Tangu Mungu amuulize Adamu, Adamu uko wapi? Wanaume hatupendi kabisa kuulizwa hilo swali

Tatizo hakuna,sababu nishatoa....
Ni sawa na kujua mchepuko wa mkeo then unamuuliza mke...hivi wamfahamu mtu fulani.....jibu lake ndiyo litakupa uhakika wa kiburi na hatari ya mkeo
Wanaume wachache sana wanaweza kufanya hivyo. Majority ni kitu chenye ncha kali straight away.
 
Yaani hapo ukiingia deep lazima ujiulize maswali mengi sana inamaana yote Mungu alikua anasubiri yatokee kwanza kisha aje kuwasambaratisha? Maana Mungu ni muweza wa yote sasa alishindwaje kumzuia Shetani asimpe Mwanamke tunda pale bustanini kwanini Mungu hakuzuia jambo hilo lisitokee? Inamaana Mungu aliweka mtego makusudi kisha akasubiri wanase?
Kwa wanaoamini inasemekana Mungu ndiyo hupanga(mapenzi ya Mungu) hivyo yote hayo aliyapanga(if you're a believer) na adhabu alishaziandaa unless tuambiwe kuwa kuna vitu/mambo yako nje ya uwezo wake.
My question: Hilo 'tunda' ni kitu gani/ni tunda la mti gani huo uliokuwa 'katikati ya bustani' ya Aden.
 
Kwa wanaoamini inasemekana Mungu ndiyo hupanga(mapenzi ya Mungu) hivyo yote hayo aliyapanga(if you're a believer) na adhabu alishaziandaa unless tuambiwe kuwa kuna vitu/mambo yako nje ya uwezo wake.
My question: Hilo 'tunda' ni kitu gani/ni tunda la mti gani huo uliokuwa 'katikati ya bustani' ya Aden.
Kwa hio yooote yaliyotokea ni mipango yake mwenyewe yaani aliumba mchongo uwe hivyo na ukawa km hivyo si ndio? Basi km ni Mungu alipanga kila kitu binadamu hana kosa ni mipango yake yeye mwenyewe kapanga Hawa ale tunda akalila akapanga liliwe na yule Adamu ikawa hivyo akapanga kuwatimua bustanini ikawa hivyo, tunda wanalolisema halipo kwenye ulimwengu huu limefungiwa
 
Ukweli ndo huu mara tu tukiulizwa swali hili upo wapi? maswali huwa ni mengi sana kichwani.

Ukiwa sehemu hatarishi hapo sasa ndo wasiwasi unakuwa mkubwa unajiuliza hivi kaniona au kaambiwa nilipo.

Inaweza chukua dk1-2 kujibu swali hili mazee.Mara nyingi huwa ni mtego usikurupuke kujibu kama uko
eneo tatanishi mazee.

Imagine Mungu mjuzi wa yote na mwenye uweza wote nikweli alikuwa hamuoni Adamu alipokuwa amejificha? jibu alikuwa anamuona ila ni mtego tu.

kuwa makini kujibu swali hili hasa akiuliza wife /mchepuko!
Ukiishi kwa kumpendeza Mungu huwezi chukia hilo swali.
Acha uzinzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom