Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,747
- 41,080
Kama wiki mbili hivi sikuwa online kwenye social media hivyo nilipata wasaa wa kusikiliza redio zetu hapa nchini.
Katika wiki zote hizo mbili nilikua natune almost radio zote , ila vipindi vingi vya radio zetu vinafanana na sio elimishi, burudani imechukua sehemu kubwa na hasa uchambuzi wa mpira.
Asubuhi radio zote wanasoma magazeti na kuchambua habari. Hapa watangazaji wanatoa maoni binafsi bila kuwa na utaalam wowote wa maswala wanayoyazungumzia. Uwezekano wa kupotosha watu ni mkubwa sana. Haiwezekani mtu ukawa na ufahamu wa kila kitu, ndio maana media za nje huwa wanaalika wataalam kuzungumzia jambo kulingana na taaluma zao.
Baada ya vipindi vya magazeti, radio zote wataanza kuchambua mpira, mechi zote za ligi ya ndani na nje zitachambuliwa hapo ni masaa mawili.
Itafuatia muziki na porojo nyingine mpaka usiku tena, ambapo watarudia tena uchambuzi wa mpira na muziki.
Katika wiki zote hizo mbili na kusikiliza Radio mbali mbali ni siku moja tu nilibahatika kusikia content ya maana, hii ilikua Radio uhuru na walikua wanazungumza na mkurugenzi wa kampuni inayotoa huduma ya kuwapatia watu wafanyakazi wa ndani. Kile kipindi kilikua kizuri sana, na kilitoa mafunzo mengi mno.
Kwakweli naona kuna haja ya serikali kupitia wizara na taasisi zake kuweka miongozo ya content za media zetu otherwise tutakuwa na jamii yenye watu wa hovyo tu.
Haiwezekani siku nzima ni mijadala isiyokuwa na tija inaendelea kwenye media zetu.
Yaani ni mpira tuu siku nzima. Hii haikubaliki.
Unless tunataka tuwe na jamii ya kubet na mpira basi tuendelee namna hii ila kama tunataka kujenga Taifa lenye watu wanaojielewa na wanafanya mambo ya maana na sio wasindikizaji tu , tunapaswa kubadilika.