Kuelekea 2025 Tundu Lissu: Abdul (mtoto wa Rais Samia) alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
Dogo ndo umekuja mjin Jana? Takukuru which?
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Huyu kijana Lissu si wa kumwamini kabisaa. Ni mropokaji tu
 
Shida Mbowe kakaa kibiashara biashara. Na ukiona Lissu hajataja atakuwa yeye au Mrema. Ndio maana Kuna kamvutano fulani. Siasa hii nchi ujinga kabisa wananchi tusipoamua wenyewe tukategemea Hawa tumepotea
 
Angeenda aone maana alimsimanga wakati huyo kijana alienda Uganda kuiwakilisha nchi.
 
S

Sio kweli unachosema.

Mtu anakamatwa ukiwepo ushahidi wa kutosha usio na shaka sio mradi fulani karopoka basi mtu anakamatwa.

Pili mtu anapotaka kutoa rushwa anachukua tahadhari zote. Huenda Allienda nyumbani kuzungumza kwanza terms wakishakubaliana terms ndio rushwa itatolewa baadae. Huwezi kubeba hela katika kapu wakatii hujui zitatakiwa pesa,kiasi gani. Pia rushwa inatolewa kupitia maajenti ili kuondoa uwezekano wa kuzungukwa ikawa skendo.

Ilo siku itajulikana tu walishindwana wapi, je dau lilikuwa dogo au hawajashindwana ila muda wa kuondoka haujafika?

Na kama ni kweli basi dau hilo hilo linaweza kugawanywa kwa wapiga kura wa uchaguzi ndani ya chadema kisha wakamchagua mtu nwingine badala ya lissu katika hizo nafasi ya makamu mwenyekiti na ya. Mgombea urais ili kutrigger Lissu kuhama.
Je ni kweli ushahidi haupo
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Anakataa pesa ila za kuchangiwa ndio anataka si ndio? 😂😂😂😂
 
hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
😂😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣😁😁😁😆😆
 
Cha msingi alipelekewa hongo asigombee......mwaka huu kitawaka.

Nguvu ya Lissu iko Wazi 2025 Patachimbika.

Kwanini wanahangaika kumhonga? Ina maana wanaamini Lissu anaweza kushinda kwa Kura?

Time will tell
Nguvu yake iwe kubwa au ndogo hawezi kushinda na hakuna kitu mtafanya
 
Kwa muhitasari:

Tundu Lissu: "aliwatumia watu wema wa chama changu. Na kwanza aliniomba tukutane katika hotel moja sijui inaitwaje huko maeneo ya Masaki, DSM...."

Tundu Lissu: "Nikawaambia mwambieni kama ana shida na mimi wamlete nyumbani kwangu. Walimleta na tulikaa hivi hivi face to face kama tulivyokaa mimi na wewe hapa mwandishi"

Tundu Lissu: "Alisema anataka kunisaidia. Nikamwambia kama kweli unataka kunisaidia, mwambie mama yako ambaye ni Rais alipe pesa zangu za matibabu zenye risisti. Hizi za kwako ni hongo, hazina risiti"

Tundu Lissu: "Akasema, ooh, mama (Rais Samia) analalamika hujawahi kumwandikia kuomba hizo pesa. Nikamwambia nilishaandika mara mbili. Pamoja na hayo nilimpa nakala ya madai yangu, nikamwambia si anasema sijamwandikia? Mpelekee barua yangu ya madai nakala hii hapa. Mpaka leo kimya, hajawahi kuwasiliana nami tena......!"

Tundu Lissu: "Kwangu hakuna CCTV cameras. Lakini sikiliza, nafahamu mimi ni mwanasheria. Na katika sheria ya ushahidi, ushahidi ulio bora kabisa kisheria ni ule wa mtu kuona, kusikia, kushika na kunusa mwenyewe. Mimi niliona mwenyewe. Zaidi pia ni kuwa katika mazungumzo yale, tulikuwa na watu wanne jumla ndani/au mahali tulipokuwa na huyo mgeni na huko nje kulikuwa na walinzi wa kutosha"

Kwa uelewa zaidi, tumia bundle lako kumsikiliza na kumtazama mwenyewe hatua kwa hatua hadi mwisho...
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Kwa njaa ya Msigwa angezichukua fastaa!!
 
Back
Top Bottom