Je kwa mtaji wa 2M naweza fungua biashara hizi mbili?

Inatosha

Binafsi ningekushauri tafuta chimbo zuri ufungue vibanda viwili vya Chipsi.

Kimoja simamie mwenyewe, kingine mpe Kijana akusaidie

Ukishindwa kutengeneza Faida almost 30,000 njoo nikurudishie Mtaji wako
Itakuwa unyama sana faida ikifikia huo wastani

Ahsante Mkuu kwa ushauri wako
 
Huenda usiamini Pesa kama Mtaji yaweza kuwa sio sababu ya kufaulu au kutokufaulu...

Unaweza kufanikisha hizo biashara bila hata senti moja na unaweza usifanikiwe hata ukiwa na bilioni moja.....

Ujuzi; location, wateja n.k. ni muhimu kulikio hata pesa
 
Haujawahi kufanya biashara wewe
Kwavile Binadamu hawezi kutaga yai haimaanishi hawezi kuona viza...

Kufungua biashara au project yoyote unahitaji mtaji lakini vitu kama ujuzi, wateja wa kile unachokifanya na sehemu husika ni muhimu kuliko hata pesa (na vyote hivyo hapo juu ni mtaji, Ujuzi, Sehemu Husika na Wateja) ambazo ni muhimu kuliko hata Pesa... ; Sasa wewe kama hauna hivyo vingine hata ukipewa bilioni kadhaa utaziunguza...
 
Hapo mtaji kutosha au kutotosha itategemeana na upande wa location, je banda unalo? Kama hauna unataka liwe la muundo gan? Ukifanikiwa kumiliki banda tu au frem hapo hata 50k unaanza nayo kwa chips, zingatia usafi pia nenda na wakati (usasa) usifunge chips au mishkaki kwenye gazeti tumia foil,vyombo tumia vya kisas usituwekee visahani vya plastik na grass za bati au vikombe vya plastik hata kama banda litakuwa uswazi, penda kujifunza kwa wenzako na ukipata fursa tembea kweny mahotel makubwa kujifunza, halaf usisahau kile kijiko kidogo cha gesi kwaajili ya kupashia
IMG20230720133025.jpg
 
Kwavile Binadamu hawezi kutaga yai haimaanishi hawezi kuona viza...

Kufungua biashara au project yoyote unahitaji mtaji lakini vitu kama ujuzi, wateja wa kile unachokifanya na sehemu husika ni muhimu kuliko hata pesa (na vyote hivyo hapo juu ni mtaji, Ujuzi, Sehemu Husika na Wateja) ambazo ni muhimu kuliko hata Pesa... ; Sasa wewe kama hauna hivyo vingine hata ukipewa bilioni kadhaa utaziunguza...
Haujawahi kufanya biashara narudia tena mfano kufungua duka la viatu unahitajika ujuzi upi?
 
Hapo mtaji kutosha au kutotosha itategemeana na upande wa location, je banda unalo? Kama hauna unataka liwe la muundo gan? Ukifanikiwa kumiliki banda tu au frem hapo hata 50k unaanza nayo kwa chips, zingatia usafi pia nenda na wakati (usasa) usifunge chips au mishkaki kwenye gazeti tumia foil,vyombo tumia vya kisas usituwekee visahani vya plastik na grass za bati au vikombe vya plastik hata kama banda litakuwa uswazi, penda kujifunza kwa wenzako na ukipata fursa tembea kweny mahotel makubwa kujifunza, halaf usisahau kile kijiko kidogo cha gesi kwaajili ya kupashia View attachment 2972806
Nimekupata vyema Mkuu

Ahsante
 
Haujawahi kufanya biashara narudia tena mfano kufungua duka la viatu unahitajika ujuzi upi?
Unafungua duka kuajiri mtu / unafungua duka kuuza wewe ? Kuuza wewe unahitaji salesperson skills, kuajiri man management katika manunuzi ya viatu unahitaji fashion sense unahitaji kujua trends unahitaji ku-strike a bargain..... na hapo juu nimeongelea ujuzi, wateja, location (sehemu husika) kwamba huenda vikawa ni vya maana kuliko hizo pesa (sababu mtaji ni zaidi ya pesa)

Hivyo viatu kama ni mzuri katika kuuza, na ninajua wateja na fashion trends na taste za watu naweza kwenda kwenye mitumba nikachukua mguu mmoja wa kiatu au kupiga picha na ku-advertise kwa wadau wengi bila kununua hivyo viatu (pesa ya bundle na nauli tu kwenda kwa wadau) na kama nina mtaji wa uaminifu naweza kupewa mzigo kwa mali kauli nikatembeza maofisini....

Ila kama sijui fashion trends na taste za watu sina wateja na mimi na kuuza ni mbingu na dunia hata nikileta container la viatu huenda vikaishia kupata buibui kwenye location ya wapenda ndala mimi nimewaletea designers shoes.....
 
Fun
Fungua biashara zote mbili kwa mtaji huo huo

Ila kuna jamaa anaitwa@dr namugari analiiuza wazo zuri la biashRa mtafute

Kuanzisha saloon inaweza kuwa garama zaid kuliko kuanzisha biashara ya chips. Sema kama analocation nzuri aanzishe biashara vibanda viwli vya chips kwa mtaji huo huo wa 2M
 
Unafungua duka kuajiri mtu / unafungua duka kuuza wewe ? Kuuza wewe unahitaji salesperson skills, kuajiri man management katika manunuzi ya viatu unahitaji fashion sense unahitaji kujua trends unahitaji ku-strike a bargain..... na hapo juu nimeongelea ujuzi, wateja, location (sehemu husika) kwamba huenda vikawa ni vya maana kuliko hizo pesa (sababu mtaji ni zaidi ya pesa)

Hivyo viatu kama ni mzuri katika kuuza, na ninajua wateja na fashion trends na taste za watu naweza kwenda kwenye mitumba nikachukua mguu mmoja wa kiatu au kupiga picha na ku-advertise kwa wadau wengi bila kununua hivyo viatu (pesa ya bundle na nauli tu kwenda kwa wadau) na kama nina mtaji wa uaminifu naweza kupewa mzigo kwa mali kauli nikatembeza maofisini....

Ila kama sijui fashion trends na taste za watu sina wateja na mimi na kuuza ni mbingu na dunia hata nikileta container la viatu huenda vikaishia kupata buibui kwenye location ya wapenda ndala mimi nimewaletea designers shoes.....
😆😆😆😆ndio maana nikakuambia wewe haujawahi kufanya biashara yeyote sijui kwanini unabisha ,, sio kila mada uwe unacomment nyingine ziache tu unajidhalilisha
 
Hio pesa haiwezi kukusaidia kama huna

-Passion na hio biashara ..

-Huna experience na hio biashara..

-Kama hujawahi kuifanya kabisa hio biashara ..

-location ya kufanyia biashara kama sio nzuri ....

Kiufupi hizo biashara zote Ni ngumu Sana na kuna asilimia 90%ya kupoteza hio pesa yote ukiwa unaanza ,kama Ni mgeni so hakikisha hukati tamaa ,unapesa nyingine pembeni ya kujazia ..

Speaking from experience nilishawahi kufanya biashara ya chips na ilikufa so najua kwanin ilikufa ....na najua nilikosea wapi na wengi wanaaoanza asilimia 100% wanakutana na niliyokutana ....
 
Unajua kuna mdau alisema kwamba yeye ni mtu mwenye Hekima kuliko wote Duniani sababu anajua kwamba hajui kwahio anaendelea kujifunza kuliko wale ambao wanadhani wanajua hivyo kuendelea kuishi na kutokujua kwao.... Kuna wahenga huko Baghdad walisema usimuulize muuza nyama (butcher) jinsi ya kufanya biashara ya Almasi...; Kila kazi ina siri zake na ujanja wake.....

Ngoja nikupe scenario ya kitu ulichosema (Ujuzi) kwanza nianzie kwenye kazi ambayo mleta uzi ameongelea alafu nije yako uliyosema Kufungua duka la Viatu halihitaji Ujuzi....

Tuseme huyu bwana anafungua banda la chips anamweka kijana pale ambaye ni mjuzi wa kupika chips na madiko diko yote..., kwa bei za kawaida huenda akawa anamlipa elfu nne au chini ya hapo kwa siku...; huyu kijana ndio anajua masoko, anapigiwa simu alete huku na kule na ndiye anajua kutengeneza hizo chips...., Kijana huyu ana-uwezo muda wowote kuchukua namba za wale wateja au kabla hajahama akawaambia kwamba nahamia sehemu fulani au Bar fulani; Kijana huyu bila mtaji wowote wa pesa (bali mtaji wa ujuzi / utaalamu) anaweza kwenda kwenye Bar akaongea na mwenye bar kusimamimia Jiko / Kununua Jiko akawa anapika chips hapo labda kwa mapatano ya kumlipa mwenye Bar kiasi fulani kwa siku baada ya mauzo..., In short kijana huyu kaweza kufanya alichofanya bila kuwa na mtaji wa pesa bali utaalamu wake....

Sasa tuje kwenye viatu ambayo umesema haiitaji ujuzi wowote (unless neno ujuzi hata haujui maana yake); Mkuu hivi unajua tu hata upangaji viatu kwenye frame kuna watu wanafuatilia saikolojia ya mnunuzi..., vipi unapanga viatu vya bei kiasi gani wapi ili kuvutia watu wa aina gani kuingia dukani ?, vitu kama rangi zipi zina-attract vipi wateja ? Unajua bila kujua machimbo au ni aina gani za muuzaji gani ni nzuri au za nani hazidumu unaweza kununua makapi ? Unajua labda kuna vitu seasonal vinavyotoka na ni wakati gani ? Sikukuu kipindi cha watoto kuanza shule n.k....; Unajua kuna sehemu labda watu wenye pesa ukiuza bei ndogo hawachukui sababu ya status au perception ya cheapness kwao ni turn-off....

Mkuu neno Secrets of the Trade halikuja kwa bahati mbaya unaweza ukawa na kila kitu sawa na mwenzako unashangaa yeye anatoboa wewe unafeli unadhani amekwenda kwa waganga kumbe anajua siri ya urembo....

Na nikirudi kwenye statement yangu ya kwanza kabisa....; Amini usiamini kuna vitu ambavyo ni muhimu na unaweza ukafanikiwa ukiwa navyo hivyo kuliko hata hio Pesa.....; Location, Wateja, Ujuzi..., Sasa bila kujua mleta uzi hivyo anavyo kiasi gani ni vigumu kumwambia anahitaji kiasi gani..., ukiwa location nzuri una ujuzi na wateja wapo huenda usihitaji hata pesa ya kununulia viazi na kuku (unachukua mali kauli sokoni kwa muuzaji asubuhi ukishauza jioni unamlipa); Tofauti na hapo na mapesa yako unaweza kununua gunia mwenyewe na huenda hizo chips zikalala na kuoza.... Au ukaweka kijana ananunua mayai yake na viazi vyake anauza wewe ukija unakuja viazi vyako na mayai yako unaambiwa hakuna wateja..., in short unakuwa umempangia yeye frame...

Katika ususi kuna dada hana hata saloon yake yeye ni mwendo wa kupigiwa simu na kuwatembelea watu kufanya shughuli hio (kwa huyu mtaji wake ni ujuzi wake) hata akiweka hema au meza uchochoroni wateja watamfuata....
 
Hio pesa haiwezi kukusaidia kama huna

-Passion na hio biashara ..

-Huna experience na hio biashara..

-Kama hujawahi kuifanya kabisa hio biashara ..

-location ya kufanyia biashara kama sio nzuri ....

Kiufupi hizo biashara zote Ni ngumu Sana na kuna asilimia 90%ya kupoteza hio pesa yote ukiwa unaanza ,kama Ni mgeni so hakikisha hukati tamaa ,unapesa nyingine pembeni ya kujazia ..

Speaking from experience nilishawahi kufanya biashara ya chips na ilikufa so najua kwanin ilikufa ....na najua nilikosea wapi na wengi wanaaoanza asilimia 100% wanakutana na niliyokutana ....
Tuambie ulikutana na nini Mkuu?
Na wapi ambapo unajua ulifeli?
Na ni kipi hiko kwa 100% naenda kukutana nacho kwenye biashara hizo?
 
inawezekana kabisa ila itategema location tu kuna mahali bei ya vyumba iko juu mfano saloon kuna ukarabati mwingi manunuzi ya vifaa pia ko unaweza kuta 3m inakata
 
Unajua kuna mdau alisema kwamba yeye ni mtu mwenye Hekima kuliko wote Duniani sababu anajua kwamba hajui kwahio anaendelea kujifunza kuliko wale ambao wanadhani wanajua hivyo kuendelea kuishi na kutokujua kwao.... Kuna wahenga huko Baghdad walisema usimuulize muuza nyama (butcher) jinsi ya kufanya biashara ya Almasi...; Kila kazi ina siri zake na ujanja wake.....

Ngoja nikupe scenario ya kitu ulichosema (Ujuzi) kwanza nianzie kwenye kazi ambayo mleta uzi ameongelea alafu nije yako uliyosema Kufungua duka la Viatu halihitaji Ujuzi....

Tuseme huyu bwana anafungua banda la chips anamweka kijana pale ambaye ni mjuzi wa kupika chips na madiko diko yote..., kwa bei za kawaida huenda akawa anamlipa elfu nne au chini ya hapo kwa siku...; huyu kijana ndio anajua masoko, anapigiwa simu alete huku na kule na ndiye anajua kutengeneza hizo chips...., Kijana huyu ana-uwezo muda wowote kuchukua namba za wale wateja au kabla hajahama akawaambia kwamba nahamia sehemu fulani au Bar fulani; Kijana huyu bila mtaji wowote wa pesa (bali mtaji wa ujuzi / utaalamu) anaweza kwenda kwenye Bar akaongea na mwenye bar kusimamimia Jiko / Kununua Jiko akawa anapika chips hapo labda kwa mapatano ya kumlipa mwenye Bar kiasi fulani kwa siku baada ya mauzo..., In short kijana huyu kaweza kufanya alichofanya bila kuwa na mtaji wa pesa bali utaalamu wake....

Sasa tuje kwenye viatu ambayo umesema haiitaji ujuzi wowote (unless neno ujuzi hata haujui maana yake); Mkuu hivi unajua tu hata upangaji viatu kwenye frame kuna watu wanafuatilia saikolojia ya mnunuzi..., vipi unapanga viatu vya bei kiasi gani wapi ili kuvutia watu wa aina gani kuingia dukani ?, vitu kama rangi zipi zina-attract vipi wateja ? Unajua bila kujua machimbo au ni aina gani za muuzaji gani ni nzuri au za nani hazidumu unaweza kununua makapi ? Unajua labda kuna vitu seasonal vinavyotoka na ni wakati gani ? Sikukuu kipindi cha watoto kuanza shule n.k....; Unajua kuna sehemu labda watu wenye pesa ukiuza bei ndogo hawachukui sababu ya status au perception ya cheapness kwao ni turn-off....

Mkuu neno Secrets of the Trade halikuja kwa bahati mbaya unaweza ukawa na kila kitu sawa na mwenzako unashangaa yeye anatoboa wewe unafeli unadhani amekwenda kwa waganga kumbe anajua siri ya urembo....

Na nikirudi kwenye statement yangu ya kwanza kabisa....; Amini usiamini kuna vitu ambavyo ni muhimu na unaweza ukafanikiwa ukiwa navyo hivyo kuliko hata hio Pesa.....; Location, Wateja, Ujuzi..., Sasa bila kujua mleta uzi hivyo anavyo kiasi gani ni vigumu kumwambia anahitaji kiasi gani..., ukiwa location nzuri una ujuzi na wateja wapo huenda usihitaji hata pesa ya kununulia viazi na kuku (unachukua mali kauli sokoni kwa muuzaji asubuhi ukishauza jioni unamlipa); ukiwa hivyo hauna hata ukinunua gunia mwenyewe huenda hizo chips zikalala na kuoza.... Au ukaweka kijana ananunua mayai yake na chips zake anauza wewe ukija unakuja viazi vyako na chips zako..., in short unakuwa umempangia yeye frame...

Katika ususi kuna dada hana hata saloon yake yeye ni mwendo wa kupigiwa simu na kuwatembelea watu kufanya shughuli hio (kwa huyu mtaji wake ni ujuzi wake) hata akiweka hema au meza uchochoroni wateja watamfuata....
Dogo acha maneno mengi ambayo ni pumba tupu mimi naitwa mnachihanguu nipo soko la mtwara nina duka la viatu na duka la vifaa vya ujenzi na mji wa tunduru nako nina duka la pembejeo za kilimo kwahiyo ninapokuambia kuwa biashara ni mtaji uwe unajua unaeongea nae ni mtu wa aina gani...kama wapo wa mtwara humu watakuwa wanayajua maduka yangu kwasababu ni maarufu hapa sokoni,Mimi sijasomea nadharia za kipuuzi kama zako bali mimi nipo uwanja wa vita kabisa
 
Back
Top Bottom