Hivi ni mimi tu haya maisha yanataka kunikataa?

philantrhopist

JF-Expert Member
Jun 18, 2023
408
688
Nimeajiriwa ngazi ya chini Serikalini lakini naona mambo hayaendi kabisa.
Mwanzo nilipoajiriwa nilikuwa nafuraha lakini siku zinavyoenda mambo yanaenda ndivyo sivyo.

Nina mawazo kuacha kazi changomoto sijajipanga.
Niwaza hadi nimefika mwisho sijui nifanyeje, nina madeni mengi, na hapo hata sijaoa sina hata mtoto wa kusingizia.

Nina watu zaidi ya watano wananitegemea hapo nyuma kwa sababu ndiye hustler (mpambanaji) wa kwanza huko nyumbani yaani nikiyumba mimi ndiyo kwishaa kabisa.

Mazingira ya nyumbani tena ndio hivyo ya ajabu na nimepambana hata niyaweke vizuri lakini ndio hivyo tena bado nimekwama.

Nimekaa hivi naangalia Magh, Mash, Kas, Kusini hakueleweki.
Nimejikuta najitenga na watu kwa sababu nasikia hadi aibu hali ya maisha.

Kazi yenyewe ni ngumu makorokocho mengi inachosha haina hata maslahi wakuu.

Ukizaliwa familia maskini aisee halafu huna mtu wa kukushika mkono kutoboa unatumia nguvu kubwa sana. Nimejaribu kuwaza kuacha kazi ila shida sina msingi tena.
Wakuu kazi yangu ya ualimu duu sijui nifanyeje kwa kweli.
 
Pole sana mkuu, cha kukushauri hapo lazima uweke bajeti na uwe strict kuifuata mfano mshahara wako ni buku nyumbani tuma 400 matumizi yako binafsi 400 na 200 fanya saving itakusaidia
Ila kwa sasa kutokana na madeni jitahidi usiongeze madeni tena jikite kwenye kulipa kwa kujipa muda hata wa miezi 6 ukimaliza ishi kulingana na kipato ndiyo njia ya kusurvive pekee
 
Mkuu pambana kitaa kigumu bila mishe mimi takribani nina mwaka sas toka nmezinguana na muajiri wangu hizi milion nimekamata san lakini leo ht 10k ni kwa mbinde san na nina mke na mtoto mmoja inafika kipind naamua kubet tu kukuza mtaji ndio nipate hela ya kula.

Shukuru kwa unachokipata kiwe kidg au kikubwa kuna watu tunatafuta ht sehem ya kujishikiza lkn bado hapa nilipo sijala toka jan usiku na hapa nmelala tayar bahati nzur familia nimeisafirisha ili niendelee kujitafuta

SHUKURU MUNGU KWA YOTE
 
Dah Mimi nipo hapa napanga bajeti hio hela mzee
FB_IMG_1714712623750.jpg
 
Mkuu philantrhopist kuwa na chochote ni bora kuliko kukosa chochote, Allah ndiye mwenye kuijua hatima yako. Usiulize sana kichwa wakati mwingine ishi maisha yako halisi usijifananishe na mtu. Akili yako na ubongo wako unakutambua wewe. Kuwa na imani ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anaijua hatima yako. Siku zote mpambanaji hakati tamaa. Think positive and act wisely.
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Pole sana mkuu, cha kukushauri hapo lazima uweke bajeti na uwe strict kuifuata mfano mshahara wako ni buku nyumbani tuma 400 matumizi yako binafsi 400 na 200 fanya saving itakusaidia
Ila kwa sasa kutokana na madeni jitahidi usiongeze madeni tena jikite kwenye kulipa kwa kujipa muda hata wa miezi 6 ukimaliza ishi kulingana na kipato ndiyo njia ya kusurvive pekee
asante mkuu
 
Back
Top Bottom