Elimu ya kuendesha duka la "mangi" itolewe mashuleni

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,445
13,133
Bila shaka duka la mangi ndilo la pili kuajiri watanzaniw wengi baada ya kilimo. Karibu kila mtaa utakuta kuna maduka ya Mangi kuanzia mawili na kuendelea.

Umbali wa dakika tano toka hapo ulipo kuna maduka ya mangi mangapi? Watu wengi sana nchi hii wanaendesha maisha kwa kutegemea duka la mangi. Tena maduka mengi utakuta hayana muuzaji mmoja, mara mara nyingi utakuta wauzaji wawili.

Kama tunataka watu wakimaliza shule waweze kujiajiri, basi tuwape elimu kulingana na mazingira watakayoenda kuishi. Mojawapo ni elimu ya kuendesha duka la mangi.
 
Bila shaka duka la mangi ndilo la pili kuajiri watanzaniw wengi baada ya kilimo. Karibu kila mtaa utakuta kuna maduka ya Mangi kuanzia mawili na kuendelea...
Tafuta mke mmja tuh huyo huyo no mwngn akzngua mbatue had akae mkao saka mtaj fungua duka weka vzuiz kama unaloga loga nasubr mrejesho ukiweza shnda nae dukan uslete mazoea na wateja
 
Kwani kuna uhaba wa Maduka ? Yaani watu tunawaza kuwa na vitu kama Amazon na kutumia muda kufanya mambo mengine ya msingi (efficiency na sio effective pekee) wewe ndio unawaza kubaki au kurudi nyuma ili mradi tu watu wapate cha kufanya (Inabidi watu wasifanye kazi ili mradi wanafanya kazi, bali wafanye kazi sababu kazi hio ina tija katika jamii)

That said..., elimu ya kuhesabu, discipline na ku-balance pesa za hapa na pale inaweza ikawa applied kwenye duka au bar wakati unanunua bia na nyama ya mbuzi (hizo zote ni basics ambazo mtu anajifunza through his life na hata shuleni)
 
Maduka kama Amazon ni hatari sana kwa uchumi wa nchi na wa wananchi. Mom & pop bado ni muhimu sana.
 
Ulishawahi kujiuliza kwanini tunafanya kazi ? Kwamba sababu huenda jembe la mkono linasaidia wau wengi zaidi kufanya kazi tusitumie tractor au combined harvester ?

Huo muda wa Mom & Pop kuuza kitu ambacho Supermarket pia kipo (economy of scale) wangetumia muda huo labda kutengeneza home made (sababu kama wanatoa convinience, kina amazon do it better)...., The tide is coming Gen Z hawana muda wa shopping ni mwendo wa online...,. Ingawa huku hatujafika sawa lakini sio tuwekeze kwenye jambo ambalo kesho halina tija....; Ni sawasawa leo unamfundisha mtoto kutumia Four Figure Table au kujumlisha na kutoa kwa kutumia Roman Numerals....; unless unafanya kama hobbie
 
Mfano wa jembe la mkono na trekta hauingii hapa. Hapa unaoingia ni mtu mmoja kumiliki ekari elfu kumi peke yake au watu elfu moja kila mtu kuwa na ekari kumi? Tuipe kampuni moja mashamba yote ya nchi hii na sisi tukafanye kazi zingine ili uchumi usonge!!!? Uchumi wa kilafi wa mtu mmoja kumiliki yote unaanza kunyanyapaliwa. Hizo Amazon kwanza zinaua local economy ya eneo. Pesa inatoka kwenye community na hairudi tofauti na duka la mangi. Usifikiri eti ukiitoa workforce kwenye duka la mangi basi lazima itaenda kufanya jambo fulani la maana sana. Asilimia kubwa itaangukia ujobless.

Kila mtu kupata share ya kazi ni muhimu kuliko kumpa kazi zote mtu mmoja na akaishia kujitajirisha kupita kiasi.

Mwisho. Elimu ya duka la mangi inahitajika hata kwa mtu anayeuza vitu online.
 
Tatizo maji yakikatika umeme nao huo unawaka sijui hata kama kazi nzur au mby naona tu sielew
 
Mfano wa jembe la mkono na trekta hauingii hapa. Hapa unaoingia ni mtu mmoja kumiliki ekari elfu kumi peke yake au watu elfu moja kila mtu kuwa na ekari kumi?
Kwamba lazima Amazon iwe ya Mtu mmoja ? Unajua Cooperative Shops ? Unajua kina Costoc je kina Crédit Agricole, unajua mababu zako wengi walisomeshwa na kupewa sponsorship kutokana na cooperatives ? Kama kuna machinery cooperative moja inaweza kulima na kulisha nchi nzima, kwanini watu tuhangaike na inefficiencies ? kama kilimo ni hoby lima uwani kwako lakini kama kuna mdau anaweza kufanya cheaply and efficient why not ?
Tuipe kampuni moja mashamba yote ya nchi hii na sisi tukafanye kazi zingine ili uchumi usonge!!!? Uchumi wa kilafi wa mtu mmoja kumiliki yote unaanza kunyanyapaliwa.
Again nani kasema apewe mtu mmoja ? Ulafi / ubinafsi ndio huo kila mtu afanye cha kwake wakati watu wanaweza kujumuisha nguvu na kutoa kitu ambacho ni bora zaidi..., waliosema Umoja ni Nguvu hawakuwa machizi
Hizo Amazon kwanza zinaua local economy ya eneo. Pesa inatoka kwenye community na hairudi tofauti na duka la mangi. Usifikiri eti ukiitoa workforce kwenye duka la mangi basi lazima itaenda kufanya jambo fulani la maana sana. Asilimia kubwa itaangukia ujobless.
Again nimekwambia Amazon nikimaanisha mfumo, nigeweza kusema Argos, Kijiji au kitu chochote kile..., moja inaongeza ufanisi (delivery) mbili generation Z; sio kama generation za zamani watu kwenda kushangaa madukani au kufanya shopping wana-prefer kuagiza; Pia duka la Mangi sio Brain child ya Tanzania hizi ndio zinaitwa corner shops au convinience stores (yaani mtu anataka kitu anachukua haraka haraka, kwa wenzetu hii ni gharama zaidi kuliko kwenda supermarket) sasa ukiondoa na hio convinience sababu hata big players kina AZAM watakapoanza kuleta mpaka bafuni, nadhani kitakachotokea haiitiji degree kutambua ni kipi....
Kila mtu kupata share ya kazi ni muhimu kuliko kumpa kazi zote mtu mmoja na akaishia kujitajirisha kupita kiasi.

Mwisho. Elimu ya duka la mangi inahitajika hata kwa mtu anayeuza vitu online.
Ndio maana nimekuuliza kwanini tunafanya kazi ? Ukishajua hilo nyote hamuhitaji kushika jembe bali tractor linaweza kufanya kazi na nyie mkagawana ujira ndio hizo mali za UMMA kama TANESCO sio wote tunasambaza Nishati ila wote tunanufaika....; by the way kuhusu elimu basic ya kutumika popote si nimesema mwanzo kabisa..., kwamba basic counting and keeping money na vitu kama hivyo hata kwa elimu ya sasa vinafundishwa ukitaka kwenda deep chukua book-keeping na commerce...
 
Kwamba lazima Amazon iwe ya Mtu mmoja ? Unajua Cooperative Shops ? Unajua kina Costoc je kina Crédit Agricole, unajua mababu zako wengi walisomeshwa na kupewa sponsorship kutokana na cooperatives ? Kama kuna machinery cooperative moja inaweza kulima na kulisha nchi nzima, kwanini watu tuhangaike na inefficiencies ? kama kilimo ni hoby lima uwani kwako lakini kama kuna mdau anaweza kufanya cheaply and efficient why not ?
Unaongelea cooperatives yaani ushirika? Hilo liliishafeli. Cooporations kama Amazon siyo ushirika.
Again nani kasema apewe mtu mmoja ? Ulafi / ubinafsi ndio huo kila mtu afanye cha kwake wakati watu wanaweza kujumuisha nguvu na kutoa kitu ambacho ni bora zaidi..., waliosema Umoja ni Nguvu hawakuwa machizi
Kama tunatafuta Efficiency kwa nini tusiwape watu 100? Kama tunatafuta efficiency zaidi kwa nini tusimpe mtu mmoja? Unachanganyachanganya logic.
Again nimekwambia Amazon nikimaanisha mfumo, nigeweza kusema Argos, Kijiji au kitu chochote kile..., moja inaongeza ufanisi (delivery) mbili generation Z; sio kama generation za zamani watu kwenda kushangaa madukani au kufanya shopping wana-prefer kuagiza;
Mazingira yanayofanya wenzetu malls ziflourish ndiyo yanafanya online business/ na delivery ziflourish. Hapa kwetu hayapo.
Pia duka la Mangi sio Brain child ya Tanzania hizi ndio zinaitwa corner shops au convinience stores (yaani mtu anataka kitu anachukua haraka haraka, kwa wenzetu hii ni gharama zaidi kuliko kwenda supermarket) sasa ukiondoa na hio convinience sababu hata big players kina AZAM watakapoanza kuleta mpaka bafuni, nadhani kitakachotokea haiitiji degree kutambua ni kipi....
Duka la mangi ni biashara ya kale sana duniani. Haiwezi kusemwa ilianzishwa na watu fulani. Toka enzi za kabla ya Yesu yapo. Na kwa nchi yetu ambayo hakuna habari ya zoning zinazokataza biashara kwenye makazi, duka la mangi litaendelea kuwepo na kuwa muajiri mkubwa.
Ndio maana nimekuuliza kwanini tunafanya kazi ? Ukishajua hilo nyote hamuhitaji kushika jembe bali tractor linaweza kufanya kazi na nyie mkagawana ujira
Unataka turudi kwenye ujamaa!!?
ndio hizo mali za UMMA kama TANESCO sio wote tunasambaza Nishati ila wote tunanufaika....;

by the way kuhusu elimu basic ya kutumika popote si nimesema mwanzo kabisa..., kwamba basic counting and keeping money na vitu kama hivyo hata kwa elimu ya sasa vinafundishwa ukitaka kwenda deep chukua book-keeping na commerce...
Kusoma bookkeeping na kusoma uhalisia wa kuendesha duka la mangi ni vitu viwili tofauti. Waendeshaji wengi hawajapitia bookkeeping.
 
Unaongelea cooperatives yaani ushirika? Hilo liliishafeli. Cooporations kama Amazon siyo ushirika.
Naanza kupata shaka kama unanielewa wako mkuu..., rudia kusoma kuanzia mwanzo nimeongelea nini ili niepuke kujirudia..., Kwanini nimeongelea Amazon (sababu tunakoelekea generation ya sasa ni tofauti na wao kununua Insta na Facebook ndio mpango mzima, ingawa utapeli unafanya movement iwe ngumu) convinience ni muhimu, mtu anakwenda kwenye duka la Mangi kupata mahitaji, na kama hayo mahitaji anaweza kuyapata kwake kwa bei nafuu kuliko Mangi atafanya hivyo...., Nilivyoongelea Amazon (ambayo ni business model) ukasema inapunguza uchumi kwa watu wachache kufaya kitu nikakwambia unajua cooperatives..., chama chochote cha ushirika kinaweza kikatumia business model ya Amazon..., kuna maduka makubwa na corporations world wide ambazo ni Ushirika..., if am not mistaken hata Tanga Fresh Maziwa ilikuwa ni ushirika..., Kwahio ku-fail au kushamiri kwa Amazon sio sababu ya kutokuwa ushirika au la ni business model yake na how the business is run...., kuwa na maduka yameongozana kila mlango yanauza kilekile sio efficiency ni kama uchafu..., zamani duka moja labda mtaa hata mwenye duka anapata cha kueleweka sasa hivi kila ukipiga tambo ni duka (kugawana umasikini) bora muda huo watu wangetumia hata kutunga singeli watu waburudike....

Na ili kuepuka kujirudia huko mbele naomba uelewe kwamba ninapoongelea AMAZON ni kile anachofanya sio necessarily Business Model nzima (Mtu kupata kitu Conveniently) Ninapoongelea Cooperatives naongelea Umiliki (Ownership) Hence badala ya Amazon kuwa owned na Bezos na jamaa wachache ingeweza kuwa owned na Cooperation ya Singasinga wote huko Saskatchewan au Gamboshi....
Kama tunatafuta Efficiency kwa nini tusiwape watu 100? Kama tunatafuta efficiency zaidi kwa nini tusimpe mtu mmoja? Unachanganyachanganya logic.
Tusiwape wewe ni nani unawapa ? Binadamu haifai apangiwe anafanya anachofanya na kwenye biashara ambayo ni ushindani akija mtu mwenye better business model wewe unakufa kifo cha kawaida...., Amazon alianza kwa kuuza vitabu ambavyo yeye sio publisher wala hana publishing company wala duka..., ukinunua anaenda madukani anachukua na kukuletea matokeo yake alipata soko kwa overheads ndogo mpaka publishing companies zikamgongea mlango sababu alichukua soko lao na yeye ni efficient kuliko wao.., kwahio maisha haupewi bali unakuwa squeezed nje ya market na kuwa obsolete IBM alikuwa ndio Baba wa Computer (Mainframes) hakutaka kuingia kwenye PC (Personal Computers) akiona kwamba yeye soko lake ni maintance kuja kushituka ni too late ikabidi atengeneza haraka haraka na kujiunga na kina Gates kwa kutumia OS yao ama sivyo angepotea kwenye ramani....

Kwahio kwa kukurahisishia ni kwamba maisha yanabadilika na yakibadilika inabidi ku-adapt na hapa issue ni mgawanyiko wa faida.., sasa kama issue ni mgawanyiko inabidi cooperative ichukue modal which works sababu zisipofanya hivyo wachache au mmoja atafanya kwa faida yake na itabidi watu waanze kulia Monopoly na kumzuia mtu (sababu anachofanya ni bora kwanini kisifanyike kwa manufaa ya wengi after all hapo which matters ni ownership) hata hii Voda ingeweza kuwa owned na wakazi wote wa Temeke kwa kupewa (shares) lakini wafanyakazi na management bado ikabakia ambavyo ilivyo sasa....
Mazingira yanayofanya wenzetu malls ziflourish ndiyo yanafanya online business/ na delivery ziflourish. Hapa kwetu hayapo.
Tofauti ya malls na soko la Kariakoo au genge au mnadani au gulio ni nini zaidi ya miundombinu ? Kwa taarifa yako hizo malls ndio minada ya huku..., ni kwamba tu kuna mpangilio..., online business huku ni ngumu ku-take another step sababu ya utapeli na uongo uongo..., leo Mangi akisema ukitaka kitu nakuletea kwako utakataa.., unacho-suggest badala ya kuwa na Duka la Mangi kila duka la tatu kila nyumba iwe na Duka la Mangi..., sasa mimi nakwambia kwa kuwaza future ni kuwa na more efficient ways na mipangilio.....

Umesema haya mambo kwetu hayapo kwahio tuwekeze yawepo sio kuwekeza kuendelea kuwa na mediocrity....
Duka la mangi ni biashara ya kale sana duniani. Haiwezi kusemwa ilianzishwa na watu fulani. Toka enzi za kabla ya Yesu yapo. Na kwa nchi yetu ambayo hakuna habari ya zoning zinazokataza biashara kwenye makazi, duka la mangi litaendelea kuwepo na kuwa muajiri mkubwa.
Ndio hapo nasema najikuta ninajirudiarudia nimekwambia haya maduka hata nje yapo yaani corner shops au convenient shops..., sababu kwa wenzetu kuliko kwenda malls ambapo huenda ni cheaper unachukua kitu karibu yako kwa rejareja hence inakusaidia kwenye muda lakini kwa giants kutaka biashara zaidi wameanza hadi kureach kwenye nyumba za watu kwa delivery (ndio hapo ukasema inaharibu uchumi local) mimi nakwambia hio ndio future na sio lazima Mangi aendelee kuwa Mangi kama biashara yake ikifa kwa kupata kitu bora maybe bore aanze kuuza mbege au kutumia muda wake kwa kitu ambacho atafanya more efficiently..., Mangi hakatazwi kuwepo ila wewe unataka hii shughuli hadi tuweke kwenye mitaala kwamba tuendelee kuwepo hapa ambapo maybe badala ya kuwepo hapa tungeinvest kwenye kutoka hapa na kwenda pale sababu teknolojia ipo.....

