Faida yangu kibiashara kwa siku nane inaweza kumlipa Mkuu wa Wilaya mshahara; anapata wapi nguvu yakinifokea?

Mkuu kwa nchi Kama Tanzania mwanasiasa Ana nguvu Sana tena Sana.

Ndo maana wafanyabiashara wote wakubwa kuanzia bakhressa , Mo, Manji ,rostam wanatoa misaada ya pesa huko Ccm ili kulinda Biashara zao.

Hii nchi mbunge wa Ccm anaheshimika Sana achilia mbali RC ,DC.

So be humble and play smart.

Hapa kwetu mamlaka Ina nguvu Sana siuliona magufuli alivyokuwa anawaweka jela matajiri na kuwafilisi pesa zao.

Je wewe Una hela kuwazidi akina MO waliotekwa au kina Rugemarila. Mzee wa FM academia.

Jitihadi uwe unawaza vyema nchi za laana sio sawa na marekani
 
Wafanyabiashara nawaomba tembeeni kifua mbele kwanini ninyi ni matajiri. Ninyi ndio walipa mishahara ya serikali, mnawanunulia viongozi mafuta ya magari, mnawapandisha ndege na kulipa ada za watoto wao.

Kwanini wale mliowaajiri waishi kama wafalme wakati hawana shengeli kama sisi? Tuamke sasa tuache kutembelea mabasi tupande ndege....tuamke sasa tuache kupambana na daladala tununue magari na twende nayo kazini,,,tuamke sasa tuache kula kimaskini tule kitajiri....nk

Hatuwezi kuwaajiri watu then wakawa mabosi zetu, tunachokiburi cha baraka za Mungu katika utafutaji,tunachokiburi cha umoja kama walipa kodi na tunazo kura kama wananchi. Tuanze sasa kujitambua, tudai haki yetu ya kulindwa katika ulipaji kodi na kuheshimiwa na waajiriwa wetu.

Tuache ulimbukeni wakuogopa magari ambayo tumenunua sisi, tuwasimamie waajiriwa hawa waboreshe mazingira ya kazi. Hakuna mfanyabiashara atafukuzwa amekunywa bia ngapi na serikali ila waajiriwa wa serikali watahesabiana vizibo na kuwajibishana kwa sasa hawana ziada.

Jifunze maana ya neno "Mamlaka" na pesa zako zote unaenda kwa nabii na mkeo mnamwagiwa maji feki na pesa mnatoa.
 
Acha woga bro.....kama wananguvu ikifika kipindi kama hiki walete kiburi mtaani sasa waone.

Sasa hivi mtaani kila mwanasiasa anataka mchango na uungwaji mkono wetu wafanyabiashara.

Kama mamlaka ina nguvu kwanini wanakuja kuomba pesa zakuwasaidia wapate mamlaka?
 
Wewe una bunduki na mabomu? lazima uongozwe hakuna namna
Hatuzungumzii vita hapa, tunajadili nafasi ya mfanyabiashara kuishi kama mfalme kwa jasho lake.

Nikibarikiwa kuwa na fedha halali sihitaji kibali cha mwanasiasa au mtawala kufanya matumizi .

Acha fikra zakuwaza kwamba uchumi inalindwa na bunduki
 
Mkuu kwa nchi Kama Tanzania mwanasiasa Ana nguvu Sana tena Sana.

Ndo maana wafanyabiashara wote wakubwa kuanzia bakhressa , Mo, Manji ,rostam wanatoa misaada ya pesa huko Ccm ili kulinda Biashara zao.

Hii nchi mbunge wa Ccm anaheshimika Sana achilia mbali RC ,DC.

So be humble and play smart.

Hapa kwetu mamlaka Ina nguvu Sana siuliona magufuli alivyokuwa anawaweka jela matajiri na kuwafilisi pesa zao.

Je wewe Una hela kuwazidi akina MO waliotekwa au kina Rugemarila. Mzee wa FM academia.

Jitihadi uwe unawaza vyema nchi za laana sio sawa na marekani
Naelewa ana nguvu ila kwa miaka mingi yakuishi kwa hizi fikra za kimaskini na kijamaa tumejikuta tunatafuta fedha kwa jasho then tunatumia kwa shida huku mwansiasa akinamiwiri na mashangingi
 
Wafanyabiashara nawaomba tembeeni kifua mbele kwanini ninyi ni matajiri. Ninyi ndio walipa mishahara ya serikali, mnawanunulia viongozi mafuta ya magari, mnawapandisha ndege na kulipa ada za watoto wao.

Kwanini wale mliowaajiri waishi kama wafalme wakati hawana shengeli kama sisi? Tuamke sasa tuache kutembelea mabasi tupande ndege....tuamke sasa tuache kupambana na daladala tununue magari na twende nayo kazini,,,tuamke sasa tuache kula kimaskini tule kitajiri....nk

Hatuwezi kuwaajiri watu then wakawa mabosi zetu, tunachokiburi cha baraka za Mungu katika utafutaji,tunachokiburi cha umoja kama walipa kodi na tunazo kura kama wananchi. Tuanze sasa kujitambua, tudai haki yetu ya kulindwa katika ulipaji kodi na kuheshimiwa na waajiriwa wetu.

Tuache ulimbukeni wakuogopa magari ambayo tumenunua sisi, tuwasimamie waajiriwa hawa waboreshe mazingira ya kazi. Hakuna mfanyabiashara atafukuzwa amekunywa bia ngapi na serikali ila waajiriwa wa serikali watahesabiana vizibo na kuwajibishana kwa sasa hawana ziada.
We nenda katibiwe Mirembe
 
Hatuzungumzii vita hapa, tunajadili nafasi ya mfanyabiashara kuishi kama mfalme kwa jasho lake.

Nikibarikiwa kuwa na fedha halali sihitaji kibali cha mwanasiasa au mtawala kufanya matumizi .

Acha fikra zakuwaza kwamba uchumi inalindwa na bunduki
Bila risasi na mabomu nani angelipa kodi?
 
K
Naelewa ana nguvu ila kwa miaka mingi yakuishi kwa hizi fikra za kimaskini na kijamaa tumejikuta tunatafuta fedha kwa jasho then tunatumia kwa shida huku mwansiasa akinamiwiri na mashangingi
OK pole Sana mkuu Ila tumia njia ya kuwa positive na kutogambana na hao wanasiasa.

Kwanini nasema hivi.

Mwanasiasa yupo kwa muda tu Leo kesho anatumbuliwa au anakufa au anastafishwa.

So ikiwa biashara yako IPO katika long run surviving usiharibu biashara yako wewe kuwa humble na jishushe. Na play low key .

Nilikuwa Bukoba nimejionea hayo mambo watu wakifanyiwa ubaya na politicians so pole Sana
 
Sawasawa.
Nafikiri hujui maana ya Dola.
Ungejua maana yake wala usingeandika hayo.
Bakhressa ni mtu mdogo sana kwenye hii nchi mbele za Watawala.
Afisa TRA wa ngazi ya juu tuu anaweza kumjambisha achilia mbali wenye serikali
Kwa kuongezea tu amtafute tajiri anayepingana na Serikali kama yupo. Ni kwa kuwa wanajua kumalizwa ni dk tu.
 
Mamlaka ni zaidi ya pesa.
The Rothschilds na Morgans wanaomba kupingana na wewe. Hawajawahi toa Rais wala nani serikalini, ila hawajawahi kosa good life wala agenda zao kutimizwa. Hebu niambie mamlaka aliyokuwa nayo Magufuli miaka mitatu iliyopita kamuachia nani kwenye cycle yake mwenye mamlaka yaleyale.

Mamlaka ni ya juu ila huisha, labda iwe dictatorship ndio ikae muda. Fortune haiishi kizembe hivyo. Hata ukienda Russia bado kuna oligarchies, Putin awe kinyume nao uone kama anabaki. Pesa na mamlaka vinategemeana sana.
 
Acha woga bro.....kama wananguvu ikifika kipindi kama hiki walete kiburi mtaani sasa waone.

Sasa hivi mtaani kila mwanasiasa anataka mchango na uungwaji mkono wetu wafanyabiashara.

Kama mamlaka ina nguvu kwanini wanakuja kuomba pesa zakuwasaidia wapate mamlaka?

You are a living example of the true meaning of the word "arrogant"
 
Back
Top Bottom