Ijue teknolojia ya OLED inayotumika katika kutengeneza TV za kisasa.

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
1,274
3,335
Teknolojia hii ya utengenezaji wa screen za TV ilianzia zamani miaka ya 1950 lakini matumizi yake yameanza miaka ya 2010 kama zilivyo teknolojia nyingi ambazo huchukua miaka hadi kufanyiwa kazi kwa ufanisi, LG Electronics ndio kampuni ya kwanza kuzalisha TV za aina hii mwaka 2010 ila mpaka sasa kampuni nyingi zinatengeneza OLED TVs ikiwemo Samsung ambao walinunua hii technology kutoka LG, sambamba na Hisense, Sony, Panasonic na Philips, hizi kampuni mbili za mwisho zinafanya vizuri kwenye soko la TV kwa nchi za mabara mengine pia.

(OLED technology enable emissive displays which means that each pixel is controlled individually and emits its own light unlike LCDs in which light come from backlighting unit). OLED ni teknolojia ambayo pixel za TV zinajiwasha na kujizima zenyewe. Pixel ni vibox vidogo sana vinavyopatikana kwenye kioo ambavyo kwa pamoja ndio huwezesha picha kuonekana kwenye kioo; hata ukiangalia screen ya laptop au TV kwa makini utaona kama kuna drafts boxes, pixel zinavyokua nyingi ndivyo picha inazidi kuwa na quality. Ndio maana ukiingia you tube ukiona resolution ya 1920 * 1080 hizo ndo idadi za pixel na unavozidi kupanda hadi 4k to 8k.

TV ambazo sio OLED pixel zake zinamulikwa na mwanga ambao hutoka nyuma ya pixel, chogo unaloliona kwenye TV pale nyuma kuna taa inayomulika kwenye screen ili tuone picha, ila OLED TV pixel zake zinajiwasha na kujizima zenyewe hapa ndipo tunapata picha yenye ubora wa hali ya juu kwani pixel zikimulikwa kutoka nyuma kule kuwaka na kuzimwa kwa mwanga kunapunguza ufanisi wa muonekano wa picha kwenye pixel.

Kama hujawahi kuona OLED TV fanya uione, kampuni nyingi zinatengeneza hizo TV, pita brandshop za LG, Samsung na Hisense au siku ukienda Mlimani City pita maduka ya electronics ulizia OLED TV, ni TV nyembamba sana unaweza kuta inazidi wembamba simu yako uliyonayo mkononi, kwa chini pale ndio inakua na unene kidogo ila ina muonekano mzuri sana na quality ya picha haipo kwenye TV nyingine yoyote. Wembamba wa screen yake pia umezifanya ziwe maarufu sana sokoni kwani hata ukiifunga ukutani unakua kama umebandika kioo.

Tuone LG OLED Series, natumia LG maana ndio kampuni ya kwanza kuja na TV za OLED;

Hawa jamaa wamezipa majina OLED TV kulingana na features ila zimetofautiana kwa uchache sana kiasi kwamba kwa mtumiaji wa matumizi ya kawaida unaweza chagua kati ya zote, kuna Z2, G2, C2, CS na A2; Z2 pekee ndio in 8K zinazobaki ni 4k, content nyingi kwa sasa hata online ni 4k na hapa bongo bado production ya content zenye 4k

Isipokua A2 yenye refresh rate ya 60Hz zilizobaki zina refresh rate ya 120Hz, hii ni perfect kwa gamers, lakini pia A2 pekee ndio ina a7 processor zilizobaki zinatumia a9 ambayo ndio powerfull processor kwa sasa, hii inakupa perfect speed ukiwa unatumia application za kwenye TV yako hasa online.

Huwezi zungumzia bidhaa za kisasa bila kutaja AI, TV hizi ni AI smart kuanzia processor na operation kiujumla, sound output yake ni 7.1.2 kwani ina 2.2Chanel speaker zenye 40W ila kwa television yoyote hasa wapenzi wa movies sound bar za ukweli ndo zitakupa sauti nzuri.

LG wamekuja na OLED TVs kwa inches 43” 48” 55” 65” 77” 83” 88” na 97”, kwa soko la East Africa nyingi zinazouzwa ni kuanzia 55” ambapo madukani zinauzwa kuanzia 3M mkiongea vizuri ila zinauzwa kuanzia 3.5 kwa maduka mengi, hii ni kwa 55”, kwa 65” bei yake ni kuanzia 5M to 6M na 77” bei yake ni kuanzia 9.5M mkiongea vizuri.

Kiafya pia OLED TV zimepunguza kiasi cha mwanga wa bluu kwa 50%, kama wewe ni content creator au director hizi ndio TV za kufanyia kazi kwani zitakupa kile ambacho mtazamaji atakiona ukisha upload kazi yako online i.e YouTube
Teknolojia inavyokua kwa kasi sijui ni TV gani zitakuja baada ya hizi sababu kama wameweza kutengeneza TV yenye wembamba kama simu ya kiganjani na perfect color kinachofuata haitakua ajabu zaidi?

Yours trully
Koffi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom