Faida yangu kibiashara kwa siku nane inaweza kumlipa Mkuu wa Wilaya mshahara; anapata wapi nguvu yakinifokea?

Hakuna mlipaji kodi mwaminifu nchi hii kama mtumishi wa umma, mchango wa mtumishi nchi hii ni mkubwa sana akifuatiwa na mkulima,

MTUMISHI,
1.Analipa kodi kila mwezi kupitia mshaara wake kwa mwezi
2. Analipa kodi kupitia manunuzi yake ya matumizi mbalimbali kila siku
3. Akifungua biashara analipa kodi na kuajiri pia
4.Akivuna shambani analipia pia ushuru na kuajiri vibarua wa kumfanyia kazi

Wafanyabiashara msijikute bila sababu , ukikuta mfanyabiashara analipa M1 kama makadilio ya kodi kwa mwaka ,jua nyuma ya pazia kaisha kwepa kodi M4
 
Manji wa Yanga aliishia wapi? Mo alifichwa siku kadhaa na hakutakiwa kuropoka na aliufya kinyaa Hadi Leo.

Wewe ni nani Hadi uitishe Mamlaka? Kiufupi unapangiwa namna ya kuishi bila kujalisha unataka au hutaki
Wamewahi kukosa nguvu ya kiuchumi? Manji alipoona maskini wanamwandama alihamisha mitaji yake kwenda nakojua.

Mo alipoona maskini wanamwandama aliamua kutokuendelea kushughulika nao na sasa yeye ni tajiri mkubwa Afrika. Jiulize wale waliomwandama MO kwa mamlaka zao enzi zile wapo wapi?

Umewahi kujiuliza wakina Musiba waliokuwa na fikra za kimaskini waliishia wapi?

Mtu anayetukuza umaskini aogopwe kama ukoma.

This is wake up call kwa watoto wetu wanaomaliza vyuo waache kutafuta madaraka waanze kutafuta fedha kwanza
 
Hakuna mwenye mamlaka anayempangia mwenye pesa namna ya kuishi ...akina bakharesa, mo, Rostam wameachana na Mamlaka zote wameamua kutafuta fedha

Sawasawa.
Nafikiri hujui maana ya Dola.
Ungejua maana yake wala usingeandika hayo.
Bakhressa ni mtu mdogo sana kwenye hii nchi mbele za Watawala.
Afisa TRA wa ngazi ya juu tuu anaweza kumjambisha achilia mbali wenye serikali
 
Wamewahi kukosa nguvu ya kiuchumi? Manji alipoona maskini wanamwandama alihamisha mitaji yake kwenda nakojua.

Mo alipoona maskini wanamwandama aliamua kutokuendelea kushughulika nao na sasa yeye ni tajiri mkubwa Afrika. Jiulize wale waliomwandama MO kwa mamlaka zao enzi zile wapo wapi?

Umewahi kujiuliza wakina Musiba waliokuwa na fikra za kimaskini waliishia wapi?

Mtu anayetukuza umaskini aogopwe kama ukoma.

This is wake up call kwa watoto wetu wanaomaliza vyuo waache kutafuta madaraka waanze kutafuta fedha kwanza
Huko nako akileta fyoto atashughulikiwa ipasavyo 🤣🤣🤣🤣

Hakuna wa kuitisha Mamlaka wewe nyumbu
 
Hakuna mlipaji kodi mwaminifu nchi hii kama mtumishi wa umma, mchango wa mtumishi nchi hii ni mkubwa sana akifuatiwa na mkulima,

MTUMISHI,
1.Analipa kodi kila mwezi kupitia mshaara wake kwa mwezi
2. Analipa kodi kupitia manunuzi yake ya matumizi mbalimbali kila siku
3. Akifungua biashara analipa kodi na kuajiri pia
4.Akivuna shambani analipia pia ushuru na kuajiri vibarua wa kumfanyia kazi

Wafanyabiashara msijikute bila sababu , ukikuta mfanyabiashara analipa M1 kama makadilio ya kodi kwa mwaka ,jua nyuma ya pazia kaisha kwepa kodi M4
Mtumishi analipa kodi kutoka wapi? Leo wafanyabiashara wasipolipa kodi serikali italipa mishahara? Watumishi hawalipi kodi kwa sababu hawafanyi biashara wakatengeneza faida......wanapunguziwa take home zao.
 
Sawasawa.
Nafikiri hujui maana ya Dola.
Ungejua maana yake wala usingeandika hayo.
Bakhressa ni mtu mdogo sana kwenye hii nchi mbele za Watawala.
Afisa TRA wa ngazi ya juu tuu anaweza kumjambisha achilia mbali wenye serikali
Anajitoa ufahamu tuu huyu nyumbu.

Angesoma walau sheria hata ya dharula au ya Uokoaji.Serikali ikiona Kuna haja ya kutwaa Mali yeyote ya mtu binafsi inafanya hivyo na hakuna wa Kuzuia utake au usitake.
 
Wamewahi kukosa nguvu ya kiuchumi? Manji alipoona maskini wanamwandama alihamisha mitaji yake kwenda nakojua.

Mo alipoona maskini wanamwandama aliamua kutokuendelea kushughulika nao na sasa yeye ni tajiri mkubwa Afrika. Jiulize wale waliomwandama MO kwa mamlaka zao enzi zile wapo wapi?

Umewahi kujiuliza wakina Musiba waliokuwa na fikra za kimaskini waliishia wapi?

Mtu anayetukuza umaskini aogopwe kama ukoma.

This is wake up call kwa watoto wetu wanaomaliza vyuo waache kutafuta madaraka waanze kutafuta fedha kwanza

Mkuu Watu humwabudu Mungu na shetani sio kwa sababu ya chochote zaidi ya Mamlaka.

Hao uliowataja kwa neno moja tuu la Mtawala unaweza kuwakuta sero na hakuamini wa kufanya chochote
 
Kuna pesa alafu kuna Mamlaka.
Mwenye mamlaka ndiye anaamua wewe uwe na pesa au uishi kifukara.

Pesa zako sio chochote mbele ya Mamlaka
hakuna kitu hicho wenye pesa ndio wenye mamlaka wenye pesa ndio wanaopambana kwenye uchaguzi watu wapate mamlaka mamlaka gani unazungumzia mkuu
 
Sawasawa.
Nafikiri hujui maana ya Dola.
Ungejua maana yake wala usingeandika hayo.
Bakhressa ni mtu mdogo sana kwenye hii nchi mbele za Watawala.
Afisa TRA wa ngazi ya juu tuu anaweza kumjambisha achilia mbali wenye serikali
Kama ni mdogo kaangalie ameajiri watu wangapi kutoka kiwandani hadi mtaani; then tuambie mkuu wa mkoa au waziri ameajiri watu wangapi?

Huwezi kumheshimu RC kabla ya Bakhressa ; nchi zote zilizopiga hatua zinathamini na kuheshimu mfanyabiashara kama mwajiri namba moja
 
Mtumishi analipa kodi kutoka wapi? Leo wafanyabiashara wasipolipa kodi serikali italipa mishahara? Watumishi hawalipi kodi kwa sababu hawafanyi biashara wakatengeneza faida......wanapunguziwa take home zao.
Uko sahihi
 
Anajitoa ufahamu tuu huyu nyumbu.

Angesoma walau sheria hata ya dharula au ya Uokoaji.Serikali ikiona Kuna haja ya kutwaa Mali yeyote ya mtu binafsi inafanya hivyo na hakuna wa Kuzuia utake au usitake.

Nafikiri hajui maana ya Dola.

Kama anamwona Bakhressa au hao matajiri ni Watu wakubwa, mwambie awashauri wajaribu kusapoti hata Chadema tuu achilia mbali ugaidi.
Alafu achukue popcorn atulie aone nini kitafuata
 
Mleta mada hajazingatia muktadha na mazingira, uzi wake una uhalisia kwa nchi za magharibi zaidi.
 
Nijuavyo hata huko Ulaya mtawala ni mtawala tuu.
Watawala wa Ulaya wametaka mfuko uwe hivyo unavyouona ndio maana upo hivyo.
Na sio vinginevyo.
 
hakuna kitu hicho wenye pesa ndio wenye mamlaka wenye pesa ndio wanaopambana kwenye uchaguzi watu wapate mamlaka mamlaka gani unazungumzia mkuu

Unaweza ukawa na pesa lakini usiwe na Mamlaka.
Tunajua viongozi kibao waliokuwa Maskini na wakawa watawala.

Ingawaje wenye pesa hupambana kupata Mamlaka ili kulinda utajiri wao.
Hiyo pekee inatosha kueleza kuwa Mamlaka ni zaidi ya Pesa.
 
Mtumishi analipa kodi kutoka wapi? Leo wafanyabiashara wasipolipa kodi serikali italipa mishahara? Watumishi hawalipi kodi kwa sababu hawafanyi biashara wakatengeneza faida......wanapunguziwa take home zao.
Aliekuelewa anisaidie ufafanuzi
 
Back
Top Bottom