Bahati Bukuku ni mama, Rose Mhando Ni kabinti kwenye uandishi

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,165
2,061
Ni kipindi kirefu kimepita nikiwa nimekwama kuamua yupi ni mahiri zaidi kwenye uandishi wa nyimbo za dini kati ya Bahati Bukuku na Rose Mhando. Kwanza, Hawa wamama wana uwezo wa ajabu katika kutunga nyimbo zenye ujumbe na hisia kali sijapata ona.

Leo ndio siku niyofumbuliwa fumbo langu la yupi ni mahiri zaidi, yupi amekomaa zaidi, yupi matamshi yake yana frequency za kiutu uzima. Hii imetokea wakati nasikiliza wimbo wa Rose - hallow, mstari ulionigusa mwandishi anasema " wagalilaya wakiniona lazima watimue mbio" Pia ndani ya wimbo huo mwandishi kajitamba sana na kumtishia Shetani Sana kwamba atampiga.

Sasa haya mambo yote ni ya kufurahisha watoto, na kuamsha fikra picha tu za kufikirika. Pia, Nikagundua huu wimbo maudhui ni kama yale ya Wimbo wake Secret agenda.

Kwa kuchunguza hizi nyimbo mbili, zinatupa taswira mtunzi anachowaza, kama kumpiga shetani, kumshinda shetani, yeye anapendwa na Mungu. Kwenye uhalisia wa maisha huwezi kutana na shetani ukampiga, huku ukubwani unakutana na watu ambao wengine ni ndugu zetu wa damu, wengine marafiki, hata watu tusiofahamiana wenye kuleta upingamizi katika kupata baraka zako stahiki.

Lakini ukija kwa Bahati unapata maudhui ya aina tofauti. Sikiliza nyimbo kama, Kesho ni fumbo, Maamuzi yako, Ester, Unapojaribiwa, nk. Mwandishi amekomaa haswa, kwa kutumia visa kutoka kwenye Biblia na vya kutunga anafikisha maudhui ya kiutu uzima yanayohusu Ndugu kuishi kwa amani, Uvumilivu, Uthubutu, Imani na mambo mengine.

Kwa herini.

Kesho jumuiya.
 
Rose ni mwimbaji wa taarabu hana tofauti na akina Hadija Kopa, Mzee Yusuph, tune za nyimbo zake ni nzuri ila content yake ni masimango, vijembe, kejeli nk, angetumia tune hizo kunukuu vifungu vya maandiko matakatifu basi angewajenga wengi kiimani
 
Bukuku ni storyteller mmoja mzuri sana na anajitahidi kucheza na Bibilia

Rose toka alivyo kengeuka na kurudi kundini amekua na nyimbo za masimango sana kama taarab
 
Ni kipindi kirefu kimepita nikiwa nimekwama kuamua yupi ni mahiri zaidi kwenye uandishi wa nyimbo za dini kati ya Bahati Bukuku na Rose Mhando. Kwanza, Hawa wamama wana uwezo wa ajabu katika kutunga nyimbo zenye ujumbe na hisia kali sijapata ona.

Leo ndio siku niyofumbuliwa fumbo langu la yupi ni mahiri zaidi, yupi amekomaa zaidi, yupi matamshi yake yana frequency za kiutu uzima. Hii imetokea wakati nasikiliza wimbo wa Rose - hallow, mstari ulionigusa mwandishi anasema " wagalilaya wakiniona lazima watimue mbio" Pia ndani ya wimbo huo mwandishi kajitamba sana na kumtishia Shetani Sana kwamba atampiga.

Sasa haya mambo yote ni ya kufurahisha watoto, na kuamsha fikra picha tu za kufikirika. Pia, Nikagundua huu wimbo maudhui ni kama yale ya Wimbo wake Secret agenda.

Kwa kuchunguza hizi nyimbo mbili, zinatupa taswira mtunzi anachowaza, kama kumpiga shetani, kumshinda shetani, yeye anapendwa na Mungu. Kwenye uhalisia wa maisha huwezi kutana na shetani ukampiga, huku ukubwani unakutana na watu ambao wengine ni ndugu zetu wa damu, wengine marafiki, hata watu tusiofahamiana wenye kuleta upingamizi katika kupata baraka zako stahiki.

Lakini ukija kwa Bahati unapata maudhui ya aina tofauti. Sikiliza nyimbo kama, Kesho ni fumbo, Maamuzi yako, Ester, Unapojaribiwa, nk. Mwandishi amekomaa haswa, kwa kutumia visa kutoka kwenye Biblia na vya kutunga anafikisha maudhui ya kiutu uzima yanayohusu Ndugu kuishi kwa amani, Uvumilivu, Uthubutu, Imani na mambo mengine.

Kwa herini.

Kesho jumuiya.
Naona Leo upako Umekushukia Sana. Hongera. Ila Naona kama nyimbo za zamani za Rozi mhando zilikuwa na vina vikali Sana
Mafunuo yalikuwa ya hali ya juu sana
 
Bukuku ni storyteller mmoja mzuri sana na anajitahidi kucheza na Bibilia

Rose toka alivyo kengeuka na kurudi kundini amekua na nyimbo za masimango sana kama taarab
Walishaachana na Mungu sasa anafanyia uzoefu. Hana ufunuo tena
Roho Mtakatifu aliyekuwa juu yake Kwa ajili ya huduma alishaondoka
Amebaki na Roho Mtakatifu ndani yake Kama mwana wa Mungu tu
 
Umechagua nyimbo mbili za Rose Muhando kulinganisha na nyimbo kali za Bahati Bukuku.

Ijapokuwa si sahihi sana kulinganisha watumishi wa Mungu katika uimbaji kwa sababu wote wanamtumikia Mungu na nyimbo zao zinamtukuza, ila honestly Rose is miles away kwa Bahati.

Kazi ya mtumishi ni kuwavuta watu wafurahi huku ukipitisha ajenda za kumtukuza Mungu..

Si lazima vifungu vya Biblia vitawale katika wimbo wako, lakini kama inawapa moyo wa kuinuka waliokata tamaa, kuwakumbusha ukuu wa Mungu wale waliokengeuka, kuwapa imani ya kumshinda shetani wanaowaza kushindwa.

Nyimbo nyingi tu za Rose zinaishi na zitaendelea kuishi.

Tafadhali msimu-under rate mtu.
 
Huyu jamaa kazingua Sana lakini tuheshimu maoni yake lakini ukweli utabaki kua ukweli Rose Muhando ndiye mwimbaji na mtunzi Bora wa Gospel Kwa wamama tangu Tanzania ianze..

Kuna Ngoma za Rose ambazo zikipigwa hata sasa hivi utatamani kuokoka...

Hebu leta Ngoma za bahati bukuku zenye utunzi maridadi kuliko hizi za Rose hapa Chini...

Nipe uvumilivu
Wanyamazishe
Nakaza mwendo
Mteule uwe macho
Yesu Nakupenda
Si Salama
Mapambio
Raha
Hatumo
Nibariki

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Rose atabaki kua legend Hadi kiama. Huwezi mlinganisha Zinduna na Mzee tupatupa
 
Hatumo one of my fav. Sasa rosee shida hajabadilika yeye kupiga vijembe tokea enzi hizo
 
Hivi moja ya nyimbo ya huyu Gwiji wa uandishi sio Story za kwenye Bible neno kwa neno ?

Siwezi kuchangia bila kufanya upembuzi zaidi lakini fahamu pia sio mara zote hawa wanaoimba ndio walioandika mara nyingi wana timu za wasaidizi au hata kuandikiwa...
 
Kila mmoja ni mzuri kwa angle yake.

Mhando
Mteule uwe macho ilikuwa mbele ya muda kipindi hicho
Nipe uvumilivu
Kina mama wa leo
Yesu nakupenda
Ndivyo ulivyo
Holini mwa ng'ombe

Bukuku
Ni nyakati za mwisho
Mapito
Ikulu ya Mbinguni
Siri
Nakutegemea
Tutakaposimamishwa kizimbani pale

Yaani wote wakali aisee,kila mtu na flavor yake
 
Umechagua nyimbo mbili za Rose Muhando kulinganisha na nyimbo kali za Bahati Bukuku.

Ijapokuwa si sahihi sana kulinganisha watumishi wa Mungu katika uimbaji kwa sababu wote wanamtumikia Mungu na nyimbo zao zinamtukuza, ila honestly Rose is miles away kwa Bahati.

Kazi ya mtumishi ni kuwavuta watu wafurahi huku ukipitisha ajenda za kumtukuza Mungu..

Si lazima vifungu vya Biblia vitawale katika wimbo wako, lakini kama inawapa moyo wa kuinuka waliokata tamaa, kuwakumbusha ukuu wa Mungu wale waliokengeuka, kuwapa imani ya kumshinda shetani wanaowaza kushindwa.

Nyimbo nyingi tu za Rose zinaishi na zitaendelea kuishi.

Tafadhali msimu-under rate mtu.

Sijamu under estimate , embu niambie ukweli, wimbo wake Nibebe ukiusikiliza au kwa uhalisia unaweza taka yesu akubebe au utake yesu akuongoze.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom