Kozi 11 za afya za kusoma mwaka 2024/2025

Ngufumu

Member
Dec 29, 2016
15
25
Hizi hapa Fani 11 za afya za kusoma mwaka 2024/2025
1700376468820.jpg

Kwa kutambua tatizo sugu la ajira nchini hizi ni Fani za Afya ambazo kwa mujibu wa Hotuba ya Bajeti ya wizara ya Afya 2024/2025 zitakuwa na uhitajio/Demand kubwa hapo mbeleni

Hivyo basi unaweza kumshauri mtoto au ndugu yako kusoma kwa kufuata uelekeo wa upepo, asome Kijanja, akumbuke hakuna tuzo ya mtesekaji bora anayetimiza ndoto/malengo yake ukipata mteremko serereka nao🤗

Ishi nazo hizi hapa👇🏿

1. Stashahada ya Tiba Lishe (Clinical Nutrition)

2. Stashahada ya Juu ya Afya ya Akili kwa Wauguzi (Higher Diploma in Mental Health Nursing) ambapo inatarajiwa kutumika kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Kingine Katika mwaka 2024/2025 Wizara itaweka msisitizo kwenye uzalishaji wa wataalam wa kada za kati(Diploma) za afya zenye upungufu mkubwa. Kada hizo ni pamoja na

3. Wataalam wa huduma za utengamao (Rehabilitation),

4. dawa za usingizi na ganzi (Anaesthesia),

5. Uchunguzi kwa njia ya mionzi (Diagnostic Radiography),

6. Wataalam wa tiba ya macho (Clinical Opthalmology),

7. Tiba kazi (Occupational Therapy),

8. Tiba kwa njia ya mazoezi (Physiotherapy),

9. Utengenezaji wa Viungo Bandia/Saidizi (Orthopedic Technology),

10. Tiba kwa njia ya saikolojia (Clinical Psychology) na

11. kusaidia kuona kwa kutumia miwani (Optometry).

Kingine kikubwa Wizara kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 imeanza utaratibu wa kutoa mikopo kwa

wanafunzi wa afya ngazi za kati(Diploma) katika fani zenye upungufu mkubwa wataalam hao. Jumla ya kozi 11 ziliainishwa katika fani za

1. Tiba Kazi,

2. Tiba Mazoezi,

3. Viungo Saidizi,

4. Teknolojia ya Vifaa Tiba,

5. Tiba Miwani,

6. Teknolojia ya Mionzi,

7. Teknolojia ya Maabara ya Meno,

8. Tiba ya Kinywa na Meno,

9. Sayansi za Afya ya Mazingira,

10. Sayansi za Maabara ya Tiba,

11. Teknolojia ya Utunzaji wa Kumbukumbu za Afya

ambapo hadi sasa wanafunzi walionufaika na mikopo hiyo ni 773 kati yao wasichana ni 355 sawa na asilimia 46 na wavulana ni 418 sawa na asilimia 54. Huu ni Ufadhili wa Serikali kwa lengo la kuhamasisha na kuongeza idadi ya wanafunzi watakaoomba kujiunga na mafunzo hayo

Pia Wizara kwa kushirikiana na shirika liitwalo Campaign for Female Education(CAMFED) imeendelea kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa kike 287 wa fani ya Uuguzi na Ukunga katika ngazi ya Stashahada wanaotoka kwenye familia masikini. Hivyo vijana changamkieni fursa

Unaweza kuzingatia mwenyewe kama linakuhusu au Mshauri ndugu na jamaa kuzingatia hayo☝🏿

Mm naitwa Kaka Gift kwenye moja na mbili, nawasilisha naomba tuendelee kuwasiliana kupitia 👇🏿

Message Kagift Online Store on WhatsApp. Kagift Online Store

Save iyo namba yangu kisha nitumie msg wsp na mm nikusave, mtu ni Watu 🤗

“Let's connect the future is now”👊🏿
 
Back
Top Bottom