SoC04 Maeneo matano ya kimkakati ambayo serikali inaweza kuyawekea mkazo kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma na rushwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Xpertz

Member
May 3, 2024
8
6
1.IUNDWE TUME YA UDHIBITI UBORA WA MIKATABA NA USHAURI KWA SERIKALI (National Commission for Contracts Review and Consultation)

Iwe taasisi huru yenye jukumu la kupitia mikataba yote ya kimkakati inayohusu fedha za umma. Taasisi hiyo ihusike kuchambua kwa kina mikataba yote kwa mapana yake na kutoa mapendekezo ya kitaalamu kwa serikali kabla ya utekelezaji wa mikataba yote ya kimkakati. Tume hii iundwe na wataalamu wabobevu (Think tanks) katika nyanja mbalimbali pia wawe watu wenye rekodi nzuri ya uadilifu kwenye utumishi wao. Tume hii ifanye kazi chini ya kiapo maalumu kwa taifa na uzalendo. Tume iwe na nafasi ya kushauri vinginevyo iwapo itaona mkataba hauna tija kwa taifa.

Mradi wowote wa serikali usitekelezwe bila mikataba yake kupitishwa na tume hii. Mikataba itayopitishwa na tume hii iwe imekidhi viwango vya ubora na ndio iwe miongozo kwenye ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi husika kuhakikisha viwango na ubora uliokusudiwa unazingatiwa. Miongoni mwa wajumbe katika tume hii wawe maafisa usalama wa siri ili kuepusha baadhi ya wajumbe kupenyeza ajenda za maslahi binafsi. Tume hii itaisaidia serikali kuepuka kuingia mikataba mingi ya hasara kwa fedha za umma, utekelezaji wenye mapungufu mengi na uchakachuaji wa mikataba katika miradi.

Tume hii itumike kufanya mchujo wa mwisho wa wakandarasi na wazabuni kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa. Nakala za mikataba yote inayopitishwa na tume hii ziwe miongozo ya ubora wa utekelezaji na vipewe vyombo vya ufuatiliaji ikiwemo taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini(TAKUKURU) na ofisi ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa ajili ya ufuatiliaji katika utekelezaji.

2. MFUMO WA AJIRA NCHINI UBORESHWE
Napendekeza mfumo wa ajira nchini uwe mseto(mchanganyiko wa maafisa usalama wa siri na watumishi wa kawaida wa umma). Taasisi nyeti ikiwemo TAKUKURU, jeshi la polisi, usalama wa taifa n.k kuwe na ajira za kimkakati za siri ambapo katibu mkuu utumishi atawapangia maafisa usalama hao waliosoma kada mbalimbali tofauti na mafunzo ya kijeshi kwenye taasisi na halmashauri mbalimbali nchini kwenda kufanya majukumu ya kawaida na watumishi wa umma ili kuweza kupata kwa urahisi taarifa zote za siri za ubadhirifu wa fedha za umma na rushwa. Baada ya muda fulani wawe wanahamishwa kuepusha kushtukiwa na watumishi wengine wa kawaida. Katibu mkuu utumishi ndio awe anaratibu ajira hizo maalumu za watendaji hao.

3. MFUMO WA UKAGUZI NA UDHIBITI WA FEDHA ZA UMMA UBORESHWE
Napendekeza ofisi ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za seikali (CAG) iongezewe bajeti na nguvu zaidi kuweza kufanya ukaguzi katika hatua tatu za utekelezaji wa miradi ya kimkakati yaani hatua ya awali, hatua ya msingi na hatua ya sekondari ili kuweka maana halisi ya UDHIBITI badala ya kusubiri ukaguzi wa jumla wa CAG ambao tayari unatoa taarifa ya hasara iliyokwisha kupatikana. Nashauri ukaguzi kwenye miradi yote ufanyike kwenye hatua tatu za utekelezaji katika asilimia 20%, katika asilimia 60% na katika asilimia 100% na iwapo mapungufu yakibainika katika hatua husika hatua kali zichukuliwe haraka. Hii itaisaidia miradi ya serikali kufanyika kwa wakati, ubora na usahihi kama ilivyokusudiwa kwenye mikataba.

4. MAFISADI WAFILISIWE NA MALI ZAO KUTAIFISHWA
Napendekeza mafisadi wote wanakaokutwa na hatia ya ubadhirifu wa fedha za umma sambamba na hukumu za vifungo jela na faini, pia mali zao zitaifishwe, hii itasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watumishi na watu wote kutambua kwamba ubadhirifu wa fedha za umma hatia yake ina matokeo makali mno.

5. MTAALA WA ELIMU YA RUSHWA UWE WA LAZIMA KWENYE ELIMU
Wizara ya elimu iboreshe somo la uraia sambamba na kufundisha uzalendo lijikite kuelimisha madhara ya rushwa kwa jamii kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu.

Kiambatanisho: Picha kwa hisani ya Global Tv (ripoti ya CAG)

FB_IMG_1714746547069.jpg
 
Iwe taasisi huru yenye jukumu la kupitia mikataba yote ya kimkakati inayohusu fedha za umma. Taasisi hiyo ihusike kuchambua kwa kina mikataba yote kwa mapana yake na kutoa mapendekezo ya kitaalamu kwa serikali kabla ya utekelezaji wa mikataba yote ya kimkakati. Tume hii iundwe na wataalamu wabobevu (Think tanks) katika nyanja mbalimbali pia wawe watu wenye rekodi nzuri ya uadilifu kwenye utumishi wao. Tume hii ifanye kazi chini ya kiapo maalumu kwa taifa na uzalendo. Tume iwe na nafasi ya kushauri vinginevyo iwapo itaona mkataba hauna tija kwa taifa.
Sawa kama lengo pia ni kuongeza wigo wa taasisi na ajira.
Tofauti na hivyo ni kuwa na kanuni zinazotaka wasomi kupewa wizara za taaluma zao. Naamini hadi hivi sasa tunao wasomi wa kufaa kabisa kutoa maamuzi yenye tija kwa taifa. Off course kuwawajibisha pale wanapokiuka. Hili jambo la Mbunge ni ajue kusoma na kuandika tu limepitwa na wakati au unasemaje mtoa mada.

Tukiachana na hilo, kamati za bunge zinafanya kazi gani. Na ninaamini kamati huwaweka wasomi na wataalamu wa mkataba husika pamoja. Uwajibikaji ndio dhima ya kufanyiwa kazi.
. Miongoni mwa wajumbe katika tume hii wawe maafisa usalama wa siri ili kuepusha baadhi ya wajumbe kupenyeza ajenda za maslahi binafsi.
Nzuri hiii kwa uwajibishaji

kuweka maana halisi ya UDHIBITI badala ya kusubiri ukaguzi wa jumla wa CAG
Nakubali. Yaani kila taasisi itende na kufanyia kazi kile inachojinasibu kuwa yenyewe Ni.

Taasisi ikijinasibu kuwa mimi ni taasisi ya kudhibiti vyura, kweli tusione chura anarukaruka mtaani bila utaratibu. La sivyo mkurugenzi wake awajibike kumuwajibisha huyo deiwaka aliyeruhusu chura azurure katika eneo lake la kazi.✔
4. MAFISADI WAFILISIWE NA MALI ZAO KUTAIFISHWA
Napendekeza mafisadi wote wanakaokutwa na hatia ya ubadhirifu wa fedha za umma sambamba na hukumu za vifungo jela na faini, pia mali zao zitaifishwe, hii itasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watumishi na watu wote kutambua kwamba ubadhirifu wa fedha za umma hatia yake ina matokeo makali mno.
Ahsante sana. Again uwajibishwaji wa waliopaswa kuwajibika na wakazembea.

Yaani kama TAKUKURU amekamilisha kazi yake akampatia polisi/mahakama, isipotendewa kazi basi huyo mkuu wa mahakama awajibike kumuwajibisha mtendaji aliyepaswa kuendesha mashtaka ya kumfunga huyo mtu. Na ikiwa mtu huyo akafungwa halafu akatoka kiajabu basi mkuu wa magereza awajibishwe kumuwajibisha aliyehusika..... sasa ndugu zangu swali linabaki je? Akija Rais akamtoa kwa msamaha🤔🤯🤣🤣........... jibu lipo, awajibishwe na katiba. Katiba inaweza kuweka labda alielezee bunge na umma sababu za kumtoa sio mambo magumu ata.

Lakini kimsingi mtoa mada, una maoni mazuri sana.
 
Back
Top Bottom