Imebidi nihamie kwangu ghafla kumkwepa mdada kausha damu

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
6,299
47,335
Wakuu poleni na mishe za hapa na pale. Sio mwandishi mzuri sana. Nimeona leo nishee nanyi kisa cha kumalizia chumba kimoja kwenye mjengo wangu mpya kumkimbia huyu singo mama.

Mwaka jana mwezi wa sita nilikutana na huyu bidada mrembo wa kuvutia kwa nje mahala ambapo nilikua nikienda mara kwa mara kuchukua mizigo yangu ninayoagiza kutoka DSM.

Ndipo nilipokumbana nae na kuanza mazoea nae hadi ikafika hatua akawa anafika gheto na kulala kabisa, hasa usiku wa kuamkia Jumapili ambapo ofisi ilikua haifunguliwi.

Wakati akiwa anatimba magetoni alinipiga tafu kama kufua kudeki na kuosha vyombo. Na mimi sikusita kumpa huduma zake kama kusuka, pamba na bili zake za maji na umeme. Ana mtoto ambae yupo kwa mama ake mzazi, hayo ni madai yake sina udhibitisho.

Sasa mwezi wa tisa mwaka jana akaanza tabia ya kupokea mizigo yangu na kwenda nayo kwake. Nikawa naifuata na kuchukua hapo kwake.

Siku niliyoagiza brender 3 in 1 akaichukua na kuipeleka kwake na kuanza kuitumia bila mimi kujua. Niliihitaji, akanambia ataileta coz alikua anaitest ili nae aagize. Muda kama wa wiki 2 ukapita hola bila ya yeye kuileta. Kumkumbusha akajichekeshachekesha akisema "usijali kama ni juisi nitakutengenezea uwe unakuja kubeba. Nikapotezea.

Next kimbwanga nilivyoagiza tv, hqpo mwanzo nilikuwa na ka inchi 32, akaniazima madai kwamba kaichoka inch 19 yake so siku nikiihitaji ni mwambie. Ilipofika desemba nikamwambia anipatie nataka niipeleke bush kwa wazee wawchane na chogo HITACHI, zikaanza drama mara ooh nunua nyingine hii niachie mambo yake bado hayajakaa vizuri.

Katikati kwenye hiyo miezi ya 9 mpaka januari kukawa sasa na tabia ya kuagizwa yani akipiga simu akauliza uko wapi ukimtaji location ni utaagizwa vitu vya kupeleka kwake, mara dawa ya mbu, mara vikorokoro kibao, utazunguka maduka ya vipodozi atake sabuni hii mara nivideo call niione.

Akija magetoni iwe hela yoyote ameiona sehemu yoyote atapita nayo huku akijitabasamisha. Ukifika kwake utasikia naomba nipeleke sehemu ninapoweka muvi za kutafsiriwa ni uswahilini huko hata sehemu ya kugeuza gari ni shida. Nilishawahi ng'oa bamper la nyuma.

Mara kadha anasisitiza niende kwake ila pamekaa kiuswahili Uswahili kiasi kwamba ukifika hapo utapishana na makarai, watoto waanze kukusalimia huku wanarudiarudia salamu. Siku moja nikamuuliza umepapendea nini huku, akajibu pamechangamka. Dah! Nilichoka.

Mwezi wa 2 mwaka huu nikaona isiwe tabu ipo siku niaazimwq moyo na asirudishe. Nikaamua kwenye mjengo ni malize chumba kimoja nihame maana hapa kashapajua kuhama hama ni kitu sipendi kabisa. Hapa nipo kwangu kajaribu kunitaka afike nimegoma, mizugo kule nabadili jina na boda ndo anaifuata.

Ogopa! Jichanganye!
Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom