Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,508
8,129
Kesi namba 16 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Wabunge 19 wa viti maalum wa CHADEMA kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea Mahakama Kuu.


Kaa nami kujua yatakayojiri Mahakama Kuu, Dar.

==========

Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.

Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.

Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.

Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.

Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
  1. Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
  2. Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
  3. Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
  4. Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.

Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.

Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
  1. Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
  2. Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
  3. Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
  4. Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
  5. Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
  6. Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.
Mawakili wa wabunge 19 na Wanasheria Serikali wanaomba wapewe "status quo" Wakitaka Wakina Mdee na wenzake Waendelee Kuwa Wabunge mpaka Kesi ya Msingi itakapo malizika Kusikilizwa.

Yanasubiriwa maamuzi ya Jaji

Jaji Mgeta ametoa zuio la Muda, "Status quo" Wakina Mdee Waendelee Kuwa Bungeni mpaka tarehe 13 June 2022 ambapo nyaraka zitapelekwa Mahakamani ambapo Kesi zote mbili zitaendelea Kusikilizwa

Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu
 
CDM mliwatumia watoto wa watu kina mdee kuitukana serekali ya ccm kwa kipind lirefu Leo mnakuja kuwataka kuwafukuza Kam mbwa hpn huo ndio uhun
Mdee kanyaga twende
Sawa goroko ndio waneshatimuliwa acha wabebwe na wanachua chako mapema
 
Kama mada inavyouliza. Huyu mtu yupo kweli? Na Kama yupo je anajua kazi yake kweli?

Ni vigumu kuamini kuwa katika suala hili la wabunge 19 fake Kama huyu mtu anafanya kazi yake kuisaidia serikali au ni serikali ndiyo haimtumii au inamdharau
Ni yule Jaji wa mchongo
 
Kama mada inavyouliza. Huyu mtu yupo kweli? Na Kama yupo je anajua kazi yake kweli?

Ni vigumu kuamini kuwa katika suala hili la wabunge 19 fake Kama huyu mtu anafanya kazi yake kuisaidia serikali au ni serikali ndiyo haimtumii au inamdharau
Weledi wa kitanzania 🤔
 
Tupo awamu inayotenda haki. Tusihangaike ku-influence kwa namna iwayo yote hukumu ya mahakama. Tuwaachie mawakili na wanasheria wafanye kazi zao.
Kabisa umeongea kwa kushirikisha ubongo wako hapa,mahakama zetu zipo huru really??bila shaka mkuu bado unaishi nchi ya mazuzu, but definitely mimi sio zuzu
 
Back
Top Bottom