Kwa wajuzi wa Tractor za Massey 290 au 385 ipo bora kwa kulimia

nyamwingi

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
933
863
Wakuu Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosema nilikuwa nahitaji kujua uimara wa hizi tractors, spare .nk
 
Hii
IMG-20200413-WA0013.jpg
IMG-20200413-WA0016.jpg
 
Vp kuhusu 290?
290 ni 2wd. Ulaji wa mafuta ni nafuu kuliko 385. Ukitaka kujua tractor kama ni 2wd au 4wd angalia ukubwa wa matairi ya mbele kwa haraka haraka, japo vipo vigezo vingine. 385 inatumia mafuta mengi zaidi kwasababu ni kubwa zaidi na ni nzito zaidi.

Ila 385 itakuruhusu kulima kwenye maeneo korofi(magumu) na ina nguvu zaidi. Hiyo 385 itatumia kati ya lita 4 hadi 7 kwa eja moja ya kulima kama shamba halina changamoto. Usinunue massey ferguson ya pakistani, nunua ya kutoka uingereza(namaanisha nunua ambazo zimekua manufactured in uk)
 
Nashukuru mkuu kwa mchango wako mzuri na wenye manufaa,naanza kupata mwanga hapa
 
290 ni 2wd. Ulaji wa mafuta ni nafuu kuliko 385. Ukitaka kujua tractor kama ni 2wd au 4wd angalia ukubwa wa matairi ya mbele kwa haraka haraka, japo vipo vigezo vingine. 385 inatumia mafuta mengi zaidi kwasababu ni kubwa zaidi na ni nzito zaidi. Ila 385 itakuruhusu kulima kwenye maeneo korofi(magumu) na ina nguvu zaidi. Hiyo 385 itatumia kati ya lita 4 hadi 7 kwa eja moja ya kulima kama shamba halina changamoto. Usinunue massey ferguson ya pakistani, nunua ya kutoka uingereza(namaanisha nunua ambazo zimekua manufactured in uk)
Akili ilikuwa haijakaa sawa kwa kuona vitairi vidogo na kubwa hasa ya mbele kumbe hii ndio maana yake !
 
290 ni 2wd. Ulaji wa mafuta ni nafuu kuliko 385. Ukitaka kujua tractor kama ni 2wd au 4wd angalia ukubwa wa matairi ya mbele kwa haraka haraka, japo vipo vigezo vingine. 385 inatumia mafuta mengi zaidi kwasababu ni kubwa zaidi na ni nzito zaidi. Ila 385 itakuruhusu kulima kwenye maeneo korofi(magumu) na ina nguvu zaidi. Hiyo 385 itatumia kati ya lita 4 hadi 7 kwa eja moja ya kulima kama shamba halina changamoto. Usinunue massey ferguson ya pakistani, nunua ya kutoka uingereza(namaanisha nunua ambazo zimekua manufactured in uk)
Asante sana ndugu kwa taarifa
 
385 inanguvu zaidi ila ujipange kwenye mafuta.
Onyo: usinunue massey ferguson za pakistan ni mbovu. Nunua za uk anazoleta mtu anaitwa Chris Lukosi yupo facebook.
 
Chris Lukosi ni mfanya biashara. Kabla hujamtafuta ni vema kueleza hapa unataka trekta kwa ajili ya nini ili tukushauri uchukue la ukubwa gani. Yeye atakuuzia trekta alizonazo bila kujali matumizi yako.

Hapa ni sawa na kutaka kununua ist kwasababu ni nafuu kwa mafuta ili ulifanye gari la shamba, utafeli vibaya sana(ni mfano tu). Point hapa ni tujue unahitaji kwa kazi gani then tukushauri la aina gani linafaa ndipo uwasiliane na bwana Chris. Bei huwa zinatofautina ila uwe na kuanzia 30m
 
Chris Lukosi ni mfanya biashara. Kabla hujamtafuta ni vema kueleza hapa unataka trekta kwa ajili ya nini ili tukushauri uchukue la ukubwa gani. Yeye atakuuzia trekta alizonazo bila kujali matumizi yako. Hapa ni sawa na kutaka kununua ist kwasababu ni nafuu kwa mafuta ili ulifanye gari la shamba, utafeli vibaya sana(ni mfano tu). Point hapa ni tujue unahitaji kwa kazi gani then tukushauri la aina gani linafaa ndipo uwasiliane na bwana Chris. Bei huwa zinatofautina ila uwe na kuanzia 30m
Mm nahitaji kwa ajili ya kuendeshea shughuli za kilimo za kwangu na kupata pesa ya kula kwa kuwalimia watu wengine
 
Chris Lukosi ni mfanya biashara. Kabla hujamtafuta ni vema kueleza hapa unataka trekta kwa ajili ya nini ili tukushauri uchukue la ukubwa gani. Yeye atakuuzia trekta alizonazo bila kujali matumizi yako. Hapa ni sawa na kutaka kununua ist kwasababu ni nafuu kwa mafuta ili ulifanye gari la shamba, utafeli vibaya sana(ni mfano tu). Point hapa ni tujue unahitaji kwa kazi gani then tukushauri la aina gani linafaa ndipo uwasiliane na bwana Chris. Bei huwa zinatofautina ila uwe na kuanzia 30m
Mkuu kama itakupendeza ningeomba uniwekee specifications za MF itakayonifaa kwa kilimo hata kama si hiyo 290!
 
Back
Top Bottom