Fredy Koublani ni mchezaji mzuri sana akitumiwa vizuri ataisaidia sana SIMBA SC atafanya maajabu NBC PL.

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,791
9,568
Mimi naomba nitofautiane kidogo na wadau wengi wa jukwaa hili hasa hasa wana YANGA wenzangu na mashabiki wa simba SC wanaodai Fredy Koublan ni garasa.

Huyu mchezaji namfananisha na the great khali (kwa walioangalia mieleka miaka ya 2005 watakua wanamjua vilivyo)
GridArt_20240501_072215259.jpg

Ana mwili mkubwa, ni mrefu, ameshiba pia ana nguvu ni kama the great khali ambaye ushindi wake WWE huupata kwa advantsge ya umbo lake na mwili wake, mbinu na ufundi sifuri, akikutana nakimtu chenye mwili mdogo kama andunje chenye mbinu alikuwa anapigwa vizuri kabisa japokuwa sio mara zote kijamaa kinaitwa REMYSTERIO si mnakikumbuka?

Fredy huwa anasumbua sana mabeki akiwa na mpira ni ngumu kumpokonya maana ananguvu kama kifaru ila hana skills nzuri za kufunga, hupenya kirahisi ndani ya 18 na ni vigumu kumpiga .mtama au kumpush akaanguka, ili kumuwini inabidi akabwe na watu wanne azingirwe pande zote. Beki kitasa BACCA alimshindwa akatufunga, magoli mengi anayofunga ni ya kuwashinda nhuvu mabeki.

Ushauri wangu huyu mwamba achezeshwe namba 10 kwa sababu hiyo namba inahitaji mtu mwenye misuri na anayeweza kupenya kirahisi ukuta wa beki zote za kati na pembeni,

Atafutwe namba tisa mwingine mwepesi mwenye mbio

Simba itapata matokeo ya haraka

NAWASILISHA
 
Mieleka ni mchezo wa maigizo kama kaole, kumfananisha tu na wacheza mieleka tayari ushamvua nyota.
Hiyo tunaita kufikiria kwa imagination, kwani wewe nikikufananisha na PROFESSOR wa LACASA DE PAPEL haimainishi kuwa ni series ya ukweli sio fiction bali ntakuwa najaribu kuwasilisha wazo kwa kutumia mfano wa kufikirika ili kufikisha ujumbe
 
Wakati wanakuja Fredy na Jobe Mechi za mwanzo niliona jobe mzuri kuliko Freddy ila baadae ndio nimegundua Freddy yuko vzr
 
Sio kwamba sijakuelewa, nimeuelewa vizuri tu. Ni sawa na mtu akusifie kuwa una mpangilio mzuri wa uandishi wa mada zako kama uandishi wa nyimbo za Elton John. Sawa nimekusifia ila nimekusifia kwa kukulinganisha na mwanamuziki ambaye ni shoga. Ukitazama ni kama sifa zina ukejeli ndani yake japo inawezekana sina nia ya kukejeli.

Mwanasoka kusifiwa kwa kulinganishwa na mcheza mieleka, mchezo ambao ni wa kikaole binafsi naona ni sifa zenye kejeli ndani yake. Kuna watu wengi wenye sifa ambazo ukiwatumia kama mfano inapendeza. Mfano drogba, Lukaku, Rooney. Hawa walikuwa na nguvu pia na miili mikubwa.
Wakati ukifika nitakuja kukumbusha
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom