Evody kamgisha
Member
- Aug 4, 2011
- 88
- 95
Hali sio hali nchini hususani kwenye uchumi wa nchi na mauzo na manunuzi. Gharama ya bidhaa iko juu sana, vyakula na bidhaa nyingine iko juu kupindukia. Ukienda kila kona ya nchi hali ni mbaya.
Kodi ni kubwa sana. Watu wanashindwa kufanya biashara. Biashara inafungwa, watu wanahifadhi pesa zao katika mfumo wa dola na kuficha pesa zao na sio Benki bali sehemu nyingine kusikojulikana ili kulinda mitaji yao.
Watu wanafanya biashara, kiwango cha faida katika biashara kimepungua kwa kiasi kikubwa hadi kupelekea watu kupoteza muda katika biashara isiyo na tija.
Ukirudi kwenye ubadilishanaji wa Dola ndo usiseme. Ukienda kwenye maduka ya kubadilishanaji fedha za kigeni, kupata dola ni shida, unawekewa kiwango cha kubadilisha fedha. Zaidi ya hapo hupati huduma.
Thamani ya fedha yetu ya kitanzania inashuka kwa kasi kubwa mno. Linganisha pesa ya Tanzania na Uganda, pesa yetu ilikuwa na thamani kubwa sana dhidi ya pesa ya Uganda, angalia kwa sasa katika exchange rate kwa sasa inaifukuza pesa yetu kwa kasi kubwa. Pesa ya Kenya(KSHS) hatuifati hata kidogo.
Tunakwama wapi katika hili? Tujiulize kama watanzania. Je ni uchumi wa dunia ndo umevurugika? Au ni kuyumba kwa uchumi wa nchi? Au washindani wetu wamekuza chumi zetu?
Mungu ibariki Tanzania