Jinsi ya Kupika mchuzi wa samaki na Nazi (chukuchuku)

Aaliyyah

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
15,910
37,988
Natumaini wazima
Leo nawaletea recipe ya kupika samaki wa Nazi chukuchuku,wengine wanasema mchuzi ambao hauna mambo mengi
MAHITAJI
Samaki wabichi unaweza tumia pia wakavu
Nazi,karoti,hoho,kitunguu maji, nyanya,chumvi na ndimu ukipenda
Andaa viungo vyako katakata size utayopenda
Unaweza kuongezea biringanya,bamia au nyanya chungu kama ukipenda

Weka kwenye sufuria samaki,nyanya,karoti,kitunguu maji na chumvi Kisha weka maji kidogo Ili kuivisha viungo pamoja na samaki zingatia kipimo Cha maji

Ukiona vimeiva weka Nazi kwenye mchuzi wako acha ichemke
Hakikisha ugeuzi Wala kukoroga koroga sana unaweza ukawa unatumia njia ya kutikisa tu sufuria kidogo Ili mchanganyiko ukae vizuri ikiiva ipua tayar Kwa kula
Unaweza kula na wali au ugali

Mimi sijatumia nyanya,nimetumia karot wewe unaweza amua kama unatumia bas zisiwe nyingi
Nazi sio lazima ya kukuna kama yangu mnaweza kutumia ya pakti 😍
IMG_20240423_134214.jpg

IMG_20240423_134202.jpg

IMG_20240423_135024.jpg
IMG_20240423_141426.jpg
IMG_20240423_141819.jpg

Nawatakia sikunjema
 
Nacheka lakini naogopa 😂
Kwa masikitiko makubwa upishi wa chapati niliamua kuachana nao
zilikuwa zinanipa shida kwenye shape nilikuwa Hadi namalizia kupika mbavu zinauma Kwa kucheka zile shape hapana ,Yani km Kuna wageni Ilikuwa nachagua za kuwapa 😀😀😀😀
 
Sana kipenzi yaani ni dakika 15 unakula kitu kizuri kabisa
Kwangu sio dk 15, ndo mana bakulaga migahawani.
Kwangu kupika wali kwa dk 45 ni kawaida, kupika huwa napoteza muda mwingi mno.

Ila natamanigi kujipikia vitu nipendavyo ila kubalance muda ndo changamoto
 
Kwangu sio dk 15, ndo mana bakulaga migahawani.
Kwangu kupika wali kwa dk 45 ni kawaida, kupika huwa napoteza muda mwingi mno.

Ila natamanigi kujipikia vitu nipendavyo ila kubalance muda ndo changamoto
Yani hii ni rahis sana hebu jaribu sabbu na samaki sio km nyama na pia hakuna kukaanga kaanga
 
zilikuwa zinanipa shida kwenye shape nilikuwa Hadi namalizia kupika mbavu zinauma Kwa kucheka zile shape hapana ,Yani km Kuna wageni Ilikuwa nachagua za kuwapa 😀😀😀😀

Mie nazipatia sana kusukuma...yani ukiona ile round navyoitoa vizuri utasema chapati si ndio hii

Subiri iive sasa uone maajabu ya kau kau 😂
 
Huwa nashangaa sana watu wanaokula biringanya japo familia inakula.
Ila mimi hata kuiona kwenye chakula napata shida.
 
Mie nazipatia sana kusukuma...yani ukiona ile round navyoitoa vizuri utasema chapati si ndio hii

Subiri iive sasa uone maajabu ya kau kau 😂
😀😀😀Basi nafikiri utakuwa unasukuma sana kati hata ukandie mafuta Lita saba ukisukumansana kati Inakuwa kaukau
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom