Ufuatao ni 'Mjumuisho' wangu wa 'Kiuchambuzi' baada ya kuiona Simba SC jana katika 'Simba Day' yao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,117
110,510
Heko kwa Msemaji Ahmed Ally amejitahidi, ila kwa Siku zijazo awe na back up ya Mtu mwingine Maarufu, Mchangamshaji na mwenye Sauti ya Juu ya Kimatukio.

Golikipa Beno David Kakolanya ameimarika na Kukomaa vyema ila ajitahidi sana kufanyia Kazi 'Footwork' yake ambayo si nzuri na hata Mwenzake Aishi Manila analo tatizo hili japo Kwake siyo kwa sana.

Beki Mohammed Outarra sina cha Kumdai kwani ni Beki ambaye amekuja Kutibu tatizo Sugu la Simba SC la kutocheza vyema Mipira ya Juu ( Aerial Balls ) ambalo limekuwa likiigharimu kwa muda mrefu. Niseme tu Asante kwa Waliomsajili na nimemkubali 100% zote.

Beki Henock Inonga Baka nilishawahi Kumuandika hapa JamiiForums Kwanza Kukiri kuwa ni Beki Bora na mwenye Kipaji ila nilisema na leo narudia tena kusema kuwa arekebishwe na tabia yake ya Kujiamini kulikopitiliza, kupenda Sifa, Kudekadeka hovyo na kupenda Jukwaa kwa kufanya Upekee.

Henock Inonga Baka asiporekebishwa haraka nina uhakika ama katika Mechi ya Jumamosi na Yanga SC au zile za Klabu Bingwa atakuja Kutugharimu pakubwa na tutajuta.

Kijana Beki wa Kulia Israel Patrick Mwenda sijui mpaka leo kwanini bado yuko Simba SC kwani ameshindwa Kuimarika, anakamia mno na hana Umakini wa Kutosha.

Sioni sababu ni kwanini Mchezaji mahiri David Kameta Duchu tuliyemtoa kwa Mkopo Geita Gold FC ambaye amecheza vyema sana katika Ligi Kuu ya NBC iliyomalizika harejeshwi Simba SC na tumebakia na Beki mbovu kama Israel Patrick Mwenda.

Kwa Mabeki Mahiri na Mafundi akina Kapombe na Tshabalala sina Deni nao kwani bado wapo vizuri na Ninawapenda zaidi.

Kama kuna Mchezaji wa Simba SC ambaye simkubali na nilishangaa kuona Yeye kabakishwa na Thadeo Lwanga kaachwa ni Saido Kanoute.

Kanoute hajui Kukaba na akikaba anakaba kwa Kucheza Rafu ( Faulo ) za Kijinga kama siyo Kipumbavu, anagombana hovyo na Marefa, Mbishi na anachoka ( Tenki linapungua ) mapema sana.

Mchezaji Okra anaonekana na Vitu vingi Mguuni na Kipaji kweli ila ameathirika na Presha ya kutaka kufanya makubwa ndani ya Simba SC kwa muda mfupi kitu ambacho ni Kigumu na with time atakuja Kuweza kufanya kile ambacho amekikamia kutaka kutufanyia wana Simba SC.

Mchezaji Sakho nadhani ni Sikio la Kufa kwani licha ya kuwa na Kipaji Kikubwa ila ni Mbinafsi ( Mchoyo ) na anapenda Chenga ambazo haziisaidii Timu bali zinamsaidia Yeye Binafsi na Utoto wake unaomsumbua. Akibadilika au akibadilishwa atakuja kuwa na Msaada mkubwa wa Ushindi kwa Simba SC yetu. Ana Mbwembwe nyingi zisizo na Faida kwa Klabu na Binafsi huwa ananiboa mno tu.

Mchezaji Okwa ( kutokea nchini Nigeria ) kama wana Simba SC wote tunajitambua basi huyu sasa ndiyo Mfalme mpya ndani ya Simba SC kwani ana Kila Kitu na ni bonge la 'Playmaker' na kwa Uchezaji wake atasumbua sana Uwanjani hasa sehemu ya Kiungo na Ushambuliaji ambayo ndiyo amebobea nayo na anaitendea vyema. Kwa Mpira mkubwa anaoucheza jana nilitamani muda wote awe anapelekewa Mpira ili afanye Maufundi ( Maudambwidambwi ) yake.

Mshambuliaji HATARI Moses Phiri niliyemfahamu Mimi Msimu uliopita alipokuwa Kwao nchini Zambia siyo huyu anayenipa MASHAKA kwa sasa.

Mshambuliaji Mzawa Habib Kiyombo namuona kama tu akirekebishwa hasa Kisaikolojia basi atakuja kuwa Tegemeo na Faida Kubwa katika sehemu ya Ushambuliaji.

Napenda Mikimbio yake, anavyojipanga, Nguvu zake na uwezo wake wa Kupiga Mashuti ya Kulenga Goli.

