Abdul anatuhumiwa kwa kugawa rushwa mama yake Yuko kimyaMakamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.
Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.
Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.
Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.
Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.
Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.
Pia soma
Haya ndo mambo huangusha watawala natawala