SoC03 Ili kuondoa Urasimu na Uzembe kwenye Ofisi za Umma, napendekeza Serikali ifanye yafuatayo

Stories of Change - 2023 Competition

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,734
UTANGULIZI : Kumekuwepo na malalamiko mengi sana kutoka kwa watanzania kuhusu utendaji kazi wa maafisa wa serikali wakiwa ndani ya ofisi za Umma.

Hii kero imekuwa ya muda mrefu na ambayo imepelekea urasimu mkubwa mno ndani ya taasisi baadhi za serikali.

Unaingia ndani ya ofisi badala upate huduma unakuta watu ambao walipaswa wakupatie hiyo huduma wanapiga soga maasa ya kazi bila kuwa na wasiwasi wala woga wowote,

Muda ambao huyo mtumishi alipaswa kusaidia watu 20 ndani ya dakika 10, kutokana na uzembe wa kutoa huduma mnajikuta mnakalishwa saa nzima bila sababu za msingi.

Taasisi zote kubwa za serikali zimekuwa zikilalamikiwa sana na wananchi bila kupatiwa ufumbuzi. Hapa Afrika hasa Tanzania ili kuwafanya wazembe wawajibike na kuonyesha utawala bora ni lazima serikali kuwa wakali na kusimamia sheria pamoja na kanuni za utumishi.

Watumishi wengi siku hizi kwakuwa wanaamini wanao uhakika wa mishahara imekuwa ni mazoea kufanya kazi kwa kujivuta kana kwamba walilazimishwa kuzifanya kazi hizo.

Ili kuondoa uzembe na urasimu napendekeza serikali ifanye yafuatayo.

1. Kuwalipa watumishi wa Umma kwa masaa.

Hii itaongeza chachu ya ufanyaji wa kazi kwa watumishi na kupusha uzembe wa wazi kabisa,kiburi cha kupokea mshahara mwisho wa mwezi kimekuwa mwiba mkali kwa watanzania wanaohitaji huduma kutoka kwa watumishi wazembe.

Kwakuwa mtumishi anajua mwisho wa mwezi anaingiziwa mshahara kwenye akaunti ya benki,unakuta anafanya kazi kwa kujisikia kana kwamba amelazimishwa kuifanya kazi hiyo,uzembe kama huu hata serikali imeshindwa kabisa kuuzuia inabaki inawatazama tu watumishi wazembe.

Sasa kulipwa kwa saa nadhani itawafanya wafanyakazi wengi kuchangamka kwasababu akizembea kidogo imekula kwake,kama wenzetu wameweza hili jambo kwanini kwetu lishindikane?.

Suala hili halitahusisha Taasisi zote za Kijeshi kwasababu za kiusalama ila taasisi nyingine zote watendaji walipwe kwa Masaa.

2. Kupiga marufuku watumishi wa Umma kuzungumza na simu masaa ya kazi.

Ili kuendana na kasi ya viwango ya utoaji wa huduma kwa wananchi napendekeza serikali kupiga marufuku inayoambatana na sheria kali kwa watumishi wa umma kutimia simu masaa pendekezwa ya kazi

Hii itaondoa urasimu kwa wananchi na matatizo yanaweza kupungua kabisa,simu zitakazoruhusiwa na sheria ni zile za ofisini tu,lakini simu binafsi zisiruhusiwe hadi muda wa kazi kupita.

Hili tatizo la kuongea na simu masaa ya kazi limekuwa sugu na lililokosa jawabu, unakuta mtumishi amewagandisha walaji kwenye foleni kisa tu yeye anaongea na simu eidha na mpenzi wake au mtu wake wa karibu huku wakipiga michapo na umbea, hii dharau imekosa kabisa utatuzi na ndiyo maana natoa mapendekezo haya.

3. Kuweka muda maalumu kwa watumishi wa Umma kupata chakula wakiwa maofisini.

Kumekuwa na tatizo kubwa mno miongoni mwa watumishi kufunga ofisi kiholela kwa kigezo cha kwenda kupata chakula kumbe ni uongo unakuta kaenda kwenye mambo yake binafsi,

kibaya zaidi unafika ofisini unamsubiri mtumishi huyo zaidi ya saa 2 unakuta hajatokea,akitokea bado anafanya kazi utadhani amelazimishwa,hili halikubaliki hata kidogo,ili kuondoa huu urasimu napendekeza kuwe na muda maalumu wa kupata chakula kisheria na kikanuni kwenye taasisi husika, muda ambao hauta muumiza mtumishi mwenyewe wala mpokea huduma.

Napendekeza iwe dakika 30 ,nusu saa inatosha kabisa kwa mtumishi kupata chakula na angalau kupata hewa ya upepo.Baada ya hapo anapaswa kurudi ofisini kuwatumikia watanzania.

Hili inapaswa alifahamu kabisa kama miongoni mwa kanuni na sheria kabla ya kuajiriwa ili kama akishindwa awapishe wataoweza kutekeleza sheria na kanuni hizo.

Hatuwezi kuendelea kuwakumbatia watumishi wazembe walioaminiwa na serikali ili kuwapunguzia wananchi kero badala yake watumishi hao ndiyo wamegeuka kuwa kero.

Watanzania waaminifu wapo wengi na waliosoma hivyo sioni sababu ya serikali kuwakumbatia watumishi mizigo maofisini.

4. Kuwaongezea malipo watumishi wote wa Umma wanaofanya vizuri katika utumishi.

Hii itasaidia sana kuondoa uzembe na urasimu serikalini kwasababu watumishi wengi wazembe watakuwa na shauku ya kujipatia nyongeza ya malipo endapo wakifanya vema katika utumishi.

Kuna mwalimu mmoja anaitwa YUSUF PANGOMA,huyu yeye amekuwa chachu kwa walimu wenzie pamoja na watanzania kwa ujumla kwasababu amekuwa na utumishi wa kutukuka,kupitia yeye walimu wenzie pia wameamua kuiga anachokifanya si kwa walimu wa Tanzania pekee bali imevuka hadi mipaka ya Tanzania, mwalimu kama huyu kwa nini asiongezewe malipo?

,Hivyo kuondoa urasimu kwa watumishi mtumishi kama huyo mwalimu anapaswa aongezewe malipo, yawezakuwa malipo anayolipwa ni kulingana na daraja la elimu yake lakini ili kuongeza ufanisi na kuondoa urasimu watumishi wanaojituma ni busara kuongezewa malipo ili wale wavivu na wazembe waige mfano ili kuondoa urasimu.

Haya yakifanyika kwa hakika hakutakuwa na urasimu kwenye ofisi za umma na badala yake tutashuhudia uwajibikaji wa kiwango cha juu kutoka kwa watumishi na pia kutapunguza malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wengi wamekuwa hawaridhishwi na huduma za kiutendaji kwenye ofisi za umma

.Naiomba serikali ijaribu kuyafanyia kazi ingawa si yote na kwa wakati mmoja ila wajaribu kuchukua yenye umuhimu na kuanza nayo.

Nawatakia siku njema.
 
Acheni ujinga na wewe niserekali yako
 
Wachapa kazi watakao pewa nyongeza utakuta ni marafiki au walio mhonga bosi tena wavivu na wazembe, hayo yameonekana wakati wa opras!
 
Serikali ivunje mwamba wa mamilioni wanayolipwa wabunge kwani wao ndio chanzo cha shida nchi hii
 
Back
Top Bottom