Heparin
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 153
- 577
"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli"
"Sheria tuliyokuwa nayo ya uchaguzi ambayo ilitupeleka kwenye uchaguzi wa 2015 iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia bungeni, sheria hiyo hiyo iliwezesha karibu asilimia 40 ya madiwani kuingia kwenye nafasi za halmashauri, tulipokuja 2020... msema kweli lazima tuseme kweli"
"Hofu ya watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, msingi wa hofu yao ni yale yaliyotokea 2019/2020. Niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi mwaka huu na mwakani mtaachwa wapiga uamuzi wao utoe tafsiri ya uchaguzi" - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Chanzo: EATV