Waziri Silaa ataka wasajili wa hati kuacha urasimu na lugha chafu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,922
12,197
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaz, Jerry Silaa amewataka Wasajili wa Hati wa Ofisi za Kamishna wa Ardhi Dar es salaam na Pwani kuacha Urasimu kabla hajaanza kuwachukulia hatua kali za kinidhamu.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati alipofanya kikao maalumu na wasajili hao katika Ofisi yake iliyopo Jijini Dar es Salaam, Januari 19, 2024 na kuwapa siku mbili tu za kujibadilisha kwa kutoa miamala ya hati haraka na kwa wakati bila urasimu.

Amesema Watumishi hao wamekithiri kwa lugha chafu na zisizo ridhisha kwa Wananchi wanaotaka huduma katika ofisi hiyo ambayo ndio inahusika na kuandaa na kutoa hatimiliki za ardhi pamoja na miamala mingine ya kisheria kwa wananchi.

Aidha, amesema hatomuamisha mtu kwa uzembe na badala yake atawachukulia hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi watakao bainika na maelekezo hayo ameishampa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Amesema “Nawapa onyo la mwisho, mbadilike, mnachowafanyia Wananchi ni Urasimu, mmezoea ukifanya kazi vibaya utahamishwa, kitakachofanyika ni adhabu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi.

“Kila mtu anatakiwa kuhakikisha meza yake ni nyeupe, Mwananchi akileta muamala wake kama haupo sahihi mrejeshee au rejesha katika Idara husika, kama upo sahihi fanyia kazi.”

Natumiwa kila siku malalamiko, nikiyatuma kwenu yanafanyiwa kazi, kwa nini hayo mengine hayafanyiwi kazi, napenda kujipa muda wa kujifunza mnachofanyi Wananchi sio jambo sahihi, mnachokifanya si utawala bora, badilikeni.”
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amewataka Wasajili wa Hati wa Ofisi za Kamishna wa Ardhi Dar es salaam na Pwani kuacha urasimu kabla hajaanza kuwachukulia hatua kali za kinidhamu.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati alipofanya kikao maalumu na wasajili hao katika Ofisi yake iliyopo jijini Dar es salaa na kuwapa siku mbili tu za kujibadilisha kwa kutoa miamala ya hati haraka na kwa wakati bila urasimu.

Amesema watumishi hao wamekithiri kwa lugha chafu na zisizo ridhisha kwa wananchi wanaotaka huduma katika ofisi hiyo ambayo ndio inahusika na kuandaa na kutoa hatimiliki za ardhi pamoja na miamala mingine ya kisheria kwa wananchi.

Aidha, amesema hatomuamisha mtu kwa uzembe na badala yake atawachukulia hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi watakao bainika na maelekezo hayo ameishampa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
tatizo linaanzia hapo. watu idara ya ardhi wanahitaji action. Kusema tu waache urasimu hawataacha maana hapo ndipo wanapopatia rushwa. Weka measures za kuacha urasimu... say KWA MFANO, kuwa hati lazima iwe processed ndani ya 30 days. short of that unafukuzwa kazi. hakuna hati ambayo itachelewa. Weka TIME LIMITATION AMBAYO IF NOT FOLLOWED CONSEQUENCES WILL FOLLOW THE COURSE!
 
Waziri Slaa njoo Ndachi Dodoma jamaa anaitwa Magige wa Jiji anapandikiza watu kwenye miliki za mashamba yanayobadilika kuwa makazi Kwa kisingizio Jiji linachukuwa asilimia 30
Bila aibu shamba linagawanywa kwakutumia kampuni ya jamaa yake Mafuru bila mwenyeshamba kuhusishwa kinachofanyika nikuonyeshwa mgawanyo na wewe kupewa kiwanja kimoja au viwili

Mh Waziri wahi utusaidie
 
Back
Top Bottom