Iran inaripotiwa kupanga kushambulia Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
600
1,840
Iran inaripotiwa kupanga kushambulia Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora makali zaidi na yenye kusafiri kwa kasi na mlipuko mkubwa kuliko kawaida kulenga maeneo ya kimkakati ndani ya Israel.

-Mifumo ya vita vya kielektroniki vya Iran inasonga mbele karibu na Ghuba ya Uajemi, ambayo inaashiria aina fulani ya shughuli za kijeshi. Huwenda Iran imejipanga kwa mashambulizi ya anga na kudhibiti njia ya maji.

-Hii yote ni kwa ajili ya Kujibu shambulio la Israel karibu na ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kuua wanachama wengi wa ngazi za juu wa IRGC.

-CIA inadaiwa kuifahamisha Israel kwamba Iran itashambulia Tel Aviv ndani ya saa 48 zijazo.

1712172052611.png
 
IsraelWarRoom,...

-Iran inaripotiwa kupanga kushambulia Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora makali zaidi na yenye kusafiri kwa kasi na mlipuko mkubwa kuliko kawaida kulenga maeneo ya kimkakati ndani ya Israel.

View attachment 2953249
Kwahiyo Israel ilivyoshambulia Iran iliyegemea ipewe zawadi au?
 
Israel huwa inaiona Iran ni babu yake, miaka nenda rudi huwa ni kuwachokoza Iran, mara kuua askari wa vyeo vya juu, mara kuua wanasayansi, yaani vijamaa vichokozi sana.

Sasa waajemi nao wamechoka wameona ngoja kwanza wawafundishe adabu kidogo, sina mashaka na uwezo wa Iran kijeshi, Israel itapondwa ichakae.

Haiwezekani kinchi kila siku uchokozi.

Hata ujerumani ilikua hivyo, leo hii imetulia, Japan leo hii imetulia, bado hivyo vijinga vigongwe vikae kimya.
 
IsraelWarRoom,...

-Iran inaripotiwa kupanga kushambulia Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora makali zaidi na yenye kusafiri kwa kasi na mlipuko mkubwa kuliko kawaida kulenga maeneo ya kimkakati ndani ya Israel.

-Mifumo ya vita vya kielektroniki vya Iran inasonga mbele karibu na Ghuba ya Uajemi, ambayo inaashiria aina fulani ya shughuli za kijeshi. Huwenda Iran imejipanga kwa mashambulizi ya anga na kudhibiti njia ya maji.

-Hii yote ni kwa ajili ya Kujibu shambulio la Israel karibu na ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kuua wanachama wengi wa ngazi za juu wa IRGC.

-CIA inadaiwa kuifahamisha Israel kwamba Iran itashambulia Tel Aviv ndani ya saa 48 zijazo.

View attachment 2953249
Iran ikibaki kimya itaonekana dhaifu, lazima itatafuta namna ya kulipiza
 
Iwe kweli sasa, na sio vitisho tu.

Out of topic👇
Iftar ya Ramadhan iliyoandaliwa na Biden katika IKULU ya White House ilighairiwa kwa sababu hakuna Waislamu waliokubali mwaliko huo

Hivi ndivyo tunapaswa kushikamana na kuwa wamoja ndugu zangu waislam

Allah awalinde, awahifadhi na awape ushindi dhidi hao maadui wakubwa waliolaaniwa
 
Narudia tena ,watu waache kujitoa ufahamu na kuiona Israel ni nchi ya kupigwa na Iran, nchi yenye nyuklia utaipigaje uifute? Yasije yakatokea kama ya mwaka 1967 na 1973
 
Gharama ya Vita zote hizi, Israel vs Hamas (Gaza), Russia vs Ukraine na nyingine zitakazo fuata, Wahanga (wanao umia zaidi) ni Third Countries.
Wanaumia kwa ujinga wao, Badala kutafuta njia za kujitegemea wameamua kuwa mategemezi, ndio maana hata hawajua wafanye nini vita kama hii inapotokea, wanaunga mkono na hawaungi mkono, inategemea na wanaongea na nani.

Third world countries walitakiwa hata kwa umoja na wao wangetengeneza hata risasi, lakini hawana mchango wowote kwnye vita hii, sasa watapataje pesa za vita na hawatengenezi hata mpini wa bunduki?
 
Back
Top Bottom