bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,199
- 2,151
Ni kipindi kirefu kimepita nikiwa nimekwama kuamua yupi ni mahiri zaidi kwenye uandishi wa nyimbo za dini kati ya Bahati Bukuku na Rose Mhando. Kwanza, Hawa wamama wana uwezo wa ajabu katika kutunga nyimbo zenye ujumbe na hisia kali sijapata ona.
Leo ndio siku niyofumbuliwa fumbo langu la yupi ni mahiri zaidi, yupi amekomaa zaidi, yupi matamshi yake yana frequency za kiutu uzima. Hii imetokea wakati nasikiliza wimbo wa Rose - hallow, mstari ulionigusa mwandishi anasema " wagalilaya wakiniona lazima watimue mbio" Pia ndani ya wimbo huo mwandishi kajitamba sana na kumtishia Shetani Sana kwamba atampiga.
Sasa haya mambo yote ni ya kufurahisha watoto, na kuamsha fikra picha tu za kufikirika. Pia, Nikagundua huu wimbo maudhui ni kama yale ya Wimbo wake Secret agenda.
Kwa kuchunguza hizi nyimbo mbili, zinatupa taswira mtunzi anachowaza, kama kumpiga shetani, kumshinda shetani, yeye anapendwa na Mungu. Kwenye uhalisia wa maisha huwezi kutana na shetani ukampiga, huku ukubwani unakutana na watu ambao wengine ni ndugu zetu wa damu, wengine marafiki, hata watu tusiofahamiana wenye kuleta upingamizi katika kupata baraka zako stahiki.
Lakini ukija kwa Bahati unapata maudhui ya aina tofauti. Sikiliza nyimbo kama, Kesho ni fumbo, Maamuzi yako, Ester, Unapojaribiwa, nk. Mwandishi amekomaa haswa, kwa kutumia visa kutoka kwenye Biblia na vya kutunga anafikisha maudhui ya kiutu uzima yanayohusu Ndugu kuishi kwa amani, Uvumilivu, Uthubutu, Imani na mambo mengine.
Kwa herini.
Kesho jumuiya.