Huyu mjamzito amenyanyaswa na wahudumu wa mwendokasi hapa Mbezi Mwisho mpaka akazimia

Aramun

JF-Expert Member
Nov 8, 2023
228
982
Nianze na Swali: Watoto wa kuanzia miaka mingapi wanapaswa kulipa nauli za mwendokasi?

Mida ya hii jioni huyu dada mjamzito alikuwa na mwanaye wakiwa wanasubiri mwendokasi za Kivukoni. Mtoto alikuwa na miaka kama mitano hivi.

Alipoingia kwenye gari cha ajabu mhudumu anayescan ticket akawa analazimisha yule dada amlipie na huyo mtoto nauli, ilhali ni mtoto mdogo anayeweza kupakatwa.

Pamoja na dada kuwaambia atampakata lakini walimgomea, ndipo ikatokea kukusukumana hapa na pale mpaka ikabidi watu wote watoke kwenye mwendokasi.

Haijalishi ni nani alikuwa na kosa hapa, lakini sijapenda namna huyu dada mjamzito alivyokuwa treated, maana wamemuharrass sana mpaka dada wa watu akazimia, huku mwanaye akilia kwa uchungu.

Hili shirika japo ni la umma, lakini staffs wake wana zero customer care, hawana utu na hawajali wateja hata kama ana hali inayohitaji kusaidiwa.

Mtoto waliyekuwa wanafosi alipie👇
IMG_20240410_212911.jpg

Mama mjamzito akiwa ameanguka chini👇
IMG_20240410_214717.jpg

IMG_20240410_214849.jpg

Mwendokasi iliyokuwa inaenda Kivukoni👇

IMG_20240410_213450.jpg
 
Na nyie mpo, hii ndo reflection ya nguvu kazi kuja kuikomboa Tanzania? Pumbavu kabisa.

1. Mlishindwa kupambana?
2. Mlishindwa kumtetea?
3. Mlishindwa kumlipia Mtoto?

Kama hamuwezagi ku act huko, hizi habari za kifala msituletee sisi wanaume tuliokamilika.

Mnashindwa kumprotect Mama mja mzito mwenye mtoto Mdogo?
 
Yaani kabla haujachukua camera yako kupiga picha zako za kipumbavu kama hizi ili uwahi kutuletea umbea jf ungetoa iko kiasi kidogo cha nauli ya mwendokasi ukamsaidia uyo mama mjamzito hayo yote yangetokea? Haya kazimia mko busy kupiga picha hamjui kapatwa na hali gani mpaka amepoteza fahamu, itachukua muda gani kurecover, badala mum mumchukue haraka kwenye kituo cha afya kilicho karibu cha muhimu umeona upige picha! Takataka kabisa
 
Miaka mitano ni darasa la kwanza huyo hivyo anapaswa alipie mia mbili.

Kumpakata na kumlipia NAURI havihusiani kabisa kwani Kila mtu anaweza kumpakata mtoto wake hata kama anamiaka saba au 14 .

Mjamzito atii Sheria bila shurti.Kuwa mjamzito asijifiche kwenye uhalifu WA kutolipia NAURI kisa mjamzito eti aonewe huruma HAPANA.

Bora angeomba asaidiwe tu kuwa Hana NAURI anaomba msaada Kwa mwanae.Hapo angesaidiwa lakini pesa unayo unaleta ujuaji WA Sheria ni kujitakia matatizo kama hayo.

Kwa hapo siwalaumu wahudumu WA mwendokasi WALIKUWA sahihi.
 
Una watoto wangapi wana 5 yrs na wapo la kwanza?
 
Haijalishi ni nani alikuwa na kosa hapa, lakini sijapenda namna huyu dada mjamzito alivyokuwa treated, maana wamemuharrass sana mpaka dada wa watu akazimia, huku mwanaye akilia kwa uchungu.

Hili shirika japo ni la umma, lakini staffs wake wana zero customer care, hawana utu na hawajali wateja hata kama ana hali inayohitaji kusaidiwa.
Nauli ya mtoto ni roughly jero, mngemsitiri mjamzito na kumpuuza huyo mhudumu
 
Back
Top Bottom