Imebidi nihamie kwangu ghafla kumkwepa mdada kausha damu

Wakuu poleni na mishe za hapa na pale. Sio mwandishi mzuri sana. Nimeona leo nishee nanyi kisa cha kumalizia chumba kimoja kwenye mjengo wangu mpya kumkimbia huyu singo mama.

Mwaka jana mwezi wa sita nilikutana na huyu bidada mrembo wa kuvutia kwa nje mahala ambapo nilikua nikienda mara kwa mara kuchukua mizigo yangu ninayoagiza kutoka DSM.
Ndipo nilipokumbana nae na kuanza mazoea nae hadi ikafika hatua akawa anafika gheto na kulala kabisa, hasa usiku wa kuamkia Jumapili ambapo ofisi ilikua haifunguliwi.

Wakati akiwa anatimba magetoni alinipiga tafu kama kufua kudeki na kuosha vyombo. Na mimi sikusita kumpa huduma zake kama kusuka, pamba na bili zake za maji na umeme. Ana mtoto ambae yupo kwa mama ake mzazi, hayo ni madai yake sina udhibitisho.

Sasa mwezi wa tisa mwaka jana akaanza tabia ya kupokea mizigo yangu na kwenda nayo kwake. Nikawa naifuata na kuchukua hapo kwake.

Siku niliyoagiza brender 3 in 1 akaichukua na kuipeleka kwake na kuanza kuitumia bila mimi kujua. Niliihitaji, akanambia ataileta coz alikua anaitest ili nae aagize. Muda kama wa wiki 2 ukapita hola bila ya yeye kuileta. Kumkumbusha akajichekeshachekesha akisema "usijali kama ni juisi nitakutengenezea uwe unakuja kubeba. Nikapotezea.

Next kimbwanga nilivyoagiza tv, hqpo mwanzo nilikuwa na ka inchi 32, akaniazima madai kwamba kaichoka inch 19 yake so siku nikiihitaji ni mwambie. Ilipofika desemba nikamwambia anipatie nataka niipeleke bush kwa wazee wawchane na chogo HITACHI, zikaanza drama mara ooh nunua nyingine hii niachie mambo yake bado hayajakaa vizuri.

Katikati kwenye hiyo miezi ya 9 mpaka januari kukawa sasa na tabia ya kuagizwa yani akipiga simu akauliza uko wapi ukimtaji location ni utaagizwa vitu vya kupeleka kwake, mara dawa ya mbu, mara vikorokoro kibao, utazunguka maduka ya vipodozi atake sabuni hii mara nivideo call niione.

Akija magetoni iwe hela yoyote ameiona sehemu yoyote atapita nayo huku akijitabasamisha.
Ukifika kwake utasikia naomba nipeleke sehemu ninapoweka muvi za kutafsiriwa ni uswahilini huko hata sehemu ya kugeuza gari ni shida. Nilishawahi ng'oa bamper la nyuma.

Mara kadha anasisitiza niende kwake ila pamekaa kiuswahili Uswahili kiasi kwamba ukifika hapo utapishana na makarai, watoto waanze kukusalimia huku wanarudiarudia salamu. Siku moja nikamuuliza umepapendea nini huku, akajibu pamechangamka. Dah! Nilichoka.

Mwezi wa 2 mwaka huu nikaona isiwe tabu ipo siku niaazimwq moyo na asirudishe. Nikaamua kwenye mjengo ni malize chumba kimoja nihame maana hapa kashapajua kuhama hama ni kitu sipendi kabisa. Hapa nipo kwangu kajaribu kunitaka afike nimegoma, mizugo kule nabadili jina na boda ndo anaifuata.

Ogopa! Jichanganye!
Ova
Mkuu pole na hongera kwa kulikwepa li toxic shangazi!

Ukiona mwanamke ana sura ya kuvutia na kila kitu kuweza kuvutia mwanaume yeyote na kisha anaishi peke yake, elewa kuwa mwanamke huyo ana kasoro.

Kasoro inayosemwa 'kasoro' huwa aidha ni tabia isiyorekebishika ama maumbile yake ya ndani ni mfupa unaowashinda mafisi.

Na usije ukajiona mjuaji na una uwezo wa kuwawin wanaume wengine kwakumpata yeye hapana, wengi walishajaribu wakashindwa kwa kunyoosha mikono yao juu.

Hata hivyo mbona umechelewa sana kuchukua maamuzi sahihi ya kiume kama hayo uliyoyachukua bwana mdogo?

Anachukua vitu vyako kwa njia ya kuazima kisha anaving'ang'ania, linawezekanaje hilo likarudiwa zaidi ya mara moja?

Halafu risiti za kupokelea mizigo yeye alikuwa anazipataje?

Una mapungufu mengi sana ambayo naweza nikakuhoji huku nikikushangaa kwa kushindwa ku handle hawara asiye mke wako.

Umeshapata somo na tayari umejifunza rangi halisi za single mother na wanawake wengi waliopo mitaani ma gold digger!

Unapendwa kwa ajili ya pesa pamoja na vitu vyako, haupendwi kwa kanuzi za kimapenzi za kiasilia hapana.

Ushauri wangu kwako, kuwa serious ya kuvunja mahusiano hayo ili uweze kutengeneza maisha yako ya sasa na ya baadaye.

Ikiwezekana tafuta mke uoe ili kujiepusha na aina hiyo ya wapenzi mamumiani wanyonya damu.
 
Mkuu pole kwa kulikwepa li toxic shangazi!

Ukiona mwanamke ana sura ya kuvutia na kila kitu kuweza kuvutia mwanaume yeyote na kisha anaishi peke yake, elewa kuwa mwanamke huyo ana kasoro.

Kasoro inayosemwa 'kasoro' huwa aidha ni tabia isiyorekebishika ama maumbile yake ya ndani ni mfupa unaowashinda mafisi.

Na usije ukajiona mjuaji na una uwezo wa kuwawin wanaume wengine kwakumpata yeye hapana, wengi walishajaribu wakashindwa kwa kunyoosha mikono yao juu.

Hata hivyo mbona umechelewa sana kuchukua maamuzi sahihi ya kiume kama hayo uliyoyachukua bwana mdogo?

Anachukua vitu vyako kwa njia ya kuazima kisha anaving'ang'ania, linawezekanaje hilo likarudiwa zaidi ya mara moja?

Halafu risiti za kupokelea mizigo yeye alikuwa anazipataje?

Una mapungufu mengi sana ambayo naweza nikakuhoji huku nikikushangaa kwa kushindwa ku handle hawara asiye mke wako.

Umeshapata somo na tayari umejifunza rangi halisi za single mother na wanawake wengi waliopo mitaani ma gold digger!

Unapendwa kwa ajili ya pesa pamoja na vitu vyako, haupendwi kwa kanuzi za kimapenzi za kiasilia hapana.

Ushauri wangu kwako, kuwa serious ya kuvunja nahusiano hayo ili uweze kutengeneza maisha yako ya sasa na ya baadaye.

Ikiwezekana tafuta mke uoe ili kujiepusha na aina hiyo ya wapenzi mamumiani wanyonya damu.
Noted.
Risiti zipo ndani ya boksi
 
Risiti zimo ndani ya box sawa, mzigo ukishatumwa huwa unajulishwa kwa njia gani?

Njia hizo zilikuwa zina leak vipi mpaka yeye ajue na kuwahi kupokea mzigo?

Hilo ndiyo swali la msingi ungeweza kunijibu.
Mizigo ikipokelewa ofisini huwa wanatoa taarifa kupitia namba ambazo zimeandikwa. Kutokana na mazoea ikitokea hali ya kubeba mizigo na kuichukulia kwake. Pitia maelezo hapo juu mkuu
 
Okay pongezi ila sasa ulikuwa unataka umkule bure? Acha woga wew ungemchanatu kwamba nini unataka nin hutak akizingua hapo ndio ubwage
 
Watu kama hao kubadilika ni ngumu huyo kashindikana kuanzia ngazi ya fsmilia Binti aliyelelewa na Maadili Mazur na akawa sikiliza wazazi lazima atakuwa na tabia nzuri na muoga kuchukua vitu vya watu.
 
Hajaliwa bure, nae alikua mnufaika wa mfuko wangu kwenye mambo mbalimbali
 
Watu kama hao kubadilika ni ngumu huyo kashindikana kuanzia ngazi ya fsmilia Binti aliyelelewa na Maadili Mazur na akawa sikiliza wazazi lazima atakuwa na tabia nzuri na muoga kuchukua vitu vya watu.
Sijajua kama atabadilika, ila kuna vitu kama tshirts na pensi na vitu vidogovidogo alivyobeba sija weka hapo. Huenda ni tabia yake ya asili ya kukusanya vya watu.
 
Wakuu poleni na mishe za hapa na pale. Sio mwandishi mzuri sana. Nimeona leo nishee nanyi kisa cha kumalizia chumba kimoja kwenye mjengo wangu mpya kumkimbia huyu singo mama.

Mwaka jana mwezi wa sita nilikutana na huyu bidada mrembo wa kuvutia kwa nje mahala ambapo nilikua nikienda mara kwa mara kuchukua mizigo yangu ninayoagiza kutoka DSM.

Ndipo nilipokumbana nae na kuanza mazoea nae hadi ikafika hatua akawa anafika gheto na kulala kabisa, hasa usiku wa kuamkia Jumapili ambapo ofisi ilikua haifunguliwi.

Wakati akiwa anatimba magetoni alinipiga tafu kama kufua kudeki na kuosha vyombo. Na mimi sikusita kumpa huduma zake kama kusuka, pamba na bili zake za maji na umeme. Ana mtoto ambae yupo kwa mama ake mzazi, hayo ni madai yake sina udhibitisho.

Sasa mwezi wa tisa mwaka jana akaanza tabia ya kupokea mizigo yangu na kwenda nayo kwake. Nikawa naifuata na kuchukua hapo kwake.

Siku niliyoagiza brender 3 in 1 akaichukua na kuipeleka kwake na kuanza kuitumia bila mimi kujua. Niliihitaji, akanambia ataileta coz alikua anaitest ili nae aagize. Muda kama wa wiki 2 ukapita hola bila ya yeye kuileta. Kumkumbusha akajichekeshachekesha akisema "usijali kama ni juisi nitakutengenezea uwe unakuja kubeba. Nikapotezea.

Next kimbwanga nilivyoagiza tv, hqpo mwanzo nilikuwa na ka inchi 32, akaniazima madai kwamba kaichoka inch 19 yake so siku nikiihitaji ni mwambie. Ilipofika desemba nikamwambia anipatie nataka niipeleke bush kwa wazee wawchane na chogo HITACHI, zikaanza drama mara ooh nunua nyingine hii niachie mambo yake bado hayajakaa vizuri.

Katikati kwenye hiyo miezi ya 9 mpaka januari kukawa sasa na tabia ya kuagizwa yani akipiga simu akauliza uko wapi ukimtaji location ni utaagizwa vitu vya kupeleka kwake, mara dawa ya mbu, mara vikorokoro kibao, utazunguka maduka ya vipodozi atake sabuni hii mara nivideo call niione.

Akija magetoni iwe hela yoyote ameiona sehemu yoyote atapita nayo huku akijitabasamisha. Ukifika kwake utasikia naomba nipeleke sehemu ninapoweka muvi za kutafsiriwa ni uswahilini huko hata sehemu ya kugeuza gari ni shida. Nilishawahi ng'oa bamper la nyuma.

Mara kadha anasisitiza niende kwake ila pamekaa kiuswahili Uswahili kiasi kwamba ukifika hapo utapishana na makarai, watoto waanze kukusalimia huku wanarudiarudia salamu. Siku moja nikamuuliza umepapendea nini huku, akajibu pamechangamka. Dah! Nilichoka.

Mwezi wa 2 mwaka huu nikaona isiwe tabu ipo siku niaazimwq moyo na asirudishe. Nikaamua kwenye mjengo ni malize chumba kimoja nihame maana hapa kashapajua kuhama hama ni kitu sipendi kabisa. Hapa nipo kwangu kajaribu kunitaka afike nimegoma, mizugo kule nabadili jina na boda ndo anaifuata.

Ogopa! Jichanganye!
Ova
Hivi tunasemaga humu ishu za single maza mnaonaga ni masihara sio?Bora umeamini lkn
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom