima nakupa experience sio maneno ya kusikia.
 
Ni kweli, mimi ndo shughuli ninazofanya hizo nafahamu kwa kiasi chake kuhusu haya mambo. Yani hapa anunue trekta, jembe la disk 3(standard) na trailer ni muhimu sana. Kule kwa Songea atapata used mazuri tu na kama mfuko wake unaruhusu anunue na mashine ya kupukucha mahindi maana Songea mahindi huwa ni mengi sana(akipata ile kubwa ambayo inatumia pto shaft ya trekta atapiga kazi kwa amani)
Ushauri mzuri umempa. Kwa kuongezea awe makini kwenye jembe kuna brand nzuri kama field king ambalo ni bomba sio chuma. Jembe likiwa chuma linakuwa zito na hupelekea kuchosha mapema Mfumo wa kuinua na kushusha jembe.

Pia atafute disc plough zenye kuzunguka ili kuepuka kuvunjika au kuvunja Draw bar pale ambapo ikikutana na kisiki au jiwe.
 
Back
Top Bottom