TATIZO LA UPATIKANAJI WA MAJI NA WIZI KATIKA ANKARA ZA MAJI
Ramadhan Kingi
Nianze upya tena safari ya kuwakumbusha BUWASA kwamba kuanzishwa kwao ni kwa sababu Serikali ilitaka kuanzisha mahusiano ya haraka kwa wale wanaohudumiwa.
Serikali ikiuona umuhimu huo kwa kuanzisha mashirika kama EWURA, SUMATRA, TRL na mengine ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
Kinyume chake mashirika mengine yamekuwa hayafanyi kazi ya huduma kama lengo la Serikali! Tunafahamu kabla ya kuanzishwa Serikali kupitia Wizara ilikuwa ikitoa huduma kama hizo!
Ajabu ni kwamba mashirika hayo yamekuwa yakisubiri Wananchi watoe mashtaka dhidi yao mbele ya viongozi! Mfano mkubwa kwa Kagera ni hili shirika la BUWASA. Hawa BUWASA ni wepesi kuleta ankara za maji zikiwa na bei ya ajabu ajabu kila mwisho wa mwezi lakini bika kuhakiki kama wametoa huduma. Kabla ya kuleta mradi wa Wahindi hapa Bukoba watu tulipata maji kwa bei ya uhakika na bila kuikosa huduma.
Leo ni ajabu baada ya mradi mpya wa Wahindi tumekuwa hatupati huduma kama mwanzo! Niseme tu mafundi hawa wamesaidia kuharibu mfumo mzima wa maji hapa mjini!
BUWASA kwa mazoea tu hawatoi taarifa kwa nini hatupati maji hata baada ya kuleta marekebisho yao mapya! Walichojaliwa sana ni kushirikiana na EWURA kupandisha gharama za maji katika mfumo waliouharibu.
Tunamwomba Mhes. RAS afuatilie kwa nini wamepandisha gharana za maji ilhali wakijua kwamba maji yenyewe hayapo!
Tangu wamechimbachimba na kuweka hizo paipu za maji sasa hatupati maji kama iluvyokuwa mwanzo!
Imekuwa ni baraka kwao ikifika mwisho wa mwezi kuleta ankara za kupikwapikwa na tishio la kukatia watu maji!
Kama wao hutishia kuyajata maji sisi tunaoyahitaji maji hayo na hatuyapati tuchukue hatua ipi? Kabla ya mfumo maji nyumbani kwangu tangu mwaka 1992 maji hayajakatika!
Leo kwa mfumo mpya tena eti wa kisasa wa digitali maji hayapatikani kabisa. Wakileta ankara zao unabaki ukijiuliza hivi nyumba yenye watu wawili na mtoto kuweza kutumia units saba kwa mwezi. Nasikia kila uniti ni sawa na ujazo wa mapipa kumi. Nyumba hiyo itatumia ujazo wa mapipa sabini. Utafikiri kaya hiyo wana mradi wa kuosha magari!
Swali je tusipopata maji twende wapi ikumbukwe kwamba tuna mkataba! Kwa hali hiyo tusipende kufikishana Mahakamani. au?
BUWASA iko chini ya himaya ya Katibu Tawala wa Mkoa Tusubiri tu waje Viongozi wa Kitaifa tutoe malalamiko yetu.
Tangu mwezi wa nane tumekuwa tukipata Huduma hii kwa kuomba. Lakini ajabu ukipata Ankara zao utafikiri umewekeshwa fedha! Unit nane ama tisa kama maji yalikuwepo muda wote
Tunaomba mawakili watusaidie tuwafikishe mahakamani kwa Huduma hafifu
Edith Ntagalinda
Umenena mzee Wangu Ramadhani Kingi mi mwenyewe kwangu watu wawili tu lkn mahesabu ya units zilizotumika toka wameingia hawa wahindi sijawahi kuzitumia toka nimeanza kutumia huduma ya Buwasa,alafu gharama Za unit zinachange kila mwezi!je tuelewe lipi? Basi tujuzwe wapi tupeleke malalamiko yetu?maana kesi ya mbuzi kumpelekea fisi nayo matatizo
Jovin John
Kwakweki mi nimechoshwa NA BUWASA mwezi Jana nililipa sh.26500 elf mwezi huu nimelipa sh.32450 je Unafuu upon wapi? Kiukweli maji hatuyapati kabisa bac kamandivyo ata bills tusipewe make mi sioni ninachokilipia mbona tunateseka utadhani hatukuzaliwa?acheniizo.
Ananis Rushojo
Wanafanya kazi kwa mazoea bili sijui wanatuletea za hewani maji hakuna bili kubwa haya ni majipu ya kansa