Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Rejea hotuba za Magufuli

nakukumbusha tu

alisema hadharani hakuwa na Mpango wa kuchukua fomu ila alienda Ikulu kumshtaki Saada Mkuya kwa kutompa pesa za kulipa wakandarasi 900 billion , Jk akamuuliza Wewe huchukui fomu ?akamuuliza ninatosha ? akamjibu Wewe kachukue kutosha au kutotosha tutajua Sisi

Hapo maana yake Rais alikuwa na Plan Kadhaa kutokana na yatakayojiri

waki react hivi itakuwa hivi na jinsi walivyo react wakaamua kadri walivyoamua na iliyobaki ni historia

Sina uhakika ila ninaamini

Jakaya, Mkapa, Mangula na Kinana walikaa kama kamati kuamua nani awe nani kwa kutumia report na ushauri wa Mamlaka za kiuchunguzi na pale Dodoma walienda kutekeleza tu maamuzi maana hata Mgombea mwenza Samia anatuambia Kamati kuu walikuwa wanakula biscuit wakati vingunge wanakamilisha taratibu kupitia chumba maalum
Mgufuli ameambiwa suala la kugombea urais kwa mala ya kwanza kikwete akiwa kalazwa nje kwa shida ya tezi dume.
 
Sho...
Nimesoma hayo hapo juu kuhusu Prof. Malima na ningependa na mimi niseme machache niyajuayo kuhusu Prof. Malima.

Katika Bunge mwezi June 1994 Prof. Malima akiwa Waziri wa Fedha alileta mswada kuwa misamaha yote ya kodi iwe chini ya Waziri wa Fedha badala ya kuiachia iwe katika mamlaka nyingi tofauti.

Maadui zake ndani ya Bunge wakalalamika kuwa Prof. Malima alikuwa anataka kujijengea himaya.

(Kwa nini Prof. Malima alikuwa na maadui ni mada ya kujitegemea).

Hata hivyo fikra zilitulia na mantiki ikatawala kuwa hilo ni jambo jema na mswada ule ukapita.

Baada ya mwezi mmoja kupita wakati Prof. Malima yuko nje ya nchi Baraza la Mawaziri likaitishwa kwa shinikizo la Waziri Mkuu John Malecela akiungwa mkono na mawaziri wanne wakongwe nia ikiwa kugeuza suala la misamaha ya kodi uliopitishwa mwezi mmoja tu uliopita.

Prof. Malima aliporejea nchini na kukuta kuwa uamuzi wa Bunge kuhusu misamaha ya kodi umepinduliwa na Bunge, Prof. Malima alimtahadharisha Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu matokeo ya kwenda kinyume na maamuzi ya Bunge na matakwa ya wahisani.

Rais akaitisha Baraza la Mawaziri lililokaa kwa siku nne.

Prof. Malima alihimili hoja zote kutoka kwa maadui zake katika serikali akitetea uamuzi wa Bunge.

Baada ya siku nne Baraza la Mawaziri lilirejea nyuma katika uamuzi wa Bunge.

Maadui zake waliumia sana na chuki yao dhidi yake ikazidi.

Hayo yote ya kuwa Prof. Malima alikuwa fisadi si kweli.

Prof. Malima hakuwa na mali nimemuona kwa karibu sana nyumbani kwake jirani na Victoria na nimeiona nyumba yake Kisarawe siku ya mazishi yake.

Prof. Malima hakuwa na mali na kama alivyokuwa akipenda kusema katika uhai wake, ‘’Hakula cha mtu.’’

Ametajwa hapa Kikwete kuwa alipewa nafasi ya Waziri wa Fedha badala ya Prof. Malima lakini mwandishi kaishia hapo tu.

Inataka ushughulishe bongo lako ujiulize kwa nini Kikwete?

Yapo mengi.

Kwa nini hakuyasema mengine na ni muhimu katika historia ya Prof. Malima?

Hakuyasema inawezekana kwa kuwa hayajui.

Wewe mzee wewee,wakati mwingine jitahidi kuwa mkweli.kighoma maxima alikuwa bonge la fisadi.
 
Nimefuatilia maandishi mengi ya mwanahistoria huyo na kugundua kuwa mengi ni upotoshaji mkubwa.Hata andishi hili siyo ukweli kwamba Kighoma Malima hakuwa fisadi.

Kwa mwandishi huyo,hakuna Muislamu kiongozi aliyewahi kuwa fisadi.Bali huwa wanaomewa na kubagazwa bila sababu.
Huyo mzee ni takataka tu,hana lolote kbs,yeye kila kitu ni udini tu.
 
Naona zimeanza kugeuzwa stories baada ya hayati kutajwa na kila mtu kua hakua na ubaya wala usaliti. Zimefufuliwa makala za kumsafisha aliechafuka kwenye msiba.

Kiukweli hata Mkwere mwenyewe moyo na nafsi vinamsuta kwa aliyoyafanya kwa Lowassa..

Waliyafanya kwa Mkapa,akaja akayafanya kwa Lowassa, nafikiri pia akayafanya kwa Magufuli.
Mkwere hana nguvu mbele ya wazee wa ccm
 
Uje uweke na stori ya namna Mrisho na Kambarage walivyoingia makubaliano ya kwamba lazima mtoto wa Mrisho aitwaye Jakaya aje kupewa nchi...
Kwani huyo mzee Mrisho alimfanyia nini Nyerere mpaka kukawa na makubaliano hayo?
 
Mwaka 1995 Jakaya Kikwete akijifanya ni masikini na Edward Lowassa akinukia noti, walisindikizana kuchukua fomu za kugombea urais, nyuma yao akiwepo king maker Rostam Aziz na Samuel Sitta.

Lowassa aliamua kukodi ndege binafsi chini ya captain Minje baba yake Lilian, walizunguka Tanzania nzima kusaka wadhamini, walikuwa na miaka 42 kwa 45 mtawalia. Wakajiita Boys II Men.

Aliyekodi ndege ni Lowassa Jk alipewa lift tu, makubaliano ni kuwa yeyote ambaye angepita amteue mwenzake kuwa Waziri mkuu na baada ya miaka kumi huyo waziri mkuu agombee urais, hapa ni kama Putin na medinedev wanavyofanyaga.

Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege, na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete, yaani Jakaya.

Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL. JK bila kutambua akampa lift EL kwenye gari aina ya Ssang yong Musso mpaka msasani.

Taarifa zikamfikia mwalimu kuwa Jk kaja na EL, mwalimu akajifanya anatoka nje kwa hasira na kumfokea kuwa amechelewa appointnent atoweke haraka mahali hapo kufumba na kufumbua Jk kwa shingo upande akaondoka bila kujua sababu.

Mwalimu akidhani JK amegundua kosa lake, kumbe wapi, kwenye vikao vya mchujo Jk uso kwa uso tena na mwalimu, na akaulizwa if you become a president who gonna be your prime minister, JK akayakoroka kwa kusema Edward Lowassa, mwalimu akamwambia asante kwa kushiriki ,jina la JK likakatwa kibabe na akapachikwa Benjamin Mkapa.

Matumizi makubwa ya pesa katika kusaka madaraka yalimponza EL.

.....,....Itaendelea
Chai
 
Yani huu uzi unatuchanganya sana sisi watoto wa 2000 kuna mauongo mengi humu na maukweli pia yani hatuelewi tushike lipi tuache lipi
 
Kuna kipindi nilikuwa nina penda sana kusoma makala zako,lkn nilikuja kugundua wewe mi mtu uliyejaa chuki za udini. Nikaacha kbs.
Yve...
Kuwa mimi nina chuki za udini si kweli.
Ningekuwa hivyo nisingealikwa vyuoni kuzumguza.

Ningekuwa nina chuki za udini nisingealikwa na vyombo maarufu vya habari ulimwenguni kuzungumza.

Nk. nk.

Wewe unaumizwa na kusoma historia ya Waislam Tanzania, historia ambayo ilifutwa isiwepo.

Hili ndilo linalokuumiza.

Sasa kama umeacha kabisa kusoma makala zangu sasa imekuwaje umenisoma?
 
Back
Top Bottom