Dr. Chris Mauki vs Kataa Ndoa 2: Feminists wanachangia kwa kiasi kikubwa watu kukataa ndoa. Kwa bahati mbaya sana asili haitakaa ibadilike!

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
631
960
mauki.jpg

JamiiForums ilipata wasaa wa kuongea na Dr. Chris Mauki, Mtaalamu wa Saikolojia, Ndoa na Mahusiano, Malezi na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juu ya suala hili la Kataa Ndoa, mjadala ambao umekuwa mkali sana hasa kwa vijana wa zama hizi.

Kusoma sehemu ya kwanza ya mahojiano haya nenda hapa: Dr. Chris Mauki vs Kataa Ndoa: Je, ndoa ni suala la Kisaikolojia? Ni lazima Uoe? Hayo na mengine mengi yamejibiwa hapa, sogea karibu kushiriki mjadala

--------
Sasa tuendelee muendelezo wa mahojiano haya...

photo_2_2024-05-06_22-20-46.jpg

SWALI: Inasemekana Wafeminia wanachangia kufanya Wanaume wasitake kuoa na Wanawake wasitake kuolewa (Hasa inapotokea Wanawake wakiwa wanafuata misingi hii ya kifemenia). Je, hii suala hili limekaaje kwa upande wako?

JIBU
: Ni kweli kabisa kwamba wafeminia (feminists) wanachangia kwa kiasi kikubwa wanawake au wanawake ambao hawajaolewa kuona hakuna haja ya kuolewa na wanaume ambao hawajaoa wanasita kuwaoa baadhi ya wanawake ambao wameshawishiwa na wafeminia.

Hii ni kwasababu mara nyingi na kwa kiasi kikubwa wanawake ambao wapo kwenye feminism movements kwa kiasi kikubwa inaonekana hata wao wana changamoto za kimahusiano, wamekuwa wakiwashawishi wanawake wengine kutosimama sana kwenye nafasi zao hususani kwenye kuwashawishi kwamba wana uwezo wa kujikomboa, wana uwezo wa kujisimamia utadhani kwenye mahusiano ni jela au kwenye ukoloni na kwamba wanatafuta ufumbuzi au kuwa huru.

Mwisho wa siku ule ushawawishi wao unawafanya wanaanza kuonekana kama wanashindana au wanatafuta kushindana na waume zao. Bahati mbaya sana, asili haitakaa ibadilike. Mwanaume ameumbwa na Mungu anatamani kuona heshima/submission kutoka kwa mwanamke kama vile ambavyo mwanamke anatamani kuona kupendwa na mapenzi kutoka kwa mwanaume.

Huu mbadilishano wa hisia ni wa asili ni ndivyo ambavyo Mungu ameitengeneza. Sasa mwanamke apokuwa na fikra za kutaka kuwa sawa au fikra za kutaka kushindana au kutaka kunyanyua mabega au mahitaji yake kwa ‘kupush’ kwa mwanaume ni Dhahiri kuna mambo yatakayotokea.

Ukatili unaweza kutokea kwa mwaume kutaka kutumia nguvu kumdidimiza huyu mwanamke au akahofia kuwa naye katika mahusiano au kuoa kwasababu anakataa kukutana na hali kama hiyo, na wale ambao wataamua kuona basi kuingia kwenye tabia zitakazomfanya amdidimize yule mwanamke; anaweza kuamua kutoonekana nyumbani, akaamua kuwa ‘reserved’ yaani hataki kuongea, yeye hayupo nyumbani, anajiondoa kwa kiasi kikubwa.

photo_5_2024-05-06_22-20-46.jpg

Mwisho wa siku mwanamke atashindwa ile ndoa na ndoa itavunjika. Infact, hiyo ni sababu ya wengi kutoingia katika ndoa au wengi kuwa na mtazamo hasi na ndoa lakini pia ni sababu ya ndoa nyingi kuvunjika

SWALI: Hali ya maisha inaweza kuwa sababu inayowafanya vijana kupinga suala la ndoa?

JIBU
: Ni kweli ya maisha kwa sasa inaweza kuwa chanzo cha vijana wengi kushindwa kuingia kwenye ndoa, kwsababu;

1. Ni uhalisia wa kwamba wanaume wengi wamekuwa siyo wa kujituma kupata kipato na mwisho wa siku ili kuoa inahitaji kuwa na chochote na sio suala tu la mahari, mahari ni mwanzo lakini uwezo wa mwanaume kuona nitashindwa kuendesha familia yangu, nitanyanyasika na huyu mwanamke kama yeye ana uwezo wa kazi lakini mimi sina. Kwahiyo watu wamekuwa wanahofia kwasababu ndoa imeonekana kuhitaji kipato.

photo_3_2024-05-06_22-20-46.jpg

2. Jamii imekuwa na msukumo mkubwa wa kuonesha kwamba ndoa na mahusiano yanahitaji pesa nyingi. Hili pia linaweza kuwa na ushawishi wa watu rika (peer pressure) kwamba huna pesa huwezi kuingia kwenye mahusiano lakini pia linaweza kuwa limeongezewa nguvu na aina ya wanawake ambao wapo kwenye jamii ambao wapo tayari kutokuangalia mapenzi zaidi lakini wakaangilia peasa. Kwahiyo kuwafanya vijana wengi kuona kama sina chochote siwezi hata kuwa na mpenzi, kama sina chochote siwezi hata kupata mapenzi, siwezi kupendwa, siwezi kupenda na siwezi kuingia kwenye ndoa.

Lakini vile vile suala la kuwa na pesa tunaangalia tu mwanzo lakini hatuangalii inavyoendelea, baadhi ya watu waliofanikiwa (hapa sasa inakuja sintofahamu), baadhi ya watu waliopush na kuzisaka sana hela na wakazipata wakafikiri kwamba baada ya kupata pesa watapata mapenzi wapo wengi, na kwa uzoefu nimekutana na ambao baada ya kufanikiwa basi wakapata wanawake wakakaa nao. Ila wakaja kugundua kwamba......

photo_1_2024-05-06_22-30-44.jpg

Lakini pia wengi wamekuja kuelewa kwamba.......

photo_1_2024-05-06_22-20-46.jpg

Pesa inaweza kumpa mtu, mtu wa kumpenda lakini isimpe hisia za yule ambaye unampenda, na hawa ambao wanapesa wamenza kuchanganyikiwa kwasbababu wamewapa wanawake wao pesa nyingi halafu wakajikuta wale wanawake wameanza kuvutiwa na baadhi ya vijana wengine ambao sasa wanawahisi mioyoni mwao wanawapenda na wale vijana hawana pesa ila ile pesa iliyotoka kwa mwenye pesa inaenda kumhudumia yule ambaye hana pesa sana lakini ana muda wa kutumia, ana uwezo wa kuwa na urafiki na moyo umemgusa au mioyo yao imeendana.

Kwahiyo suala la pesa ni suala mtambuka, linatakiwa liangaliwe kwa pande zote kama vile sarafu zilivyokuwa na pende mbili. Ukiliangalia upande mmoja, umeliwa!

Mpaka kufikia hapa umejifunza nini mdau?

Itaendelea.....

===

Pia soma: Hivi Mshauri wa Saikolojia na Ndoa za watu nchini Tanzania Dkt. Mauki ndiyo kusema yeye ni Malaika na hakumbani na kero zitupatazo?
 
Hapa wanaguswa kabisa Jadda na Dr. Mariposa

Wafeminia wabobevu hapa jf
Mchawi wenu wanaume ni ninyi wenyewe wala msiwasingizie wanawake, tangu mmeanza kuwalalamikia wanawake je mmeona mabadiliko yoyote au ndio hali inazidi kuwa mbaya hasa kwa upande wenu, kwa sababu sasa hivi ninyi ndio mnaongoza kulalamika wanawake wengi wameamua kukaa kimya so mchague ni either muanze kubadilika ninyi au muendelee kulalamika hadi mwisho wa dahari chaguo ni lenu
 
Mwenzio kama endleleas na usingle uone
 
Mchawi wenu wanaume ni ninyi wenyewe wala msiwasingizie wanawake, tangu mmeanza kuwalalamikia wanawake je mmeona mabadiliko yoyote au ndio hali inazidi kuwa mbaya hasa kwa upande wenu, ofcourse hali ni mbaya zaidi kwenu kwa sababu sasa hivi ninyi ndio mnaongoza kulalamika wanawake wengi wameamua kukaa kimya so mchague ni either muanze kubadilika ninyi au muendelee kulalamika hadi mwisho wa dahari
Asili itabaki palepale
 
Asili itabaki palepale
Sawa endeleeni kujifariji na hiyo asili yenu mliyojitengenezea vichwani mwenu sisi sasa hivi tunaangalia uhalisia, mimi nilitegemea kutokana na malalamiko yote haya wanaume wangeshaacha kuoa siku nyingi sana, lakini cha ajabu kila siku ndoa zinafungwa na zitaendelea kufungwa na wanawake wanaoolewa ndio hawa hawa wanaotukanwa kila siku..pathetic!!
 
Wanataka uhakika wa kula K tu wakati wowote wakijisikia
 
Mchawi wenu wanaume ni ninyi wenyewe wala msiwasingizie wanawake, tangu mmeanza kuwalalamikia wanawake je mmeona mabadiliko yoyote au ndio hali inazidi kuwa mbaya hasa kwa upande wenu, kwa sababu sasa hivi ninyi ndio mnaongoza kulalamika wanawake wengi wameamua kukaa kimya so mchague ni either muanze kubadilika ninyi au muendelee kulalamika hadi mwisho wa dahari chaguo ni lenu
Wanawake wana kaa kimyaa ?
 
Ndio mkuu hata hapa jf tu, jaribu kulinganisha idadi ya nyuzi za kulalamikia mapenzi na jinsia nyingine, kati ya wanaume na wanawake ni kina nani wanaongoza
JF mtu akijisikia kuandika chochote anandika tu.

So, far mpaka sasa kwa umri wangu sijawahi kushuhudia makongamano yaliyo kithiri ya wakina baba/wanaume na agenda kuu ikawa kusemwa wanawake.
 
Ya ndani haina gharama kabisa bureeee!
Hapana huwa mnasema ya nini kufuga ng'ombe mzima wakati maziwa mnapata kirahisi, tena wengine wanasema kwenye ndoa wanawake wengi huwanyima sana waume zao hivyo kuoa siyo guarantee ya kuipata kila siku, na wengine wanasema ndoa za siku hizi ni utapeli sababu ya hizi sheria za mgawanyo wa mali zinazowabana wanaume na kuwapendelea wanawake lakini cha ajabu bado wanaendelea kuoa
 
JF mtu akijisikia kuandika chochote anandika tu.

So, far mpaka sasa kwa umri wangu sijawahi kushuhudia makongamano yaliyo kithiri ya wakina baba/wanaume na agenda kuu ikawa kusemwa wanawake.
Mkuu makongamano ya wanawake ni kwa ajili ya kumfunza mwanamke asiwe tegemezi kwa mwanaume, sema ni vile wanaume mnajihami ndio maana mnahisi kama wanawasema au wanashindana na ninyi, mimi naongelea malalamiko ya kwenye uchumba na ndoa kuhusu tabia mbovu ni jinsia gani inayoongoza kuilaumu nyenzake
 
Au sio ? Kwamba mimi sina masikio ya kusikia wanayo ongea ?
 
Back
Top Bottom