Kusema Maji ya mafuriko ya Rufiji yatafutiwe njia ya kwenda baharini, si kumtukana Rais. Wananchi wanateseka

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,494
54,905
Tunashukuru Serikali ya Tanzania kwa kuyoa Tan 300 za unga, mchele na maharage kwa watu wa Rufiji japo ambazo zimefika na kuonekana kwa macho ni Tan 32. Labda hizo tani nyingine bado zipo njiani.

Huko Rufiji Serikali imepeleka tan 100 za maharage, tani 100 za mchele na tani 100 za maharage kwa Mjibu wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Mwenyewe kasema Mama Samia ndo katoa msaada.

Japo sijajua ni msaada kutoka kwa Samia Suluhu au ni msaada kutoka kwa Serikali sababu Kunenge Mkuu wa Mkoa wa wa Pwani kasema Msaada umetoka kwa mama yetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan, Mara nyingi kutokana na Siasa za Nchi yetu Tanzania, ukiona sehemu imeandikwa katoa Samia, jua Sio samia ni Serikali. Kama msaada katoa Samia, Serikali imefanya nini hadi sasa?

Huko Rufiji mpaka sasa kuna kambi 7 zenye wananchi 749 kwa wilaya za Kibiti na Rufiji waliokimbia Makazi yao kutokana na Mafuriko na idadi nyingine kubwa ya waathirika wamehifadhiwa kwa ndugu jamaa na marafiki Wilaya mbalimbali.

Wito wangu ni Serikali iingie Garama kwa kutengeneza njia ya Maji yaende Baharini. Kusema eti haya mafuriko sio mara ya kwanza, kwani yalishatokea Mwaka 1974, huo sio utetezi.

UVCCM Rufiji wametukalia Kooni. Ukisema kwamba Wanafunzi hawasomi kwani Shule zimefanywa Makambi ya Watu waliokimbia Mafuriko, Wanakupa kibano eti unamtukana rais Samia na kutotambua Mchango wake wakati tunaelekea Uchaguzi Serikali za Mtaa.

Ukisema njia ya maji ifungunguliwe wanasema umetumwa.

Ukisema mahema yalotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu hayatoshi, wanasema Ukipotea Polisi wasiingilie.

Vitisho vimezidi. Tukimbilie wapi?

Tunashauri maji yaondolewe ili wananchi waendelee na kilimo, vingine Serikali itawalisha Mwaka Mzima sababu shughuli zote za Uchumi zimesimama.
 
Hili tatizo lilinifanya nikaona niangalie nchi zingine zinafanya nini kukabiliana na matatizo haya
Kuna wengine wameboresha na kuweka hata kuta kwenye mito sehemu hatarishi na zinazochepua maji

Na wengine kwenye Dam zao pia mbali na kuweka uzio lakini wamechimba mabwawa ya kusaidia pindi mafuriko yanapotokea

Tatizo letu tumejifungia kwenye bubbles na hatutaki kujifunza kwa wengine hilo ndio kosa la serikali yetu

Viongozi wakienda nje wao wanaangalia maduka yako wapi wakanunue suti tu
Ila leo pia Kuna mitandao ya kila aina kwanini hawajiongezi na kuona wenzetu wanakabiliana vipi na matatizo kama haya ?
 
Tunaisema serikali ya SAMIA ila aliyechagiza mafuriko hamtaki asemwe...kisa marehemu
 
Rufiji na mkoa wa Pwani ndiyo mkome. Mmezidi uzuzu, kila mwaka mnachagua ccm. Acha iwanyooshe.
 
Tunashukuru Serikali ya Tanzania kwa kuyoa Tan 300 za unga, mchele na maharage kwa watu wa Rufiji japo ambazo zimefika na kuonekana kwa macho ni Tan 32. Labda hizo tani nyingine bado zipo njiani.

Huko Rufiji Serikali imepeleka tan 100 za maharage, tani 100 za mchele na tani 100 za maharage kwa Mjibu wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Mwenyewe kasema Mama Samia ndo katoa msaada.

Japo sijajua ni msaada kutoka kwa Samia Suluhu au ni msaada kutoka kwa Serikali sababu Kunenge Mkuu wa Mkoa wa wa Pwani kasema Msaada umetoka kwa mama yetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan, Mara nyingi kutokana na Siasa za Nchi yetu Tanzania, ukiona sehemu imeandikwa katoa Samia, jua Sio samia ni Serikali. Kama msaada katoa Samia, Serikali imefanya nini hadi sasa?

Huko Rufiji mpaka sasa kuna kambi 7 zenye wananchi 749 kwa wilaya za Kibiti na Rufiji waliokimbia Makazi yao kutokana na Mafuriko na idadi nyingine kubwa ya waathirika wamehifadhiwa kwa ndugu jamaa na marafiki Wilaya mbalimbali.

Wito wangu ni Serikali iingie Garama kwa kutengeneza njia ya Maji yaende Baharini. Kusema eti haya mafuriko sio mara ya kwanza, kwani yalishatokea Mwaka 1974, huo sio utetezi.

UVCCM Rufiji wametukalia Kooni. Ukisema kwamba Wanafunzi hawasomi kwani Shule zimefanywa Makambi ya Watu waliokimbia Mafuriko, Wanakupa kibano eti unamtukana rais Samia na kutotambua Mchango wake wakati tunaelekea Uchaguzi Serikali za Mtaa.

Ukisema njia ya maji ifungunguliwe wanasema umetumwa.

Ukisema mahema yalotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu hayatoshi, wanasema Ukipotea Polisi wasiingilie.

Vitisho vimezidi. Tukimbilie wapi?
t
Tunashauri maji yaondolewe ili wananchi waendelee na kilimo, vingine Serikali itawalisha Mwaka Mzima sababu shughuli zote za Uchumi zimesimama.
Yupo aliyeukataa ushauri wa kutunza mazingira na mkamfanya shujaa wenu. Leo mnamshambulia asiyehusika! Ni maonezi makubwa. Aliyesababisha yote haya, alisifiwa kila kona yq JMT! Wakati mwingine tuwe na kiasi cha kusifu. Huyu aliyepo kamwe asilaumiwe.
 
Back
Top Bottom