Unataka turudi kwenye ujamaa!!?
Ujamaa ni nini ? Au unaongelea duka la Kaya ? Nadhani wewe ndio unataka tubaki kwenye maduka ya Kaya kwamba Mangi lazima awepo ili apate Pesa mimi nakwambia Mangi awepo ila kama Azam anaweza kufanya kazi kwa gharama ndogo na bei ndogo basi aje hata kama kina Mangi wakifa kifo cha kawaida so be it.... (sio lazima owner awe Azam wanaweza kuwa Mangi wote wa Kibosho)
Kusoma bookkeeping na kusoma uhalisia wa kuendesha duka la mangi ni vitu viwili tofauti. Waendeshaji wengi hawajapitia bookkeeping.
Ndio hapo unakosea tena..., Ujasiriamali haufudishwi shule pekee its way of life..., wahindi tangia mtoto anazaliwa anakaa dukani na mama yake huku mama yake anauza (anfanya practicals since day one) huenda mimi ninajua theory zaidi kuliko Mangi na nikizi-apply huenda nikafanikiwa kuliko Mangi ila sina discipline ya pesa wala muda na uvumilivu wa kukaa dukani masaa na masaa wala customer care...., hayo hayafundishwi kwenye makabrasha ni maisha ya mtu anayoyaishi kila siku hence kuboresha (na huenda kuboresha huko ni kuongeza reach na kuwa kama kina Amazon na sio kubakia nyuma sababu wakati utakupita)

Au kama vipi basi shule wapeani zamu ya kila mwanafunzi kuuza maandazi na pipi za mwalimu mkuu kwa mwaka kila watu 100 kwa mwezi mmojamoja..., hio itakuwa more practically ingawa huenda tukapelekea watoto kuiba chenji za kutoa sadaka kanisani sababu mwalimu kanuna fulani hanunui maandazi yangu....
 
Naanza kupata shaka kama unanielewa wako mkuu..., rudia kusoma kuanzia mwanzo nimeongelea nini ili niepuke kujirudia..., Kwanini nimeongelea Amazon (sababu tunakoelekea generation ya sasa ni tofauti na wao kununua Insta na Facebook ndio mpango mzima, ingawa utapeli unafanya movement iwe ngumu) convinience ni muhimu, mtu anakwenda kwenye duka la Mangi kupata mahitaji, na kama hayo mahitaji anaweza kuyapata kwake kwa bei nafuu kuliko Mangi
Hata sasa, vitu vinavyouzwa dukani kwa mangi haviuzwi mitandaoni. Au haufahamu duka la mangi ni kitu gani? Na mazingira yetu na nchi kama US ni tofauti. Tz ukikatisha kona ya pili unakutana na duka la mangi. Ni rahisi kwenda kununua duka la mangi kuliko mtandaoni. Nchi kama US maduka na migahawa huwa mbali na makazi. Ili kwenda ni mpaka upande gari, ndiyo maana delivery services na biashara za mtandaoni zinashamiri. Siyo tu kusema Gen z Gen Z. Mazingira yana matter.
atafanya hivyo...., Nilivyoongelea Amazon (ambayo ni business model) ukasema inapunguza uchumi kwa watu wachache kufaya kitu nikakwambia unajua cooperatives..., chama chochote cha ushirika kinaweza kikatumia business model ya Amazon..., kuna maduka makubwa na corporations world wide ambazo ni Ushirika..., if am not mistaken hata Tanga Fresh Maziwa ilikuwa ni ushirika..., Kwahio ku-fail au kushamiri kwa Amazon sio sababu ya kutokuwa ushirika au la ni business model yake na how the business is run...., kuwa na maduka yameongozana kila mlango yanauza kilekile sio efficiency ni kama uchafu..., zamani duka moja labda mtaa hata mwenye duka anapata cha kueleweka sasa hivi kila ukipiga tambo ni duka (kugawana umasikini) bora muda huo watu wangetumia hata kutunga singeli watu waburudike....

Ushirika haumaanishi kutakuwa na maduka machache. Maduka yatakuwa yale yale. Tofautisha cooperatives na Coorporations. Cooperative(ushirika) ni kama wote wenye maduka ya mangi waunde umoja wao. Cooporation ni kama kampuni moja iwe inamiliki maduka yote ya mangi. Hayo maduka ya mangi yanaendesha maisha ya watu ambao vinginevyo wasingeweza au wangepata tabu kuendesha maisha. Wengi wana kipato kuliko waajiriwa rasmi. Basi na watu waache kuajiriwa maana ni umasikini tu.
Na ili kuepuka kujirudia huko mbele naomba uelewe kwamba ninapoongelea AMAZON ni kile anachofanya sio necessarily Business Model nzima (Mtu kupata kitu Conveniently) Ninapoongelea Cooperatives naongelea Umiliki (Ownership) Hence badala ya Amazon kuwa owned na Bezos na jamaa wachache ingeweza kuwa owned na Cooperation ya Singasinga wote huko Saskatchewan au Gamboshi....
Tena, cooperative haitapunguza idadi ya maduka ya mangi. Zaidi itatengeneza cartel ya kupanga bei na kumuumiza mlaji. Cooperative ya wauza maziwa wa Tanga haijapunguza idadi ya wazalisha maziwa. Amazon and the like siyo cooperative.
Tusiwape wewe ni nani unawapa ? Binadamu haifai apangiwe anafanya anachofanya na kwenye biashara ambayo ni ushindani akija mtu mwenye better business model wewe unakufa kifo cha kawaida...., Amazon alianza kwa kuuza vitabu ambavyo yeye sio publisher wala hana publishing company wala duka..., ukinunua anaenda madukani anachukua na kukuletea matokeo yake alipata soko kwa overheads ndogo mpaka publishing companies zikamgongea mlango sababu alichukua soko lao na yeye ni efficient kuliko wao.., kwahio maisha haupewi bali unakuwa squeezed nje ya market na kuwa obsolete IBM alikuwa ndio Baba wa Computer (Mainframes) hakutaka kuingia kwenye PC (Personal Computers) akiona kwamba yeye soko lake ni maintance kuja kushituka ni too late ikabidi atengeneza haraka haraka na kujiunga na kina Gates kwa kutumia OS yao ama sivyo angepotea kwenye ramani....
Biashara huria siyo huria kama unavyodhani. Ndiyo maana kuna antimonopoly laws. Lakini chain stores zinaweza kuja kama zinaweza kupambana na duka la mangi. Duka la mangi litaendelea kuwepo nchi hii. Ndiyo maana nimependekeza elimu itolewe katika kuyaendesha.
Kwahio kwa kukurahisishia ni kwamba maisha yanabadilika na yakibadilika inabidi ku-adapt na hapa issue ni mgawanyiko wa faida.., sasa kama issue ni mgawanyiko inabidi cooperative ichukue modal which works sababu zisipofanya hivyo wachache au mmoja atafanya kwa faida yake na itabidi watu waanze kulia Monopoly na kumzuia mtu (sababu anachofanya ni bora kwanini kisifanyike kwa manufaa ya wengi after all hapo which matters ni ownership) hata hii Voda ingeweza kuwa owned na wakazi wote wa Temeke kwa kupewa (shares) lakini wafanyakazi na management bado ikabakia ambavyo ilivyo sasa....

Tofauti ya malls na soko la Kariakoo au genge au mnadani au gulio ni nini zaidi ya miundombinu ? Kwa taarifa yako hizo malls ndio minada ya huku..., ni kwamba tu kuna mpangilio..., online business huku ni ngumu ku-take another step sababu ya utapeli na uongo uongo..., leo Mangi akisema ukitaka kitu nakuletea kwako utakataa.., unacho-suggest badala ya kuwa na Duka la Mangi kila duka la tatu kila nyumba iwe na Duka la Mangi..., sasa mimi nakwambia kwa kuwaza future ni kuwa na more efficient ways na mipangilio.....
Kuwa na duka la mangi ni more efficient kwa mteja kuliko kununua mtandaoni. We ukitembea kama mita 100 unakuta duka lenye mahitaji yako yote ya kila siku. Ukitembea kidogo unakuta genge, bucha nk. Kwa nini uagize mtandaoni na kusubiri kuletewa au upande gari kwenda malls? Kwa efficiency duka la mangi linazishinda biashara za mtandaoni. So kwa nchi yetu bado duka la mangi ndiyo future.
Umesema haya mambo kwetu hayapo kwahio tuwekeze yawepo sio kuwekeza kuendelea kuwa na mediocrity....
Uwekeze kwenye kitu inefficient? Usione kitu kwa sababu kipo Ulaya au USA ukadhani kitafit kote.
Ndio hapo nasema najikuta ninajirudiarudia nimekwambia haya maduka hata nje yapo yaani corner shops au convenient shops..., sababu kwa wenzetu kuliko kwenda malls ambapo huenda ni cheaper unachukua kitu karibu yako kwa rejareja hence inakusaidia kwenye muda lakini kwa giants kutaka biashara zaidi wameanza hadi kureach kwenye nyumba za watu kwa delivery (ndio hapo ukasema inaharibu uchumi local) mimi nakwambia hio ndio future na sio lazima Mangi aendelee kuwa Mangi kama biashara yake ikifa kwa kupata kitu bora maybe bore aanze kuuza mbege au kutumia muda wake kwa kitu ambacho atafanya more efficiently..., Mangi hakatazwi kuwepo ila wewe unataka hii shughuli hadi tuweke kwenye mitaala kwamba tuendelee kuwepo hapa ambapo maybe badala ya kuwepo hapa tungeinvest kwenye kutoka hapa na kwenda pale sababu teknolojia ipo.....
Huko nje, sehemu kubwa ya sheria zao za zoning hairuhusu maduka kwenye makazi. Ndiyo maana zikajengwa malls na online business zikakua. Hayo maeneo yenye convenients stores ni ya mijini hasa. Huko suburbans watu wanalazimika kwenda malls au wanarahisisha kwa kununua mitandaoni.
Ujamaa ni nini ? Au unaongelea duka la Kaya ? Nadhani wewe ndio unataka tubaki kwenye maduka ya Kaya kwamba Mangi lazima awepo ili apate Pesa mimi nakwambia Mangi awepo ila kama Azam anaweza kufanya kazi kwa gharama ndogo na bei ndogo basi aje hata kama kina Mangi wakifa kifo cha kawaida so be it.... (sio lazima owner awe Azam wanaweza kuwa Mangi wote wa Kibosho)
Hakuna aliyesema mangi lazima awepo. Mazingira yetu yanamfanya mangi aendelee kuwepo siku ntingi mbeleni.
Ndio hapo unakosea tena..., Ujasiriamali haufudishwi shule pekee its way of life..., wahindi tangia mtoto anazaliwa anakaa dukani na mama yake huku mama yake anauza (anfanya practicals since day one) huenda mimi ninajua theory zaidi kuliko Mangi na nikizi-apply huenda nikafanikiwa kuliko Mangi ila sina discipline ya pesa wala muda na uvumilivu wa kukaa dukani masaa na masaa wala customer care...., hayo hayafundishwi kwenye makabrasha ni maisha ya mtu anayoyaishi kila siku hence kuboresha (na huenda kuboresha huko ni kuongeza reach na kuwa kama kina Amazon na sio kubakia nyuma sababu wakati utakupita)
Haya mambo unaweza kufundishwa vizuri tu. Ubahili, uvumilivu na kutunza pesa vinafundishika vizuri tu.
Au kama vipi basi shule wapeani zamu ya kila mwanafunzi kuuza maandazi na pipi za mwalimu mkuu kwa mwaka kila watu 100 kwa mwezi mmojamoja..., hio itakuwa more practically ingawa huenda tukapelekea watoto kuiba chenji za kutoa sadaka kanisani sababu mwalimu kanuna fulani hanunui maandazi yangu....
Practical ni nzuri zaidi ila Wanafunzi wanaweza kufundishwa theory ya jinsi duka la mangi linavyoendeshwa na ikawa na msaada mkubwa kwao siku wakitaka kujiajiri kwenye sekta hiyo. Habari za leseni, bidhaa zinavyojumuliwa, kusafirisha bidhaa, shelf life, bidhaa zinavyotakiwa, namna ya kupiga hesabu faida, kutunza pesa, mikopo, kodi nk nk.
 
