Tangu Mungu amuulize Adamu, Adamu uko wapi? Wanaume hatupendi kabisa kuulizwa hilo swali

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
5,827
11,836
Ukweli ndo huu mara tu tukiulizwa swali hili upo wapi? maswali huwa ni mengi sana kichwani.

Ukiwa sehemu hatarishi hapo sasa ndo wasiwasi unakuwa mkubwa unajiuliza hivi kaniona au kaambiwa nilipo.

Inaweza chukua dk1-2 kujibu swali hili mazee.Mara nyingi huwa ni mtego usikurupuke kujibu kama uko
eneo tatanishi mazee.

Imagine Mungu mjuzi wa yote na mwenye uweza wote nikweli alikuwa hamuoni Adamu alipokuwa amejificha? jibu alikuwa anamuona ila ni mtego tu.

kuwa makini kujibu swali hili hasa akiuliza wife /mchepuko!
 
Adamu upo wapi? 😃😃
Huyu Mwanamke.."
Jamaa hakujibu swali
Yaani hapo ukiingia deep lazima ujiulize maswali mengi sana inamaana yote Mungu alikua anasubiri yatokee kwanza kisha aje kuwasambaratisha? Maana Mungu ni muweza wa yote sasa alishindwaje kumzuia Shetani asimpe Mwanamke tunda pale bustanini kwanini Mungu hakuzuia jambo hilo lisitokee? Inamaana Mungu aliweka mtego makusudi kisha akasubiri wanase?
 
Yaani hapo ukiingia deep lazima ujiulize maswali mengi sana inamaana yote Mungu alikua anasubiri yatokee kwanza kisha aje kuwasambaratisha? Maana Mungu ni muweza wa yote sasa alishindwaje kumzuia Shetani asimpe Mwanamke tunda pale bustanini kwanini Mungu akuzuia jambo hilo lisitokee? Inamaana Mungu aliweka mtego makusudi kisha akasubiri wanase?
Kah! kwani wao walishindwaje kutii alichowaambia?
 
Wasingeweza kutii walichoagizwa, maana waliletewa shetani awajaribu.
Na kipindi hicho shetani alikuwa moto sana wasingeweza kuzuia moto wake.
uwezo walikuwa nao, kwani sasa hivi shetani sio moto? uwezo ulikuwa ndani yao ila waliamua kumsikiliza ambaye hakuwaweka pale wala kuwapa maagizo yoyote, yaani ni sawa na dada wa kazi anayeshawishiwa na jirani aache kazi kwa Boss wake aliyemtoa kijijini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom