Swali, Youtube huwa wanalipa kutokana na nchi uliosajili chaneli yako?

Hivi hata hizo bongo series zinapitia mgongo ule ule. Kwa sasa kuna watengeneza films wengi wanaweka series zao YouTube na ukiangalia mahadhi yake unaona kuna investment imetumika kutengeneza. Je inawalipaje?...

Nakumbuka inasemekana urefu wa video unachangia, mfano video ya dakika tatu na film ya dakika 30.. Filamu zinapokea zaidi per view

Lakini pia hata quality ya video na content yake..

Je vigezo hivi vipo sahihi na kama kuna vingine ni vipi mkuu
Video refu ina double impression . Tangazo linaweza kutokea zaidi ya mara mbili. Hivyo video refu inalipa kuliko video fupi
 
Hivi hata hizo bongo series zinapitia mgongo ule ule. Kwa sasa kuna watengeneza films wengi wanaweka series zao YouTube na ukiangalia mahadhi yake unaona kuna investment imetumika kutengeneza. Je inawalipaje?...

Nakumbuka inasemekana urefu wa video unachangia, mfano video ya dakika tatu na film ya dakika 30.. Filamu zinapokea zaidi per view

Lakini pia hata quality ya video na content yake..

Je vigezo hivi vipo sahihi na kama kuna vingine ni vipi mkuu
Video ndefu kuna watu wanaweka matangazo mengi, unakuta Video ina dakika 30 kila dk 5 kuna Tangazo, matangazo 7 hayo.

Pia kuna Watanzania wapo Ughaibuni wanaangalia hizo video, nao wanachangia kipato kikubwa.
 
Naona 5000 zimekutoa roho, ukiingia huko kwa motive ya hela utaona watu kama waongo
Umeongea kweli kaka!
YouTubers wengi wa bongo wamekosa ubunifu na hawafanyi investment ya kutosha.
Sio tu kuwekeza pesa, bali uwekezaji wa muda na maarifa ni muhimu mno ili kuwa youtuber mwenye mafanikio!

Hapa tz asilimia kubwa ya YouTubers wanaigana, kila mmoja anadeal na entertainment, udaku na asilimia kubwa wanazalisha maudhui ya uongo!

Badala ya kuzingatia ubora wa contents, wao wako bize kuandaa fake thumbnails.

Kiufupi bado safari ni ndefu, tamaa na matarajio ya muda mfupi.. yamewafanya vijana wengi waishie njiani!
 
Fanya kazi mkuu hela.ikukute mbele. Nunua camera nzuri chagua niche, tengeneza, maudhui mazuri , kuwa na mwendelezo nadhan matunda yatakufuata. Ukianza kwa lengo la kupata pesa utafanya self click halafu watakufungia ukose vyote😂
Sawa chief nimekupata
 
Nimeona baadhi ya chaneli za Youtube, zinazomilikiwa na watu wa huko US, Canada, UK, Nigeria, SA n.k ambazo baadhi zina maudhui ya kusaidia wahitaji mbalimbali ili kuvutia watazamaji.

Kinacho nishangaza zaidi, kila video wanazozitoa ni kusaidia tu watu; sasa najiuliza, ina maana huko kwao Youtube inawalipa sana kiasi cha kila video kuwa na maudhui ya kusaidia watu kifedha na mali?

Na kama ni hivyo, wanazipataje hizo fedha? Na huku kwetu, je wanalipwa sawa na hizo nchi zingine?

Leteni majibu​
Wewe subiri kupewa kanga ya siku ya wanawake ushone iwe mwanamke au mwanaume.
 
Sasa kama hauna content niuongo mkuu huwezi kutoboa
Mkuu sijasema kwamba sina maudhui, ya kwangu yapo kikaangoni maana nilisubiri nipate vitendea kazi vyote muhimu so niko jikoni napika najua audience yangu inapenda nn so najua nikianza tu kuweka kazi zangu angalau nina audience na sio kwamba nitakua naanza upya. Maudhui ambayo niliyokuwa nimekwisha pakua sio ya kwangu yana copyrights. Nadhani umenielewa. Kutuboa kupo sana ishu ni kujua niche yako tu
 
Swali zuri. Mm sijaanza kulipwa kwa sababu sina maudhui yangu mwenyewe, niliyonayo ni miliki ya watu wengine
Kwa mfano, nikiweka maudhui ya kwenda kuwinda mbugani; inaweza kuchukua muda gani kuanza kupata malipo?
 
Kwa mfano, nikiweka maudhui ya kwenda kuwinda mbugani; inaweza kuchukua muda gani kuanza kupata malipo?
Hayo ni maudhui mazuri sana kwa wewe kuanza kupakia YouTube. Ishu ya itakuchukua muda gani hapo inategemea na umakini wako ktk kutengeneza kazi zako, ubora wa content zako, engagement yako kwenye social media pamoja na kasi yako katika kupakia hizo kazi zako. With time you gonna gain massive. Kumbuka ku-build YouTube channel ni suala moja, kuanza kulipwa ni suala lingine.
 
Back
Top Bottom