Hata sasa, vitu vinavyouzwa dukani kwa mangi haviuzwi mitandaoni. Au haufahamu duka la mangi ni kitu gani? Na mazingira yetu na nchi kama US ni tofauti. Tz ukikatisha kona ya pili unakutana na duka la mangi. Ni rahisi kwenda kununua duka la mangi kuliko mtandaoni. Nchi kama US maduka na migahawa huwa mbali na makazi. Ili kwenda ni mpaka upande gari, ndiyo maana delivery services na biashara za mtandaoni zinashamiri. Siyo tu kusema Gen z Gen Z. Mazingira yana matter.
Again nachofanya nadhani ni kujirudia kama santuri mbovu..... kwahio unachosema anacho-offer mangi ni nini zaidi ya convenience ? Na huu mpangilio wa duka kila nyumba ya barabarani unaona ndio maendeleo ? kwamba miaka yote ilikuwa hivyo au maduka yalikuwa kila mtaa wa pili au wa tatu...., na hayo maduka kutokana na utitiri unadhani yakikatwa kodi ipasavyo hata return on investment itapatikana..., Kwa sasa ni rahisi kununua kwa Mangi kuliko online sababu ya utapeli na watu sio technical savvy sasa badala ya kubadilisha watu wawe technical savvy na kupunguza overheads za salesman na kuokoa muda wewe unasema tuendelee kufundisha ili tuendelee kuwa na utitiri wa convenient shops bila convenience..., hivi unajua supermarkets zina economy of scale na zingemwangwa kila kaya huenda bei ya vitu kwa mlaji wa mwisho ingeshuka hence kuokoa pesa za kila mwana kaya ?
Ushirika haumaanishi kutakuwa na maduka machache. Maduka yatakuwa yale yale. Tofautisha cooperatives na Coorporations. Cooperative(ushirika) ni kama wote wenye maduka ya mangi waunde umoja wao. Cooporation ni kama kampuni moja iwe inamiliki maduka yote ya mangi. Hayo maduka ya mangi yanaendesha maisha ya watu ambao vinginevyo wasingeweza au wangepata tabu kuendesha maisha. Wengi wana kipato kuliko waajiriwa rasmi. Basi na watu waache kuajiriwa maana ni umasikini tu.
Hivi unajua cooperative ni form ya corporation ? Ingawa huku wauzaji ndio wanaweza kuwa wamiliki lakini pia maduka yanaweza yakawa na wafanyakazi ila yanakuwa owned na a corporation ambayo ina shareholders ambao ni wananchi wa kawaida au kila kaya husika katika mtaa husika ?...., Ni kwamba hao ambao hawana kipato unawaita masikini bado wanaweza waka-own kitu kama Amazon ambacho ambacho kina distribution centre kila kaya na bado wakapata faida...., Hapa issue ya ownership can be formed in any way Ingawa mimi sijikiti huko per se nakwambia Mangi ni convenient, lakini kuwepo na utitiri wa kina mangi sio convenience tena bali ni kupoteza muda na kugawana umasikini...
Tena, cooperative haitapunguza idadi ya maduka ya mangi. Zaidi itatengeneza cartel ya kupanga bei na kumuumiza mlaji. Cooperative ya wauza maziwa wa Tanga haijapunguza idadi ya wazalisha maziwa. Amazon and the like siyo cooperative.
Any cooperative (workers ndio owners) inaweza ikatumia mfumo kama wa Amazon..., Nimeanza kuongelea mambo ya cooperative kuunganisha nguvu baada ya wewe kusema kina Amazon watachukua vipato vya watu..., Clans can not defeat empires you need to unite ili uweze ku-compete na bigger giants hivi unadhani zikija big massive supermarkets kuna hazi duka za kuunga unga zitakazo-survive ?
Biashara huria siyo huria kama unavyodhani. Ndiyo maana kuna antimonopoly laws. Lakini chain stores zinaweza kuja kama zinaweza kupambana na duka la mangi. Duka la mangi litaendelea kuwepo nchi hii. Ndiyo maana nimependekeza elimu itolewe katika kuyaendesha.
Naendelea kujirudia ni nini faida ya chain stores zinaleta convinience ipi ? na kwanini sehemu nyingi duniani chain stores nyingi za makampuni makubwa zilifungwa what happened ?
Kuwa na duka la mangi ni more efficient kwa mteja kuliko kununua mtandaoni. We ukitembea kama mita 100 unakuta duka lenye mahitaji yako yote ya kila siku. Ukitembea kidogo unakuta genge, bucha nk. Kwa nini uagize mtandaoni na kusubiri kuletewa au upande gari kwenda malls? Kwa efficiency duka la mangi linazishinda biashara za mtandaoni. So kwa nchi yetu bado duka la mangi ndiyo future.
Tofauti ya Mangi na Supermarkets kwa Bongo ni ipi Kwa Bei n.k. Bongo Supermarkets kwenda ni ufahari na kipato kikubwa wakati kutokana na economy of scale inabidi wao ndio bei iwe ndogo..., sasa kipato cha watu kidogo ndio maana wanakwenda kununua sukari hata nusu kijiko au kukopa kwa Mangi au mafuta ya kibaba (kuendeleza umasikini) lakini giants wenye stock kubwa Mangi hawezi kushindana nao...., nilisikia hivi karibudi AZAM ana kitu kinaitwa Sarafu nina uhakika huko ndio anataka kwenda kuweza kuleta mahitaji zaidi karibu kwa mlaji... , Hicho unachosema kila kona kuna bucha na genge ni mipango miji ya hovyo wala sio kitu cha kuplan kiwepo in future generations
Uwekeze kwenye kitu inefficient? Usione kitu kwa sababu kipo Ulaya au USA ukadhani kitafit kote.

Huko nje, sehemu kubwa ya sheria zao za zoning hairuhusu maduka kwenye makazi. Ndiyo maana zikajengwa malls na online business zikakua. Hayo maeneo yenye convenients stores ni ya mijini hasa. Huko suburbans watu wanalazimika kwenda malls au wanarahisisha kwa kununua mitandaoni.
Aliyekwambia maduka yalipigwa marufuku pote ni nani au yalikufa kifo cha kawaida kwa kushindwa kupata soko na bidhaa..., wewe unauza machungwa yako kwenge genge alafu kesho inashushwa supermarket yenye bei sawa na bure unadhani uta-survive ?
Hakuna aliyesema mangi lazima awepo. Mazingira yetu yanamfanya mangi aendelee kuwepo siku ntingi mbeleni.

Haya mambo unaweza kufundishwa vizuri tu. Ubahili, uvumilivu na kutunza pesa vinafundishika vizuri tu.
Unafundisha ubahili shule ? Uvumilivu ? na kutunza Pesa kwanini usianze wewe kama mzazi kumfundisha mwanao ?
Practical ni nzuri zaidi ila Wanafunzi wanaweza kufundishwa theory ya jinsi duka la mangi linavyoendeshwa na ikawa na msaada mkubwa kwao siku wakitaka kujiajiri kwenye sekta hiyo. Habari za leseni, bidhaa zinavyojumuliwa, kusafirisha bidhaa, shelf life, bidhaa zinavyotakiwa, namna ya kupiga hesabu faida, kutunza pesa, mikopo, kodi nk nk.
Na aliyosema hayo hayafundishwi sasa ni nani katika nyanja tofauti tofauti ? Mtu akifundishwa business general duka la mangi, genge la nyanya au hata kuuza makahaba sio subset ya biashara ?!!!
 
Again nachofanya nadhani ni kujirudia kama santuri mbovu..... kwahio unachosema anacho-offer mangi ni nini zaidi ya convenience ? Na huu mpangilio wa duka kila nyumba ya barabarani unaona ndio maendeleo ? kwamba miaka yote ilikuwa hivyo au maduka yalikuwa kila mtaa wa pili au wa tatu...., na hayo maduka kutokana na utitiri unadhani yakikatwa kodi ipasavyo hata return on investment itapatikana..., Kwa sasa ni rahisi kununua kwa Mangi kuliko online sababu ya utapeli na watu sio technical savvy sasa badala ya kubadilisha watu wawe technical savvy na kupunguza overheads za salesman na kuokoa muda wewe unasema tuendelee kufundisha ili tuendelee kuwa na utitiri wa convenient shops bila convenience..., hivi unajua supermarkets zina economy of scale na zingemwangwa kila kaya huenda bei ya vitu kwa mlaji wa mwisho ingeshuka hence kuokoa pesa za kila mwana kaya ?
Kila nyumba kuwa na duka ni jambo zuri. yatakayoshindwa yatafunga. Ni jambo zuri kwa wakazi wa eneo husika na uchumi wa eneo lao. Kwanza sababu kubwa si utapeli, sababu kubwa ni kuwa ni rahisi kununua vitu dukani kwa mangi kuliko online. Kwenye miji mikubwa, ndani mwendo wa dk 5 kutoka makazi ya kila mtu utakutana na duka kubwa la mangi. Niagize kitu online na kwa "mangi" ni hapo nje? Kuna somo refu la ubaya wa hizo supermarkets na madhara yatokanayo na kuweka bei chini kuliko uhalisia, ni somo refu.
Hivi unajua cooperative ni form ya corporation ? Ingawa huku wauzaji ndio wanaweza kuwa wamiliki lakini pia maduka yanaweza yakawa na wafanyakazi ila yanakuwa owned na a corporation ambayo ina shareholders ambao ni wananchi wa kawaida au kila kaya husika katika mtaa husika ?...., Ni kwamba hao ambao hawana kipato unawaita masikini bado wanaweza waka-own kitu kama Amazon ambacho ambacho kina distribution centre kila kaya na bado wakapata faida...., Hapa issue ya ownership can be formed in any way Ingawa mimi sijikiti huko per se nakwambia Mangi ni convenient, lakini kuwepo na utitiri wa kina mangi sio convenience tena bali ni kupoteza muda na kugawana umasikini...

Any cooperative (workers ndio owners) inaweza ikatumia mfumo kama wa Amazon..., Nimeanza kuongelea mambo ya cooperative kuunganisha nguvu baada ya wewe kusema kina Amazon watachukua vipato vya watu..., Clans can not defeat empires you need to unite ili uweze ku-compete na bigger giants hivi unadhani zikija big massive supermarkets kuna hazi duka za kuunga unga zitakazo-survive ?

Naendelea kujirudia ni nini faida ya chain stores zinaleta convinience ipi ? na kwanini sehemu nyingi duniani chain stores nyingi za makampuni makubwa zilifungwa what happened ?

Tofauti ya Mangi na Supermarkets kwa Bongo ni ipi Kwa Bei n.k. Bongo Supermarkets kwenda ni ufahari na kipato kikubwa wakati kutokana na economy of scale inabidi wao ndio bei iwe ndogo..., sasa kipato cha watu kidogo ndio maana wanakwenda kununua sukari hata nusu kijiko au kukopa kwa Mangi au mafuta ya kibaba (kuendeleza umasikini) lakini giants wenye stock kubwa Mangi hawezi kushindana nao...., nilisikia hivi karibudi AZAM ana kitu kinaitwa Sarafu nina uhakika huko ndio anataka kwenda kuweza kuleta mahitaji zaidi karibu kwa mlaji... , Hicho unachosema kila kona kuna bucha na genge ni mipango miji ya hovyo wala sio kitu cha kuplan kiwepo in future generations
Uwepo wa bucha na magenge kila sehemu ni jambo zuri na mipango mizuri ya miji. Mahitaji ya kila siku ya watu yanatakiwa kupatikani umbali wa kutembea. Usidhani kuendesha gari kwenda "madukani" ndiyo mipango mizuri. watu wanataka kutoka huko. Hivyo future ni duka la mangi. Pia hii inafaida sana kwa uchumi wa community.
Aliyekwambia maduka yalipigwa marufuku pote ni nani au yalikufa kifo cha kawaida kwa kushindwa kupata soko na bidhaa..., wewe unauza machungwa yako kwenge genge alafu kesho inashushwa supermarket yenye bei sawa na bure unadhani uta-survive ?
Ndiyo maana nimekwambia kwenye suburbs, huko hakuruhusiwi maduka na shughuli zingine. Ndiyo maana watu wanalazimika kusafiri kufuata mahitaji yao ya kila siku. Ndiyo hao watumiaji wakubwa wa kununua online na kwenye malls. Maeneo ya mijini watu wanafuata mahitaji yao kwa kutembea tu. Na pia elewa kuwa supermarkets kutaka kuuza vitu sawa na bure ni hatari kwa uchumi, hatari kubwa sana.
Unafundisha ubahili shule ? Uvumilivu ? na kutunza Pesa kwanini usianze wewe kama mzazi kumfundisha mwanao ?

Na aliyosema hayo hayafundishwi sasa ni nani katika nyanja tofauti tofauti ? Mtu akifundishwa business general duka la mangi, genge la nyanya au hata kuuza makahaba sio subset ya biashara ?!!!
 
Kila nyumba kuwa na duka ni jambo zuri. yatakayoshindwa yatafunga. Ni jambo zuri kwa wakazi wa eneo husika na uchumi wa eneo lao. Kwanza sababu kubwa si utapeli, sababu kubwa ni kuwa ni rahisi kununua vitu dukani kwa mangi kuliko online. Kwenye miji mikubwa, ndani mwendo wa dk 5 kutoka makazi ya kila mtu utakutana na duka kubwa la mangi. Niagize kitu online na kwa "mangi" ni hapo nje? Kuna somo refu la ubaya wa hizo supermarkets na madhara yatokanayo na kuweka bei chini kuliko uhalisia, ni somo refu.

Uwepo wa bucha na magenge kila sehemu ni jambo zuri na mipango mizuri ya miji. Mahitaji ya kila siku ya watu yanatakiwa kupatikani umbali wa kutembea. Usidhani kuendesha gari kwenda "madukani" ndiyo mipango mizuri. watu wanataka kutoka huko. Hivyo future ni duka la mangi. Pia hii inafaida sana kwa uchumi wa community.
Moja je ni Vizuri kuwa na Duka kila Mlango: Ulishawahi kuwa na Duka au umeshaongea na mtu mwenye duka mitaa ya Bongo ? Kwa taarifa yako zamani walikuwa wanafurahia sababu wanapata wateja wa kutosha sasa hivi supply ni kubwa kuliko demand (hawana alternative cha kufanya ni mwendo wa kugawana umasikini utasikia wanasema riziki analeta Mungu) Nikupe case study ndogo unayoweza ukarelate.., hapo mwanzo Bodaboda walikuwepo hatua hata ishirini na watu kwa siku walikuwa wanaweza kulala na hata elfu sitini sasa hivi ukitoka tu getini kwako kuna Boda hence watu hata kupata elfu kumi kwa siku imekuwa shughuli.., kwahio supply inabidi iendani na demand na Mipango miji haikupanga kila nyumba ya barabarani iwe frame imetokea tu kwa kuwa na sera mbovu hence watu kudhani tujaribu labda tuuze duka (fanya research ni biashara ngapi zinakufa baada ya mwaka kuanzishwa) au muulize mwenye nyumba kwa mwaka anapangisha watu tofauti wangapi huyu anakuja anajaribu kuuza pombe, mwingine anakuja anaweka betting kesho anakuja anaweza game la watoto ili mradi ni mzunguko usio na tija....

Kwa logic yako tuongeze hata vituo vya taksi, daladala na hata ikibidi kila mtu awe na duka sebuleni kwake ili asiende mbali... (ooh thinking about it kuna alternative ambayo ni simu yake aliyonayo mkononi)
Ndiyo maana nimekwambia kwenye suburbs, huko hakuruhusiwi maduka na shughuli zingine. Ndiyo maana watu wanalazimika kusafiri kufuata mahitaji yao ya kila siku. Ndiyo hao watumiaji wakubwa wa kununua online na kwenye malls.
Hivi unadhani wapanga miji huko wanapanga wakiwa under influence au wakiwa na kilevi kichwani ? Kwa taarifa yako wakipanga miji wanaona na kuweka huduma zote muhimu kwa wakazi ili kuleta convinience tena kipindi cha Post Office kulikuwa karibia na kila sehemu ya Makazi (mfano UK) kuna post office..., kila mitaa miwili kuna Corner shops n.k. (Lakini zote hizo zimekufa kifo cha kawaida kutokana na wakati; nani anatuma barua ?, Pia Supermarkets zinaweza zikaleta mpaka delivery though corner shops bado zipo.....
Maeneo ya mijini watu wanafuata mahitaji yao kwa kutembea tu. Na pia elewa kuwa supermarkets kutaka kuuza vitu sawa na bure ni hatari kwa uchumi, hatari kubwa sana.
Unajua kitu kinaitwa A Broken Windows Fallacy ?!!!! Wewe unaweza kudhani mtoto kuvunja kioo anakuza uchumi sababu muuza mwenye kioo atanunua kipya ambacho kiwanda kitatengeneza kipya n.k. unasahau kwamba mwenye kioo huenda hizo pesa angenunulia viatu jambo ambalo hataacha kununua....

Hence mahitaji ya Binadamu ni Chakula, Malazi na Mavazi kama Chakula kitakuwa bei ndogo sana watu watapata disposable income ambayo huenda wakapeleka kwenye luxuries na vitu vingine..., sio Lazima kila mtu awe muuza duka au mchuuzi anaweza kwenda kulima ili auzie hizo supermarkets
 
Back
Top Bottom