The Great Haya
JF-Expert Member
- Apr 6, 2014
- 1,773
- 1,659
4 years no update, viongozi waone aibu,WEBSITE YA BUKOBA MUNICIPAL COUNCIL
Website updated 2012, taarifa zote zilizopo na matangazo yaliyoandikwa 'NEW' ni ya 2012. Taarifa ya idadi ya watu ni ya sensa ya 2002 . Website haijui hata kama uwanja wa ndege ulishapanuliwa na kwasasa una lami, manispaa haijui hata kama kuna ndege zinatokea dar na kuja moja kwa moja Bukoba.
Yeyote anayetamani kuwekeza Bukoba akifungua website yetu haangalii hata mara mbili anakua keshaghairi. Sijui tunatangaza vipi fursa zilizopo, sijui tunatoa taarifa kwa wananchi wetu kwa njia gani
Idara ya IT
TUONE WENZETU WA IRINGA, MOROGORO NA KINONDONI WANAFANYAJE
NA TUONE BASI ENTEBBE WAMEFANYAJE
Kuna vitu huonekana kuwa vidogo sana lakini vina maana kubwa kiuchumi, tusivipuuze. Tutengeneze website yetu ya Bukoba Manispaa kibiashara ili kuvutia uwekezaji na kutoa taarifa kirahisi kwa wananchi. Wananchi wanaotumia mtandao ni wengi sana
Bukoba Kazi, Amani na Maendeleo