Mshambuliaji Kibu Denis anaendelea Kuimarika ila naomba tu asaidiwe jinsi ya kujua ni wapi atumie Nguvu na wapi atumie Akili kwani nimegundua ana tatizo Kubwa la kutokujua ni wapi avitumie Kiufasaha vyote hivi Viwili, ila ni Mchezaji muhimu na atatusaidia zaidi Simba SC hasa katika zile Mechi zinazohitaji 'Physical' hasa.

Mwisho nimesikitika sana kuona Wapumbavu fulani ambao wanasema ( wamesema ) kuwa Mzungu Mserbia Dejan Simba SC tumepigwa na kwamba si mzuri.

Sasa leo GENTAMYCINE nawaambieni msiojua Mpira kuwa kama kuna Mchezaji ambaye kama tu akipewa Ushirikiano mzuri na Wenzake, akiyazoea Mazingira ya Tanzania na Ligi yetu, akiaminiwa na asipofanyiwa Mambo ya Uswahili na Wenzake atakuja kuwa Msaada na Tegemeo ni huyu Mserbia Dejan.

Ana Nguvu, Kasi, Mpambanaji halafu anachonivutia ni kwamba hasimami sehemu moja, ana Pumzi na anaweza hadi Kushuka chini kuja kusaidia Kukaba na kuanzisha Mashambulizi.

All in all ni Usajili wa Matumaini ila ninachokiomba hasa kwa Uongozi wa Simba SC na wana Simba SC wote ni Umoja, Nguvu Moja na Ushirikiano mkubwa, Kujitoa na Kupambana kweli ndani na nje ya Uwanja hasa tukitambua kuwa Mpira ni Mchezo wa Vita isiyotumia Silaha za Moto.

Mikakati ya Ubingwa ianze sasa hivi!!!

Cc: Bila bila, Msanii, adriz
 
Kwa sakho hapo ni kweli, yaan ni mtu anayetafuta mafanikio binafsi na sio kitimu. Hili nilishaona tangu msimu uliopita.

Huyu inatakiwa aambiwe ukweli, kuwa hapa yupo kwa team ko acheze kuisaidia team, sio kutafuta fame yake. Na hivi ni km mfalme ndani ya team, ndo anazidi kabisa ubinafsi. Inafika hatua team inakosa ufanisi na matokeo chanya

Inonga kujiamini kunakopitiliza itafika hatua ataigharimu team, penalty zisizo na mpango, au yeye kutolewa nje kwa Umeme.

Kanoute, huyu kaka namkubali sana, na hata kocha maki anamkubali, ndo maana alirudishwa, tatizo la huyu ni 1 tyuuh, anakamia mnoo afu anachoka mapema bas, ila vinginevyo yuko sahihi kwa mtazamo wangu lakini.

Ni hayo tyuuh.
 
Je Cletus Chama nae?
 
Umechambua vizuri mno, wengi tumesema hayo ila kwakuwa unakuwa unashibikia Yanga basi wanaona kama umesema kishabiki kumbe mtu ameongea kwa uhalisia wa timu ilivyo.

Simba warekebishe makosa hayo hasa ubinafsi wa wachezaju wao kujiamini kuliko pitiliza kwa mabeki wao.

Nimesema hapa kuwa kwa nionanyo na kama Simba kama hawatojirekebisha humo, kilio kitakuwa kila wiki.
 
Kwa Dejan Georgijevic nilisema kwenye usajili wake kuwa huyu ni Clinical mbele ya lango.

Kuhusu Israel nilisema toka mwezi wa tatu kwenye Uzi kuwa Hamzidi Chochote David Kameta, ilikuwa wakati mwafaka kurudi kwenye Simba SC.

Kanoute alikuja vema lakini sasa ananipa wasiwasi, na huenda akatafutiwa mbadala..!
 
Kwa sakho hapo ni kweli, yaan ni mtu anayetafuta mafanikio binafsi na sio kitimu. Hili nilishaona tangu msimu uliopita.

Huyu inatakiwa aambiwe ukweli, kuwa hapa yupo kwa team ko acheze kuisaidia team, sio kutafuta fame yake. Na hivi ni km mfalme ndani ya team, ndo anazidi kabisa ubinafsi. Inafika hatua team inakosa ufanisi na matokeo chanya

Inonga kujiamini kunakopitiliza itafika hatua ataigharimu team, penalty zisizo na mpango, au yeye kutolewa nje kwa Umeme.

Kanoute, huyu kaka namkubali sana, na hata kocha maki anamkubali, ndo maana alirudishwa, tatizo la huyu ni 1 tyuuh, anakamia mnoo afu anachoka mapema bas, ila vinginevyo yuko sahihi kwa mtazamo wangu lakini.

Ni hayo tyuuh.
cocastic mpaka sasa ujanitumia ile video ebu ingia dm yangu
 
Israel namtetea kwa performance ya jana alijitahidi sana.
Ule upande aliokuwepo ndo unafanya tumuone hakucheza vyema lakini ni upande ambao kila muda simba walitaka waanzie mashambulizi huko. Lakini pia St George walitaka pia kutumia upande huo kupiga cross. So alikuwa na kazi ngumu ukilinganisha pia siyo mzoefu kama kapombe katika kupanda na akushuka.
Huyu dogo ni potential
 
Back
Top Bottom