mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 16,311
- 36,822
Mwaka 1995 Jakaya Kikwete akijifanya ni masikini na Edward Lowassa akinukia noti, walisindikizana kuchukua fomu za kugombea urais, nyuma yao akiwepo king maker Rostam Aziz na Samuel Sitta.
Lowassa aliamua kukodi ndege binafsi chini ya captain Minje baba yake Lilian, walizunguka Tanzania nzima kusaka wadhamini, walikuwa na miaka 42 kwa 45 mtawalia. Wakajiita Boys II Men.
Aliyekodi ndege ni Lowassa Jk alipewa lift tu, makubaliano ni kuwa yeyote ambaye angepita amteue mwenzake kuwa Waziri mkuu na baada ya miaka kumi huyo waziri mkuu agombee urais, hapa ni kama Putin na medinedev wanavyofanyaga.
Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege, na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete, yaani Jakaya.
Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL. JK bila kutambua akampa lift EL kwenye gari aina ya Ssang yong Musso mpaka msasani.
Taarifa zikamfikia mwalimu kuwa Jk kaja na EL, mwalimu akajifanya anatoka nje kwa hasira na kumfokea kuwa amechelewa appointnent atoweke haraka mahali hapo kufumba na kufumbua Jk kwa shingo upande akaondoka bila kujua sababu.
Mwalimu akidhani JK amegundua kosa lake, kumbe wapi, kwenye vikao vya mchujo Jk uso kwa uso tena na mwalimu, na akaulizwa if you become a president who gonna be your prime minister, JK akayakoroka kwa kusema Edward Lowassa, mwalimu akamwambia asante kwa kushiriki ,jina la JK likakatwa kibabe na akapachikwa Benjamin Mkapa.
Matumizi makubwa ya pesa katika kusaka madaraka yalimponza EL.
.....,....Itaendelea