Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,990
- 46,767
Tukio la Jana la Israel kushambulia kwa ndege nchini Iran kujibu shambulizi la drones la Iran lililotangulia ni la kiwango cha juu kuashiria vita kamili . Hili Shambulizi lilipangwa kwa mkakati kama vile jeshi lililoko vitani serious na sio kama michezo ya kidali poo anayojaribu kufanya Iran. Hili ni shambulizi la mkakati mpana ukilitizama kwa sababu
Moja, Kuna chenga ya kijeshi waliofanyiwa Iran, ''military deception''(MILDEC) na serikali ya Israel. Chenga ya kijeshi ni kitendo cha kumuaminisha kiuongo adui kwamba utafanya au hautafanya jambo fulani ili kumchanganya afanye namna itakavyokuwa na faida kwako, ni kama kumpoteza maboya. Baada ya shambulio la Iran serikali ya Israel ilikaa vikao vingi na taarifa za mwisho za vikao hivyo zilizotoka ziliashiria Israel hawatafanya shambulizi lolote ndani ya Iran hivi karibuni lakini muda mfupi tu wameshambulia. Hii ni tofauti na vile Iran ilivyofanya shambulizi la kupanga la droni na kulitekeleza kwa siku nzima ikiwapa Israel na washirika wake muda mrefu wa kutosha kujipanga kukabiliana nalo.
Mbili, wamepiga karibia katikati kabisa ya Iran na zaidi wamepiga eneo muhuimu na la kimkakatil la Iran kijeshi na kiulinzi. Isfahan ni eneo ambalo kuna miradi ya nuclear, kambi kubwa ya jeshi na viwanda vya uzalishaji silaha zikiwemo droni. Hili ni onyo kwa Iran kwamba wamedhamiria vita na wanaweza kufika na kupiga popote katika nchi hiyo yenye ukubwa wa eneo mara mbili ya Tanzania.
Tatu, Israel wamepiga nchi tatu kwa wakati mmoja kwa mkupuo. Katika siku moja wameshambulia Syria, Iraq na Iran kuwaonyesha wa-Iran kwamba wako tayari kwa lolote.
Sasa tutegemee majibu kutoka kwa Iran.
Nne, Israel imeonyesha kwamba inaweza kufanya maamuzi yake peke yake kama nchi huru bila kujali washirika wake wa Marekani na Ulaya linapokuja suala la ulinzi, vita na pride ya nchi yao. Pamoja na msimamo wa Marekani na Uingereza wa kwamba hawataiunga Israel katika mashambulizi ya Iran kwa sasa, Israel imeendelea mbele na kufanya mashambulizi yenyewe kama ilivyopanga na kuona inafaa bila kujali msimamo wa washirika wake.