Ajali za barabarani ni matokeo ya nidhamu mbovu ya madereva

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
139
179
Nianze kwa kutoa salaam na heri za mwaka mpya kwa jamii ya wanajamii forum wote.
Baada ya Salaam nirejee kwenye mada husika, Kwa siku za hivi karibuni ajali za barabarani zimekuwa tatizo na kichwa cha mwendawazimu, tumepoteza ndugu, Jamaa na marafiki kwa sababu ya ajali ambazo pengine zinaepukika na wala si kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, bali kwa mapenzi ya "madereva wahuni"

Zipo sababu za msingi ambazo mamlaka husika wanapaswa kuzimulika ili kupunguza janga hili, sababu hizo ni pamoja na; Mosi, Nidhamu mbovu ya madereva wawapo barabarani, Madereva wengi utumia simu janja 'smartphone" kufanya mawasiliano na aidha marafiki, ndugu au wenza wao huku wakiendesha vyombo vya moto.

Pili, Utumiaji wa vilevi kama, Pombe na madawa ya kulevya mfano: Bangi, Mirungi na Ugoro ni sababu kubwa inayochangia madereva walio wengi kushindwa kumudu vyombo vya moto na hivyo kusababisha ajali na kusababisha vifo na majeruhi.

Tatu, Msongo wa mawazo na mfadhaiko kwa baadhi ya madereva upelekea kusababisha ajali, Mara kadhaa nimeshuhudia madereva wengi wakiongea peke yao huku wakisikitika na kunungunika juu ya aidha ugumu wa maisha au uwepo wa migogoro ya kifamilia kati ya dereva na mke, au mchepuko wake.

Nne, Rushwa, Miundombinu mibovu ya barabara, ubovu wa magari, upatikanaji wa leseni kinyume na utaratibu na sheria za nchi, kutojali utu, ukosefu wa hofu ya Mungu na imani za kishirikina ni sehemu ya sababu zinazochangia madereva wengi wa Tanzania na bara la Afrika kusababisha ajali zinazogharimu uhai wa binadamu, Wakati ni sasa, Taifa na Watanzania kushikamana na kukemea madereva wanaokiuka miiko ya udereva.

Watanzania tupaze sauti, Tupaze sauti, Tupaze sauti, wakati ni sasa, tusipofanya hivyo tutakwisha na kuachwa na ulemavu wa kudumu kwa sababu ya uzembe wa mtu mmoja, ambaye anaitwa dereva.

Aidha ni wajibu wa serikali kuwachukulia hatua stahiki na kali sana madereva wote wahuni wanaoenda kinyume na sheria na utaratibu wa usalama barabarani, ni wakati sasa wa kutungwa sheria kali inayozuia matumizi ya simu wakati wa utumiaji wa chombo cha moto, sheria hii ije sasa na ndio wakati wake.​
 
Tulisha shauri kikosi cha usalama barabarani kifumuliwe, waliopo wanafanya kazi kwa mazowea.
Walicho nacho kichwani ni shilingi ngapi zitaingia mifukoni jua likizama.
Tulishauri muwekeni Afande Thiopista ambae sasa ni Rpc Songwe.
Wakati akiwa staff one traffic huyu mama alifanya kazi ya kutukuka.
Ulikuwa ukiwa na changamoto barabarani, ukipiga simu haipiti sekunde ameshaookea na kutatua tatizo kulingana na mahali ulipo.
Hivi sasa utapiga simu hadi una kata tamaa na haina majibu.
IGP ana takiwa kusikiliza vilio vya Watanzania.. Hebu tujiulize hivi leo, ni nani mwenye namba ya staff one? Ni nani mwenye namba ya mkuu wa kitengo cha trafic makao makuu??
Kipindi cha Thiopista namba zilikiwa kula mahali.
 
Ajali za barabarani zimekuwa nyingi siku za hivi karibuni baada ya kupungua sana enzi za mtemi Joseph Pombe Magufuli. Haipiti wiki au mwezi bila kusikia ajali za barabarani.
Kwa kuwa ajali zote kwa asilimia 80 zinatokana na makosa ya kibinadamu, nashauri Jeshi letu la usalama barabarani liige mfano wa Rwanda, ambao wamesimika kamera kando ya barabara kudaka matukio ya uvunjaji wa sheria za barabarani, unaopelekea kwenye hasara ya mali na uhai watu.
Nchini Rwanda, kutoka Rusumo hadi Kigali ukiwa mdadisi utaziona kamera kadhaa kando ya barabara. Kutoka Kigali hadi Gisenyi njia nzima kando ya barabara zipo kamera, Kigali hadi Bugesera ni vivyo hivyo. Tanzania nchi kubwa ambayo hivi sasa inajenga barabara za Kigoma Katavi Bukoba na Tabora, nashauri barabara mnazojenga sasa na barabara zote kuu mijini na mikoani, fungeni hizi kamera kwenye maeneo yote hatarishi. Achaneni na utaratibu wa sasa wa kuwaanika matrafiki juani au kuwaficha vichakani, nendeni na usasa Artificial intelligence....Rwanda wako smart kuliko Sisi....Kwa Nini?
2-f83a04c51a.jpeg
 
Back
Top Bottom