Hivi ni mimi tu haya maisha yanataka kunikataa?

Nimeajiriwa ngazi ya chini serikalini lakini naona mambo hayaendi kabisa.
mwanzo nilipoajiriwa nilikuwa nafuraha lakini siku zinavyoenda mambo yanaenda ndivyo sivyo.

Nina mawazo kuacha kazi changomoto sijajipanga.
Niwaza hadi nimefika mwisho sijui nifanyeje, nina madeni mengi, na hapo hata sijaoa sina hata mtoto wa kusingizia.

Nina watu zaidi ya watano wananitegemea hapo nyuma kwa sababu ndiye hustler (mpambanaji) wa kwanza huko nyumbani yani nikiyumba mimi ndiyo kwishaa kabisa.

Mazingira ya nyumbani tena ndio hivyo yaajabu na nimepambana hata niyaweke vizuri lakini ndio hivyo tena bado nimekwama.

Nimekaa hivi naangalia Magh, Mash, Kas, Kusini hakueleweki.
Nimejikuta najitenga na watu kwa sababu nasikia hadi aibu hali ya maisha.

Kazi yenyewe ni ngumu makorokocho mengi inachosha haina hata maslahi wakuu.

Ukizaliwa familia maskini aise halafu huna mtu wa kukushika mkono kutoboa unatumia nguvu kubwa sana. Nimejaribu kuwaza kuacha kazi ila shida sina msingi tena.
Wakuu kazi yangu ya ualimu duu sijui nifanyeje kwa kweli.
Acha kabisa kubet
 
Pole mkuu kwa changamoto unayopitia.
Kama mdau alivyosema huenda mikopo ndio inakutesa zaidi kwa maana umekopea mshahara na hela ya mkopo imeisha lakini majukumu yako pale pale na imefikia wakati mshahara hauwezi kukidhi mahitaji.

Usikate tamaa, punguza matumizi yasiyo lazima, punguza kusaidia ndugu pasipo ulazima (kuwa bahiri na ukubali kusemwa na hao utakaowanyima hela). Shida za familia zetu huwa haziishi hasa kwenye extended families, shida zingine ignore sema huna hela hata kama ipo. Kubali nao wapitie kipindi kigumu cha mpito hawatakufa, hii itakupa ahueni ya mzigo kwenye matumizi kwa kiasi kidogo cha pesa unachopata.

Kubali kuwa umekosea mahali fulani jipe mda urekebishe kosa hilo (mpaka utakapomaliza kulipa mkopo).
Jitahidi kulipa madeni uliyokopa, usijaribu kudhulumu uliowakopa bora ulipe kidogo kidogo kuliko kudhulumu.

Punguza matumizi then ufocus kwenye kulipa madeni hasa hasa ya watu binafsi maana kama ni ya benki unakatwa automatically.
Kingine jitahidi kufanya saving hata kama ni ndogo kiasi gani iweke tu at least 10% ya unachopata kama utaweza.

Kwa sasa usifikirie kuacha kazi endelea na kazi ila acha kuwaza kwamba watu wengine watakuonaje kwa hali yako ya sasa. Hayawahusu, ishi maisha yako usiishi watu wanavyotaka uishi, ishi utakavyo kulingana na hali yako.

Nakutia moyo kuwa hayo unayopitia, kwenye maisha hutokea kwa wengine pia. Mwiko kukata tamaa maadamu una afya njema mengine unaweza kuyafix na ukabadilisha kabisa hali uliyo nayo kwa sasa na ikawa historia. Jipe mda!
asante mkuu ubarikiwe
 
Nimeajiriwa ngazi ya chini serikalini lakini naona mambo hayaendi kabisa.
mwanzo nilipoajiriwa nilikuwa nafuraha lakini siku zinavyoenda mambo yanaenda ndivyo sivyo.

Nina mawazo kuacha kazi changomoto sijajipanga.
Niwaza hadi nimefika mwisho sijui nifanyeje, nina madeni mengi, na hapo hata sijaoa sina hata mtoto wa kusingizia.

Nina watu zaidi ya watano wananitegemea hapo nyuma kwa sababu ndiye hustler (mpambanaji) wa kwanza huko nyumbani yani nikiyumba mimi ndiyo kwishaa kabisa.

Mazingira ya nyumbani tena ndio hivyo yaajabu na nimepambana hata niyaweke vizuri lakini ndio hivyo tena bado nimekwama.

Nimekaa hivi naangalia Magh, Mash, Kas, Kusini hakueleweki.
Nimejikuta najitenga na watu kwa sababu nasikia hadi aibu hali ya maisha.

Kazi yenyewe ni ngumu makorokocho mengi inachosha haina hata maslahi wakuu.

Ukizaliwa familia maskini aise halafu huna mtu wa kukushika mkono kutoboa unatumia nguvu kubwa sana. Nimejaribu kuwaza kuacha kazi ila shida sina msingi tena.
Wakuu kazi yangu ya ualimu duu sijui nifanyeje kwa kweli.
Pole Sana .

Ila ungeanza kujikita katika vipaumbele kwanza .

Mfano Una familia ya watu watano wanakutegemea.

Na unaona mshahara hautoshi , hapo jibu linakuja kuwa unabidi kuanza kujijenga kwanza wewe ili usimame then ndo uwasimamishe ndugu zako.

Mshahara wa ualimu ni Mdogo Sana hivyo ungeweza kufikiwa kwa kuweka vipaumbele kwanza.

naweza kusema mkuu kuna mambo hayapo sawa katika mpangalio wako wa mambo ktk uchumi .

Kukopa ni vizuri ikiwa Unaenda kuizalisha hiyo hela
Ila Kutokukopa ni vizuri zaidi ikiwa hauna jambo la msingi unaenda kufanya.

Hivyo usiache kazi Ila punguza matumizi ili yaendane na kipato chako .
 
Maisha bhana muda mwengine hayataki unyooke sanaaaa!

Sijajua kwa kazi za walimu zipoje! Ila kwenye kazi hiyo hiyo kama kuna mianya ya namna fulani ya kupiga wewe jiseti halafu piga.

Muhimu usidhulumu mtu.
 
Regardless of the situation, never give up!

njoo nikukopeshe tena weka kiwanja bondi
ushauri: Ndugu yangu kama unapata mshahara kama 350,000 after tax, chukua 150,000 mapema sana weka Mpesa yani usiiguse hii hela jikaushe kabisa, itakusaidia kuanza maisha mengine baada ya miezi kadhaa..

Any way mimi ni mpambanaji mwenzio.. nilianza biashara ya kausha damu kwa mtaji 40,000 tu sasa hivi nina 2,000,000 na nishanunua kiwanja. nakula navaa nalipa kodi na nasaidia wazazi pia.

Najikausha kama vile sizioni starehe
Screenshot_20240506-114256.jpg
 
Maisha bhana muda mwengine hayataki unyooke sanaaaa!

Sijajua kwa kazi za walimu zipoje! Ila kwenye kazi hiyo hiyo kama kuna mianya ya namna fulani ya kupiga wewe jiseti halafu piga.

Muhimu usidhulumu mtu.
labda uuze boksi la chaki
 
labda uuze boksi la chaki
Kama hali ndiyo hiyo kitu muhimu hapo jijenge wewe mwenyewe kwanza.

Ukishaweza kufika level fulani itakuwa ni rahisi kwako kuweza kuwanyanyua wengine mmoja baada ya mmoja.

Ila kwa sasa hiyo nguvu hauna! Kuwa mbinafsi. Jijenge mwenyewe kwanza.
 
asante kwa ushauri mkuu
 
Huwa nawashangaa sana watu ambao wako kwenye ajira halafu wanawaza kuacha kazi. Wakati kuna watu wanaenda mpaka Kwa waganga ili wapate hiyo ajira. Tatizo linaanzia pale unapojitwika majukumu ambayo yako juu ya uwezo wako mpaka unaingia madeni. Nakushauri usifikirie kuacha kazi. Nitumie ajira uliyonayo kufanikiwa kimaisha. Kama uko mjini omba uhamisho ukae kijijini, Lima mazao kama mpunga, ufuta, alizeti, au Katanga nk. Ukivuna toa shukrani Kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom